TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,743
Nimemsikiliza vizuri sana Mbunge Wa kigoma Mjini katika mkutano wa Chama chake cha ACT-WAZALEDO uliofanyika katika viwanja vya Zakhem Mbagala, mkutano uliopewa jina "Operesheni Linda Demokrasia Nchini".
Mkutano huu ulikuwa ni wa:
1. Kutaka kuvigonganisha vichwa vya watanzania ili waichukie Serikali na wamchukie rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. John Pombe Magufuli.
2. Zitto Kabwe kutaka kujionesha kama ilivyo kawaida yake kuwa yeye ndiye bora zaidi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania(angalia alivyomalizia hotuba yake kwenye mitandao ya kijamii, ilikuwa ni hotuba yake kama yeye, hakuna sehemu ambayo inaonesha ni msimamo wa ACT-WAZALENDO)
3. Zitto Kabwe kutaka kujikomba kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) hususan Chama chake cha Zamani cha CHADEMA na hasa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe(Kitendo cha kukimbilia Kupiga picha na Mbowe baada ya Mbowe kutangaza kuwa Upinzani utasusia vikao vya Bunge vitakavyoongozwa na Naibu Spika na kitendo cha kukimbilia kuviandikia barua za Mwaliko vyama vinavyounda UKAWA hasa akilenga kiwatega CHADEMA, matukio yote haya yanathibitisha nia hiyo ya Zitto). Hata hivyo, azma yake hiyo imegonga mwamba, Mapema sana CHADEMA walikanusha kupokea barua ya aina hiyo na kwa uhakika wamempuuza.
4. Kutaka kuviteka vyombo vya habari. Zitto alitegemea Leo Magazeti yote kwenye kurasa za mbele zingesheheni picha na maneno kedekede yahusuyo Zitto Kabwe na Mkutano wake. Leo Magazeti yote yametawaliwa na kazi nzuri iliyofanywa na Jeshi letu la Polisi lilivyopambana kikamilifu na watu waliojificha kwenye Mapango kule jijini Mwanza wakiwa na silaha nzito, mapambano yaliyopelekea Jeshi hilo kufanikiwa kuyaua matatu yao.
Hongereni sana Jeshi la Polisi. Wanahabari wamenifurahisha sana leo, Nawapongeza sana Chadema kazi kubwa wameifanya(ZITTO kama ulikuwa haujui, basi na ujue kwamba Mahasimu wako wamefanyakazi kubwa kuhakikisha haupati Coverage kwenye media na hasa Magazeti, Wewe ndiye unatakiwa kunyoosha mikono kwa Chadema, siyo Chadema kunyoosha mikono kwa Zitto Kabwe).
TAFAKURI: Tunahitaji Mjadala wa Kitaifa, wale tunaoona Rais Magufuli ni lulu isiyohitaji kuchezewa tusimame kidete kumuunga mkono rais wetu ili kupambana na Mazoea, rushwa, ufisadi, siasa za maji taka na uozo mwingi ambao ulikuwa ukilitafuna taifa.
Vivyo hivyo wale wanakubali kugonganishwa vichwa na Wanasiasa na kupepesuka kama jani linalopeperushwa na upepo na wabaki huko. Uongozi huu wa Dkt. John Magufuli siyo uongozi wa majukwaa ya siasa. Huu ndiyo uongozi ambayo mara kadhaa tuliulilia kukabiliana na Mazoea yaliojengeka miongoni mwa wahujumu uchumi wakubwa ambo ni WANASIASA.
TUWAKATAE.