Tukubaliane tu kuwa "Urais" ni kama "Umalaika" hivyo asikosolewe

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,874
Sasa kumezuka dhana ya kutaka kuonyesha kuwa "Urais" ni kama "Umalaika",watu wanataka tuimbe nyimbo za kusifu kiti cha "Urais" kana kwamba ni nafasi ya Malaika isiyokosea.Hawataki watu wakosoe wala kurekebisha,kwa sasa kila linalofanyika ni zuri,limekamilika,hapana hatutafika..Wapeni nafasi watu waongee na kutoa ushauri.Hii ndio dhana ya "Political Prularism",serikali,vyama vya upinzani na Asasi za Kiraia ktk uwanja mmoja wa piga nikupige,na katikati ya hiyo piga nikupige ndipo dhana ya maendeleo yenye uwazi hufikiwa.Kama tunataka kukubaliana kuwa "urais" ni "umalaika" basi wacha mkuu huyu asipate cahangamoto za wakosoaji.

Watu wanafikia hatua hata ya kudhihaki Kituo cha Sheria cha haki za Binadamu,labda ni kwa sababu hautuzisomi reports zao za kila mwaka na za kila mwisho wa Mwezi,Wamekuwa wakiyasemea haya mambo kwa kiasi kikubwa,ikiwa ni pamoja na msongamano wa watu mahabusu,kucheleweshwa kwa kesi za watuhumiwa,kuongezwa kwa posho ya chakula ya wafungwa toka iliyo shilingi 500(?) kwa sasa iwe zaidi ili wapate mazingira mazuri ya chakula,wamekuwa wanatoa idadi ya vifo vya ajali za barabarani na kuonyesha jinsi wananchi wanavyopoteza haki ya kuishi kwa ajali za barabarani

Ukisoma reports zao za kila mwezi na hata zile za mwaka utaona wanaeleza ajali za barabarani na kushauri njia ya kuchukuaa kuzuia ajali hii,hizi report zao wamekuwa wakizipeleka Serikalini na kwenye Taasisi za watu binafsi kuikumbusha jamii umuhimu wa haki za binadamu.

Rais aliyetokana na uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi hana haja ya kushangaa uwepo wa LHRC,Rais anayetamani kufuta na kuondoa uwepo wa "Civil Society" katika nchi iliyokubaliana na mfumo wa "Political Prularism" ni wa kukumbushwa,kwamba dhana ya demokrasia na utawala bora inayoakisi katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni pamoja na kuruhusu vyombo vya habari binafsi kurusha bunge "live" kama TV ya Serikali imeshindwa sababu ya "kubana matumizi".Kuwakatalia waandishi kuingia bungeni na kamera au aina yoyote ya chombo cha kunasa sauti na picha ni kukandamiza dhana ya "Uwazi na utawala bora".Maendeleo ya kweli hayaji katikati ya jamii yenye manung'uniko na woga wa kinafiki.Maendeleo ni pamoja na kukosoana kwa kuheshimiana


LHRCWana Kipindi maalumu Channel Ten ambacho huelezea maswala mbalimbali ya haki za binadamu na namna ya kuzitatua,huelezea kwa kina migogoro ya ardhi na namna ya kuitatua,na wakati mwingine wao wamefika "remote areas" maeneo ambayo serikali imeshindwa kufika.

Ni kweli tunampenda Rais,ni hakika Rais amerudisha imani kwa watu uliyokuwa imepotea kwa serikali kwa muda mrefu,lkn imani hii na kasi hii isitufanye tumuone Rais ni "Malaika" ukizingatia kwamba aamezungukwa na watu ambao ni sehemu ya madudu yaliyolalamikiwa.Tumkumbushe kwa pamoja Mh.Rais kuwa nia yake ni njema,hivyo yote yaliyo na nia njema katika nchi hii tuyaweke katika mfumo wa kisheria ili hata nchi akija kuchukua yule asiye na nia njema abanwe na utaratibu wa kisheria tuliyojiwekea.Sio kila mtu atakuja na nia nzuri kama ya Rais wetu mpendwa.Tujenge mfumo wa kisheria katika yote tunayotaka kusawazisha ambapo huko nyuma kuna watu walikosea.Wenye Lugha yao ya sheria wanasema "LEGUM SERVI SUMUS UT LIBERI ESSE POSSIMUS= WE ARE SLAVES OF THE LAW IN ORDER THAT WE MAY BE ABLE TO BE FREE"

Ni lazima tuwe "watumwa" ww sheria ili tuweze kuwa "huru",yoyote anayetaka kuwa "huru" juu ya sheria anajitengenezea minyororo ya "utumwa".Ni kweli,kama hutaki kufuata "utumwa" kisheria wa Katiba ya nchi kwa kuwa na mpango kazi wa miaka mitano,basi unajiandalia nafasi ya kutokuwa huru huko mbeleni,ndio maana sababu ya "matamko" mpaka sasa Wizara ya Ujenzi imetumia Mara 4 ya Bajeti iliyopitishwa bila ridhaa ya Bunge,maagizo ya Rais ambaye ni Waziri wa zamani wa Ujenzi.Hii ni kwasababu "matamko" hayo hayana "utumwa" wa kisheria

