Habari za siku wanajamii
Kama ilivyo kawaida ya jukwaa pendwa la teknolojia ambapo huwa tunaelekezana mambo mbalimbali yanayoendelea katika ulimwengu huu wa sayansi.
Katika pitapita zangu kwenye kakimeo kangu ka tecno hatimae kuna sehemu nimekuta kuna setting yenye kusomeka VPN
Na ukifungua hapo unakuta application zote za vpn ulizoinstall kwenye simu
Pia kuna alama ya +
Ukiifungua kuna nafasi za kujaza yaani custom setting za vpn mbali na zile za kudownload mtandaoni
Sasa wakuu wenye ujuzi juu ya hili hebu wachukue muda kiasi kutufafanulia nini cha kufanya ili kuweza kutumia VPN za namna hii
Wadau waje na majibu apa me natumia iphone x na mtandao wa airtel, kuna jamaa nimeona wanaserereka tu free vpn sema walikua na android so sijui kwa sisi wa ios ni vipi