Tujifunze hili toka kwa Yahoo

Tujifunze hili toka kwa Yahoo

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
14,137
Reaction score
33,547
Miaka ya 90’s kwenye teknolojia ukisikia mtu akiwa na barua pepe uwezi kukosa yahoo.

Leo nitapenda kuzungumzia yahoo ila nitaanza mfano wa facebook ambayo imejifunza kutoka kwa yahoo!

Facebook ilishawahi kufanya kosa hili la yahoo kuzarau watu waliotoka kampuni kubwa kama ambayo yahoo mfano mzuri Brian Acton na Jan Koum kuzaraulika kipindi wanauza app yao kwa facebook mwanzoni.

IMG_7742.jpg

Bwana Brian Acton na Jan Koum baada ndio wavumbuzi wa WhatsApp. Wakati facebook wanaletewa mfumo huu wanunue hawa kuweza kukubaliana nao wakiona ni mawazo ya kijinga au kwakuwa waliona wamemaliza kila jambo.ila bei waliopewa ilikuwa pesa ambayo facebook wanaweza kununua mifumo hiyo hata kumi ila baadae kushtuka wamekuja kununua kwa bei kubwa sana.

Tuje kwenye yahoo

IMG_7743.jpg

Kampuni ya yahoo ilianza mwaka 1994 ambayo ikibeba tokea miaka 27 kuwa na bidhaa kama Yahoo! News; Yahoo! Mail; Yahoo! Finance; Yahoo! Sports; Yahoo! Search na n.k

Ila sababu ya yahoo kushindwa kufikia malengo ambayo kama angekuwa ametumia wazo la facebook japo naye alishtuka kwenye hatari ! Sasa tungekuwa tunazungumzia yahoo yenye uwezo mkubwa ambao google aliopo.

Angalia uzembe ambao yahoo alichukuria kwake

Historia:
Mwaka 1998:yahoo walikataa kununua google kwa kiasi cha usd milioni 1
Swali: hapa tunakuja tatizo lilikuwa kujiamini kama maelezo yanayo sema mwanzoni

Mwaka 2002: yahoo anatambua kosa alilolifanya na anajaribu kubembeleza kuinunua kwa kiasi cha usd milioni 3 huku kumesha kucha, japo google nayo ilitaka kuuza kiasi cha usd bilion 5. Yahoo alikataa hiko kiasi cha pesa huku akitaka kununua kwa dau nililo sema usd milioni 3.

Swali: je bado kama kulikuwa na kuitaji kununua bodi ya yahoo ikujitambua wakati miaka hiyo ndio mapinduzi ya teknolojia yalikuwa yanaanza kukua kwa kasi nyanja za mawasiliano na vifaa.

Mwaka 2008: Hapa yahoo ilikuwa inatembelea mkongojo lakini kuto kubali matokea huku kampuni ya microsoft akishika tamu aliomba kununua kampuni hiyo kwa kiasi usd bilioni 44.6. Yahoo alikataa kabisa?

Swali: bado bodi ijaona mabadiliko au tunasema unakufa na tai yako shingoni, ijakubari matokeo!

Mwaka 2016: Hapa ndipo mambo yalipo kuwa mabaya baada ukisikia kuangukia pua yahoo aliamua kuuzia kampuni kwa verizon kiasi cha usd bilioni 4.6.

Hitimisho:historia inaonyesha mwenendo mbaya ambao bodi yenyewe na wakuu wa kampuni kushindwa kuendana na wakati hili kukabili hali ya biashara na teknolojia za wakati.

Katika biashara ambazo kampuni nyingi zinashindwa kutumia au japo zina puuziwa ni!

Identifying and Managing Business Risks

Hili jambo ndilo limemfanya bwana elon musk naona kaliweza sana

IMG_7747.jpg


Baishara zake na bodi yake ndio imeweza kutumia mfumo huu kuendana na wakati

IMG_7745.jpg


Vitu vitano ndivo vinaweza kukusaidia kupambana na mbinu hizi:
Japo nitaeleza kirahisi sana.

1) Indentify
Hatua ya kwanza ni kutambua hatari ambazo biashara inakabiliwa na mazingira yake ya kiutendaji. Kuna aina nyingi za hatari - hatari za kisheria, hatari za mazingira, hatari za soko, hatari za kisheria, na mengi zaidi. Ni muhimu kutambua sababu nyingi za hatari iwezekanavyo. Katika mazingira ya mwongozo, hatari hizi zinajulikana kwa mikono.

2) Analyze
Mara hatari inapogundulika inahitaji kuchambuliwa. Upeo wa hatari lazima uamuliwe. Ni muhimu pia kuelewa uhusiano kati ya hatari na sababu tofauti ndani ya biashara. Kuamua kwa ukali na uzito wa hatari ni muhimu kuona ni ngapi kazi za biashara zinaathiri hatari. Kuna hatari ambazo zinaweza kusababisha biashara nzima kusimama ikiwa imesimamishwa, wakati kuna hatari ambazo zitasumbua tu uchambuzi. Katika mazingira ya mwongozo wa usimamizi wa hatari, uchambuzi huu lazima ufanyike kwa kutathimini kwa kujionea.

3) Evaluate or Rank
Hatari zinahitaji kuwekwa katika nafasi na kupewa kipaumbele. Suluhisho nyingi za usimamizi wa hatari zina aina tofauti za hatari, kulingana na ukali wa hatari. Hatari ambayo inaweza kusababisha usumbufu fulani huwa zimekadiriwa kiwango cha chini, hatari ambazo zinaweza kusababisha upotezaji wa janga zimekadiriwa kuwa hali ya juu zaidi.

4) Treat
Kila hatari inahitaji kuondolewa au kuwezeshwa kutatuliwa iwezekanavyo. kwa kuungana na wataalam wanao juha sababu ambazo hatari hiyo . Katika mazingira ya mwongozo, hii inajumuisha kuwasiliana na kila mdau na kisha kuanzisha mikutano ili kila mtu azungumze na kujadili maswala hayo mfano maono,mawazo na kukalibisha changamoto ambazo zinajitokeza.

5) Monitor and Review
Sio hatari zote zinaweza kuondolewa - hatari zingine zipo kila wakati. Hatari za soko na hatari za mazingira ni mifano miwili tu ya hatari ambazo kila wakati zinahitaji kufuatiliwa. Chini ya ufuatiliaji wa mifumo ya mwongozo hufanyika kupitia wafanyikazi wenye bidii. Wataalam hawa lazima wahakikishe kuwa wanaangalia kwa karibu mambo yote ya hatari.

Asanteni:
Kama kutakuwa kuna makosa mnaweza jadili:

IMG_7744.jpg
 
So Sasa hv Yahoo imeshakufa au inaendeleaje na mpinzani wake Ni Nani kwa sasa
 
Mapinduzi ya teknolojia yameua biashara/makampuni mengi sana ambayo hayakushtuka mapema.
 
Back
Top Bottom