Wakati tunakimbizana na haya maendeleo,ni heri sana tuendelee kuimarisha mfumo wa "Political Pluralism" ambapo zaidi ya ukosoaji wa serikali kufanywa na vyama vya siasa tu,turuhusu asasi za kiraia kutukumbusha mle ambapo serikali inajisahau,hizi ndizo kazi za "Civil Societies" na huu ndio wajibu wao,ndio maana wao ni "Watch-dogs",mbwa mlinzi huwa habweki kwa asiye mshuku,hubweka kwa anayemshuku ili tu kuhakikisha dhana ya "ulinzi shirikishi".Tuache kazi ya Asasi za Kiraia zichukuwe nafasi ya mbwa mlinzi ili kuikumbusha serikali pale inapojikwaa.Ulinzi shirikishi ni pamoja na kumkumbusha Rais pale wanapoona wao amekengeuka,ila kama tunakubaliana kuwa "Urais" ni "Umalaika",basi tukubaliane kusifia tu mwanzo mwisho

Rais ashirikiane na watakaomsaidia kumkumbusha,asijibanze na wanaomsifia kila anapokosea,wale watakaoshindwa kumwambia "mfalme chutama" siku nguo itakapotatuka mbele ya kadamnasi,wale wanaoshabikia hata kutatuka kwa nguo ya Rais mbele za watu na kushangilia badala ya kumkumbusha kuchutama,kama tunakubaliana kuwa Rais wetu ni "Malaika" basi tuungane pamoja kumpigia makofi hata nguo zinapotatuka.Haiwezekani tukaanza kutengeneza Taifa la kusifiana na kuimbiana mapambio.Tuogope hizi dalili za kuminya uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari.Wao wanasema "Information is Power",kama kila siku tunakumbushana kuombeana kwa Mungu,basi hivyo hivyo tushirikiane kupatiana habari za kusaidia maombi yetu yawe na tija.Wanasema "Verbum sat Sapient" = "A word is enough to a wise people".Tupende kusikilizana,huo ndio utaratibu wa waungwana.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Mbariki Rais wa Tanzania
 
Bandiko lipo vizuri.
Naunga mkono hoja zako lakini kuna mambo ambayo wengi wetu tunaweza tusifahamu hali halisi ipoje.

Kuna taasisi ambazo zina watu wenye maarifa na ni hazina kwa taifa, wanafanya kazi zao vizuri tu shida ipo moja. Taasisi hizi hutumiwa na wajanja wachache wakijua zinaaminika na kutambulika ndani na nje ya mipaka yetu.

Angalia ni kiasi gani tafiti au ripoti zenye tija kwa taifa zinapewa kipaumbele na taasisi husika na linganisha na ripoti ambazo zina tija kwa wanasiasa zinavyoripotiwa. Hii si bahati mbaya.

Magufuli amekuwa sehemu ya Serikali kwa muda mrefu na lobbying zinazofanyika anazielewa vizuri, hii inachangia yeye kupuuza baadhi ya wakosoaji.

Jambo la msingi ni kutopuuza kinachoongelewa maana hata pale penye nia mbaya kinaweza patikana cha kujifunza.
 
Bandiko zuri hakika. Watazania ni watu wa ajabu, tunakawaida ya kufikiri kuwa mara mtu akichaguliwa/teuliwa anabadilika kuwa superhuman jambo ambalo si kweli hata kidogo.
 
Bandiko lipo vizuri.
Naunga mkono hoja zako lakini kuna mambo ambayo wengi wetu tunaweza tusifahamu hali halisi ipoje.

Kuna taasisi ambazo zina watu wenye maarifa na ni hazina kwa taifa, wanafanya kazi zao vizuri tu shida ipo moja. Taasisi hizi hutumiwa na wajanja wachache wakijua zinaaminika na kutambulika ndani na nje ya mipaka yetu.

Angalia ni kiasi gani tafiti au ripoti zenye tija kwa taifa zinapewa kipaumbele na taasisi husika na linganisha na ripoti ambazo zina tija kwa wanasiasa zinavyoripotiwa. Hii si bahati mbaya.

Magufuli amekuwa sehemu ya Serikali kwa muda mrefu na lobbying zinazofanyika anazielewa vizuri, hii inachangia yeye kupuuza baadhi ya wakosoaji.

Jambo la msingi ni kutopuuza kinachoongelewa maana hata pale penye nia mbaya kinaweza patikana cha kujifunza.
Umesema sahihi mkuu KXY ,kwamba Mkulu amekuwa sehemu ya serikali kwa zaidi ya miaka 20(Umri wa mtu mzima)...hii inampa nafasi ya kujuwa nini nafasi ya Asasi za kiraia ktk uongozi.
Tumuhimize na kumkumbusha kuwa Demokrasia yenye tija ni pamoja na kuwasikiliza wale wanaokuzunguka kila wanachosema..si kila wanalosema wewe ni kukashifu na kutaka kuwaondoa wasifanye kazi zao
 
Kuna ukweli mkubwa hapa,Umechambua vizuri sana mkuu barafu
Umnifungua na kunipa hoja za msingi...Kweli kuna mahali Mh akumbushwe
 
Back
Top Bottom