Uchaguzi 2020 Tujadili kwa manufaa ya Taifa: Uchaguzi 2020 twende na Nani na kwanini?



Kwa wanasiasa wa hapa Tanzania for the next 30 years anayefaa kuongoza nchi yetu ni Magufuli tu, hao wengine ni waganga njaa. Angalia maendeleo anayoleta Magufuli toka aingie madarakani na ujinga walioufanya marais vinyago waliopita katika utawala wao wa miaka 30. With Magufuli, tutafika mbali sana ila hao vinyago uliowataja hapo juu watarudisha kule kule kwa marais wasanii waliopita.
 
Kuna watu mnaishi kwa hisia (imani) basi mnataka watu wote waishi kwa hisia (imani). 'maisha mazuri yatakuja' lini na wapi
 
- SGR ni kichaa tu atakayeamini kuwa ni mradi wenye manufaa. hivi unajua TAZARA ni SGR pia lakini 90% ya mizigo & abiria ambako reli inapita vinatumia barabara?
Hujuia hata unachokiongea, tangu lini cape gauge (3 ft 6 in - TAZARA) ikaitwa standard gage (4 ft 8 1⁄2 in)?

Unafahamu kuwa neno "standard" linatokana na Marekani kuviita vipimo vya Imperial (inch and foot), standard?

Kwa hiyo 4 ft 8 1⁄2 in gage, ambayo ndiyo inyotumika nchi hiyo ikapata jina standard gage wakati ile ya (3 ft 6 in) iliyoanzia Cape town ikapata jina cape gage ambayo ndiyo iliyochaguliwa kutumika TAZARA kwa kuwa Zambia teyari walikuwa wanayo ikiunganishwa na Zimbabwe mpaka Afrika ya kusini.
 
Sasa TAZARA serikali imeshindwa kuiendesha. Hata ile ya kati ya TRC inasuasua. Muujiza gani mtafanya muweze kuiendesha hiyo ya umeme kama mradi mdogo tu wa BRT umewashinda?
 
Sasa TAZARA serikali imeshindwa kuiendesha. Hata ile ya kati ya TRC inasuasua. Muujiza gani mtafanya muweze kuiendesha hiyo ya umeme kama mradi mdogo tu wa BRT umewashinda?
TAZARA ni tofauti kidogo kwa kuwa inajumuisha nchi mbili ila TRC serikali inahusina 100% na kwakweli wanajitahidi sana. Kuna ukarabati mkubwa unafanyika kuiongezea reli ubora hiyo (wanabadilisha reli na mataluma), hata ile ya Tanga ambayo ilikuwa imekufa kwa zaid ya miaka 10 inafufuliwa.
 
irani* ilani

kwa kuwa mimi si mpiga ramli , basi , yeyote yule ambaye CCM itatuletea, mimi nitakuwa naye. lakin ingekuwa maamuzi yangu pekee yanafaa kumuweka Rais, basi ni SGR, bomba la mafuta ningechagua
Hata ukiletewa CHAWA wee sawa tuu
 
Kama tunataka kuiokoa tz
Kama tunataka mtanzania awe na hadhi nchini kwake
Kama tupo tayari kuwa na uongozi unaondeshwa kwa mujibu wa sheria
Kama tunahitaji kutendewa haki kutoka mihimili yote ya nchi
Kama tumeamua kuitaarisha nchi kwa kizazi kijacho na uchumi unaoweza kusomeka
Kama tumechoka kutawaliwa na makundi ya watu wanaohisi kutoa huduma za kijamii ni hisani
Kama tumechoka kudharauliwa na kutawaliwa kwa matamko
Kama tunataka jeshi letu la polisi liwe jeshi la kulinda na kutoa huduma kwa wananchi
Kama tunahitaji uongozi badala ya utawala
Haya yote yatawezekana katika uongozi wa kisheria tu na MTU pekee anaefaa ni LISSU
Kwa wale wenye uwezo wa kufikiri wataona ukweli huu
 
Bado hujajibu swali langu. TRC haijiendeshi kwa faida. Kuna wakati treni zake zinaishiwa mafuta njiani! Ile ya kaskazini ilikufa kabisa..well sasa unasema mnafufua. Swali liko pale pale nininkitasuia hiyo sgr isiwe au ishindwe kujiendesha kama hizo nyingine? Miradi midogo tu kama BRT tumeona inatutoa jasho, au nayo itahamishiwa vote 20 ili isikaguliwe wala kuhojiwa?
 
Matatizo ya TRC, BRT yametokana na sera mbovu za azimio la Zanzibar, wafanyakazi wa serikali kufanya biashara kwa kutumia nafasi zao kujitajirisha. TRC ilikufa kwa kuwa kuna watu walifanya jitihada kudhorotesha shirika ili biashara zao za malori zifaidike.

Uongozi wa sasa inachofanya ni kuondoa yale makosa yaliyofanyika miaka 30 iliyopita, hivyo tutegemee ufanisi kwenye reli zote zinazo milikiwa na serikali.
 
whatever.

the bottom line is kujenga reli ambayo uzoefu unaonyesha haina tija is akin to mental retardation.
 

Kwa taarifa yako deni la taifa ndani ya hii miaka minne lemepanda 1/3 dhidi ya marais wote wanne waliopita.
 
Kwa taarifa yako deni la taifa ndani ya hii miaka minne lemepanda 1/3 dhidi ya marais wote wanne waliopita.


Still, nakushauri wewe na familia yako pamoja na watanzania wote kumpigia kura Magufuli. Kama uliweza vumilia ujinga uliofanywa na marais waliopita kwa miaka 30 basi utaweza funga mkanda kwa utawala huu bora chini ya Magufuli, sawa?
 

Kuna reli inamilikiwa na mtu binafsi? Hii mikopo kwa ajili ya hiyo miradi ina mkakati mzuri wa kulipa au tunakopa tu kusaka polical millage? Kama SGR ya Kenya inaendeshwa kwa hasara, hii yetu tuna uhakika gani itakuwa na manufaa?
 
Huu ni ubaguzi,mbona umemwacha Mh.Job Yustino Ndugai,muongeze kwenye list ya ccm
 
Still, nakushauri wewe na familia yako pamoja na watanzania wote kumpigia kura Magufuli. Kama uliweza vumilia ujinga uliofanywa na marais waliopita kwa miaka 30 basi utaweza funga mkanda kwa utawala huu bora chini ya Magufuli, sawa?

Hastahili kuwa rais kwani amejikita tu kwenye miundo mbinu, ila kwenye uchumi kaharibu, ajira zimemshimshinda, kwenye demokrasia ndio sifuri kabisa, amegeuza nchi ya uonevu huku akiminya uhuru wa kujieleza. Akae pembeni aingie rais anayeweza kufanya vyote kwa uwiano sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…