Tukipendwa tupendeke.....

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,348
1,805
Uso mkunjufu ni alama ya furaha na amani moyoni,utaonekana mwenye furaha hata nje sababu kilichopo moyoni huonekana usoni,kuna wanawake wengi wenye elimu nzuri na kazi nzuri na Mungu amewapa uzuri wa tabia na imani ila bahati mbaya wameolewa na wanaume mzigo wasio na shukrani kwa wake zao.

Mwanaume mwenye bahati ya kupata mke mwema wengi wao huwa hawajui kuwa mke mwema ni chemichemi za mafanikio na hazina ya furaha,mwanamke anafanya kazi,anakusomeshea watoto,anakupikia chakula na anakufulia nguo na kukupa mapenzi ya dhati pamoja na kukupa mtaji ili ufanye shughuli za kukidhi mahitaji yako ila tatizo huja kwenye kushukuru kwa wanaume ,kushukuru yatakiwa kurejesha mapenzi ya dhati na kutoa maneno ya faraja kwa mke ili apate nuru na amani ya ndoa na kumsaidia baadhi ya majukumu.

Baadhi ya wanaume waliopo kwenye ndoa wasio na kazi wameshindwa rejesha mapenzi ya dhati kwa wake zao na shukrani za maneno na vitendo kwa wanawake bora na wajenzi wa familia zao,kuna wanawake wamechukua mikopo kwa ajili ya waume zao ili shukrani waliorejeshewa ni kuletewa watoto wa nje ya ndoa.

Mtu mwenye jicho la tatu ni kazi rahisi kumgundua mwanamke asiye na furaha na amani kwenye ndoa yake sababu daima sura za wanawake wasio na amani kwenye ndoa huonyesha simanzi na masikitiko ya mioyo yao,wengi wamepoteza uzuri na shape zao kwa kukosa kuheshimiwa na mapenzi ya dhati kwa waume zao ,ubaya unakuja kuhusu ule wimbo wa vumilia ndoa ndivyo zilivyo siku zote ,ndoa zimekuwa ngumu sana siku hizi.

Penye mapenzi matamu pana furaha na amani na kusameheana kwa haki na mafanikio ya pamoja kati ya mume na mke na penye mapenzi ya chuki pana ndoa ya kinafiki na kusameheana kinafiki na pana matatizo yasiyo kwisha na malumbano kila uchwao kati nya mume na mke .

Ndoa zote zina shida ila tumetofautiana hekima na busara za kutatatua matatizo ya ndoa pamoja na uvumilivu wa ndoa..It is not a lack of love, but a lack of friendship that makes unhappy marriages.
GedsellianTz
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom