Unakaribisha maoni ya nini wakati majibu na hitimisho umefanya kabla hata ya kuleta mada yako!
Hakuna kitu kibaya katika siasa kama unafiki na ndumila kuwili.
Ni katika unafiki kama huu ndiyo maana tulisikia baadhi ya wanasiasa wakijitahidi kumsafisha kisiasa mwanasiasa ambaye wao wenyewe walianza kutueleza kuwa ni fisadi papa na wakaendeleza kusisitiza kwa miaka zaidi ya minane lakini siku ambayo lupia ilipenyezwa, wakawa wa kwanza kuyakana maneno yao kinafiki.
Haishangazi UKAWA ni kati ya wale walikuwa wanasema huyu mwanasiasa ni fisadi papa lakini nitampa kura yangu!
Kupambana kihoja na Serikali ya Rais Magufuli lazima kwanza ujivike ujinga au upumbavu kama wewe siyo mpumbavu au mjinga!
Kwa sasa hata wajinga pia wamekuwa wachambuzi wa mambo ya kisiasa kuhusu utendaji wa serikali ya Rais Magufuli!
Wapumbavu wameamua kujilipua ili upumbavu wao ufahamike kwa wengi hapa Jamiiforums!
Wengine kwa sasa wanatafuta shule zinazofundisha ujinga ili wakasome na wapate hoja za kuweza kupambana na utendaji wa serikali ya Rais Magufuli!
Awamu hii ya tano tutaona na kusikia mengi!
Naamini umejibu/kuchangia hii mada kwa kukurupuka!,laiti ungejipa muda wa kutafakari na kuvuta pumzi ya kutosha ili kuruhusu hewa safi iingie kwenye mapafu yako,wala usingeandika haya uliyooyaandika.
Tusiwe wepesi wa kusahau na kuwa walipukaji mithiri ya gesi pale tunapoona hoja kinzani.Ninayaandika haya nikiwa na kumbukumbu sahihi,laiti miaka 10 au 5 iliyopita nchi yetu ingekuwa imeongozwa na serikali ya chama tofauti na hii ya Magufuli,hakika ungekuwa na haki ya kupaza sauti na uthubutu wa kukemea ubadhirifu wa serikali iliyotangulia.
Maovu yote ambayo tunaweza kuyaorodhesha hapa yaliyolikumba Taifa letu,chanzo chake ni utendaji na utekelezaji usioridhisha wa wale tuliowapa dhamana ya kuongoza Taifa letu.Tangu Magufuli akalie kitu cha Ikulu,ni eneo moja au mawili aliyoyagusa lakini Taifa limeshuhudia ubadhirifu wa kutisha kiasi cha watu kuhoji kama Tanzania ilishawahi kuwa na serikali hapo awali.
Kama eneo moja limetupa picha halisi ya namna watu walivyokuwa wanashirikiana na maafisa wa Serikali kuliibia Taifa,vipi maeneo mengine yaliyosalia yakimulikwa si utaibuliwa ufisadi wa kutosha kiasi cha kuweza kuwafanya Watanzania "wazimie mioyoni"?
Yaliyobumbuluka Bandarini yanaweza kuwepo katika sekta zote zilizopo nchini.Ulishajiuliza kama haya ndiyo yaliyokuwa yanafanyika huko bandarini,vipi kuhusu sekta Kubwa kabisa hapa nchini ambayo ndiyo inayoongoza kwa kutengewa bajeti Kubwa na kuwa na miradi mingi ya ufadhiri?Namaanisha sekta ya ujenzi hususan ujenzi wa barabara.
