Pombe haramu
Senior Member
- Dec 19, 2017
- 151
- 238
Najaribu kujiuliza haya matukio ya kutisha yanayokea nchini yameigwa kutoka nchi gani. Nikiangalia nchi mbalimbali zinazotuzunguka, naziona nchi tatu zina madikteta. Nazo ni DRC, Rwanda, na Uganda. Katika nchi ya Rwanda matukio ya watu kuuwawa, kutekwa, na kubambikia kesi yameshamiri. Na tangu mwaka 2015 nchi yetu imekuwa na ushirika madhubuti na Rwanda kupitia urafiki wa undugu kati ya Magufuli na Kagame. Marais hawa wawili wamekuwa mara kadhaa wakitembeleana. Na bila shaka wanashauriana masuala mbalimbali ya kiuchumi, usalama, na kisiasa. Katika nchi ya Rwanda mwanadada aliyetaka kugombea urais yupo mahabusu na mali za familia yake zipo katika mkakati wa kufilisiwa. Aina hii ya siasa za kuchunguza mali za raia wanaopinga serikali imeingia Tanzania. Askofu kakobe alimpinga rais Magufuli kwa kukiuka katiba na kumtaka atubu: aliishia kuchunguzwa na TRA na Uhamiaji. Kauli mbalimbali zimetolewa na viongozi mbalimbali kuhusu kumfilisi yeyote atakeipinga serikali. Mauaji ya kisiasa na utekaji ni jambo la kawaida huko Rwanda. Suala hili la mauaji na utekaji limekuwa la kushangaza na la kutisha kwa Tanzania, kwani halikuwahi kukithiri kama ilivyo katika awamu ya tano. Katika awamu hii polisi huwatawanya waandamanaji kwa risasi za moto, sio kwa maji ya kuwasha au mabomu ya machozi. Ni wazi sasa kuna haja ya kujitafakari kama kuna faida ya kuendelea kuwa na Urafiki na Rwanda chini ya Kagame..