Tukubali kwanza kuna gari model nyingi za Toyota ilichemsha kimauzo na zengine kwenye utengenezaji

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,722
Asilimia kubwa ya hapa kwetu wote tunatumia gari za Toyota.

ila kiukweli kuna gari zilizofanya vizuri na zengine zilifanya vibaya kama kichwa cha habari hapo juu.

Na kumbuka IST ilivotoka mwanzoni yani ilifanya vizuri sana kimauzo ila ilivotoka new model yake kama ikaishiwa kupendwa.

Kuna magari yalitengenezwa ila yakaongoza kwa ubovu kama passo,brevis na n.k

Toyota gari zinazompa jina ni haya land cruser na hilux zinazo nunuliwa sana na taasisi binafsi ,serikali na watu binafsi.

Gari gani unaona toyota ilizingua na isiyozingua
 
Magari ya TOYOTA na hata ya aina nyingine ni mazuri.

Tatizo ni sisi wanunuzi ambao tunanunua gari moja kwa ajili ya kufanya kazi zote za gari kumbe magari nayo nikama Viatu
  • Namaanisha; Viatu Vipo vya kutembelea ndani ya nyumba
  • Vipo vya kupandia Mlima, Vipo vya kukorogea Zege,
  • Vipo vya kwendea ofisini/Msikitini/kanisani; Ukiangalia hizo kazi zinaendana na uimara wa Kiatu
Sasa unanunua Passo huku unaishi milimani na rafu rodi, lazima ife muda mfupi
Lakini pia; Ukinunua Landcruiser ya kwendea kazini mjini Dar, Ni matumizi mabaya ya Pesa na gari lenyewe. Namaanisha ukinunua gari linaloendana na matumizi yako, Kila gari litakuwa zuri hata kama Passo.

Na yale Magari watu wanayofikiri ni mazuri ni kwa kuwa yapo katikati (yana faa sehemu nzuri na kiasi kwa sehemu mbaya (rafu rodi/Milima) na bei yake huwa ni ya juu zaidi ukilinganisha na hayo mengine
 
Gari ambazo hazijafanya vyema sokoni.
1.Vista
2.Verossa
3.Progress
4.Opa
5.Nadia
6.Voltz

Hizi gari hazikutengenezwa kwa wingi sababu hazikukubalika sana sokoni. Sio kwamba zilikuwa mbovu. LA HASHAA!

Utaona kabisa hazina muendelezo ama new model yake. Zote zilikuwa discontinued!!!
 
Back
Top Bottom