Tufike mahali tukubaliane kama Taifa kuwa tumefikishwa hapa na tuliowapa dhamana ya kuliongoza Taifa letu,kama tatizo la msingi la ubadhirifu ndani ya Taifa hili alikuwa ni Mh.Lowassa,mheshimiwa huyu alikuwa nje ya serikali kwa zaidi ya miaka 8,kama yeye ndiye S.I. Unit ya ubadhirifu nchini na alikuwa nje ya mfumo wa serikali,nani aliruhusu ubadhirifu wa kutisha ulikuwa unafanywa na makampuni makubwa hapo bandarini?Nani aliyehusika na uhujumu wa uchumi wa kulikosesha Taifa mapato stahiki kwa kuruhusu kuzimwa kwa mita zilizokuwa zinapima kiasi cha mafuta yaliyokuwa yanaingia nchini ili serikali ipate mgao wake wa 50% kwa mujibu wa sheria? Hivi ni nani aliyenyamanzia kuunganishwa kwa bomba la siri kutoka kwenye mitambo ya kupokelea mafuta bandarini na kwenda moja kwa moja Kigamboni bila kupitia vipimo vyovyote?Mradi mkubwa kiasi hicho ulijengwaje ndani ya Jamhuri yetu tukufu kiasi cha wenye dhamana ya kusimamia ujenzi wasijuwe kwamba kuna bomba chini ya ardhi linalochepusha mafuta na kuyapeleka Kigamboni bila kupimwa?
Uozo wa serikali ya CCM hakuna asiyeujuwa,kashfa zilizolitafuna Taifa hili zipo nyingi mno tena zingine zilitokea ikulu.Ni Tanzania pekee ambako Rais anaweza kujigeuza mjasiliamali hadi kufikia hatua ya kufungua Kampuni ya ANBEN tena kwa anuani ya Ikulu na wanaojiita "WASEMAJI UKWELI" wakakaa kimya.
Serikali inayojinasibu kutumbua majipu,kwa nini isianze na wale waliogawana mabilioni ya Escrow hadharani na kuyabeba kwenye viroba mchana kweupe? Serikali yenye vyombo vyote vya ki- intelejensia imeshindwa kufumbua kitendawili hiki,badala yake vyombo vyake vimeishia kukamata vijana waliokuwa wanakusanya na kujumlisha matokeo ya Urais yaliyokusanywa kutoka vituo vya kupigia kura.
Ni kweli tumehitimu darasa ya ujinga na upumbavu kama ulivyotuita,lakini ujinga na upumbavu wetu hautufanyi tusione madhira ya serikali hii hata kama inajaribu kuturubuni kwa mambo machache.Pamoja na upumbavu wetu,bado tunaweza kupaza sauti ya juu kabisa kukemea mazingaombwe ya serikali,haiwezekani serikali ijinasibu inatowa Elimu bure,halafu ipeleke ruzuku ya sh.600 kwa kila mtoto kwa mwezi kughalamia Elimu ya masikini wa Taifa hili,halafu "WASEMAJI UKWELI" wapige makofi na vigelegele kwamba serikali inawajali masikini wa Taifa hili.
Ni bora upumbavu wa "kuhitimu darasani" unaotuwezesha kutambua kuwa sh.600 kwa mwezi kwa mtoto mmoja haziwezi kuwa muarobaini wa Elimu yetu ya msingi,kuliko busara zenu za kipumbavu zinazokubali ghiliba za aina hii.Hivi ni kweli katika hali ya kawaida kabisa ruzuku ya sh.600 kwa kila mwezi kwa mtoto inaweza kuleta mapinduzi ya Elimu ndani ya Jamhuri yetu tukufu ya Wadanganyika?Namshukuru Mungu aliyenipa ulofa na upumbavu,lakini akanipa pia uwezo wa kutambua ghiliba za wanasiasa na wapambe wao.
Kuitetea kihoja serikali ya CCM unapaswa ujitoe ufahamu,uwe zaidi ya msukule.Hakuna hata moja linalotokea leo ambalo halijaletwa/kusababishwa na serikali yenyewe,kuipigia makofi na kuishangilia katika yale iliyoyaumba kwa mikono yake nafikiri ni upumbavu zaidi ya upumbavu wenyewe.