Salaaam wana jukwaa,
Naenda moja kwa moja kwenye point, jamani tujifunze kutoa sadaka kidogo ulichonacho jitahidi umgawie mwenzio asiyenacho, huenda ndio maana wenzetu wahindi wamezidishiwa kwakuwa nawaona wanatoa sadaka sana, wakati mwingine unawaona weekend huku city centre wanagawa vyakula.
Ngozi nyeusi tumekuwa na tabia mbaya sana mtu akipata vijihela kidogo basi ni pombe na wanawake, pombe na wanawake havitakuvusha popote tubadilike.
Kifupi mimi nimekuwa mwepesi kusaidia jirani yangu na nimejiona kama vile nimekuwa sina stress na mungu amenifanyia wepesi kwenye maisha yangu kwakweli, najikuta vile vizingiti vijana wenzangu wanavyovilalamikia mimi naviruka kiwepesi kabisa.
Tukio la jana: Jana nimeenda zangu sokoni nikakumbuka ngoja nimchukulie na jirani yangu bidhaa mbili tatu, basi nikafungasha nikarudi home, nikashusha mizigo yangu then nikatoa na mzigo wa jirani nimefika hodi hodi jirani katoka kifua wazi, nikamsalimia then nikamwambia jirani nimetoka sokoni nimekukumbuka kidogo ndugu yangu japo kidogo, machozi yakaanza kumshuka ananiambia Mungu akuzidishie anasema yaani tangu asubuhi watoto wamelala sio kwa usingizi bali njaa imewalevya, muda huohuo nasikia anamwita mkewe aje kuchukua mzigo akapike, niliona huruma sana isee, yaani usijione una matatizo kuna watu wenye matatizo jamani.
TUJIFUNZE KUTOA JAPO KIDOGO