Elections 2020 Tujadili kwa manufaa ya Taifa: Uchaguzi 2020 twende na Nani na kwanini?

1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
4,497
2,000
Nijuavyo rais wa sasa lazima atapita ili amalize kipindi cha miaka kumi kama wenzie, hili swali lilipaswa kuulizwa uchaguzi wa mwaka 2025 ndio watu wajipange kumuweka mpendwa wao.
Analipwa kwa kodi za watanzania kama wafanyakazi wengine.
Mfanyakazi akiharibu anastaafishwa kwa manufaa ya umma.
Kumvumilia mfanyakazi anayevuruga kwa kumuonea huruma mpaka astaafu ni kuzidi kuvuruga kazi.
Miaka mitano akimaliza pia anastaafu na anapata marupurupu yake na atakua na bafasi ya kujaribu tena 2025/2030 n.k.

Tusiibinafsishe nchi kwa MTU mmoja na familia yake.
Hayo mambo ya kuwaaminisha wanasiasa kuwa watakaa muda mrefu madarakani ndio maana Viaongozi wa Afrika wanakua mafisadi wanaojilimbikizia Mali na marafiki zao mana wanajua hawatoki mpaka wastaafu au watumie ubabe kuzeekea madarakani.

Nchi zote za kiimla zina Watawala Mabilionea na matrilionea kupitia Mali na pesa za umma. Hawajali mana wakishakalia kiti wanajua hawaguswi mpaka wastaafu au wazeekee madarakani.
Tunawakabidhi kila kitu.
Ardhi yote ni Mali yao.
Fedha zote ni Mali yao.
Vyeo vyote ni Mali yao.
Sifa zote ni za kwao.
Heshima yote ni ya kwo.
Sheria zote zipo chini yao.
Roho na nafsi za watu wote ni zao.
Waafrika wengi wamelogwa.
 
MWALLA

MWALLA

JF-Expert Member
14,982
2,000
Nimeona thread nyingi zikimponda huyu na kumsifia yule kuhusu uchaguzi wa uraisi 2020..

nikapata wazo , kwanini tusijadili bila ushabiki wa vyama vyetu , kwa maslahi ya taifa letu kwanza kwani tukikosea kuchagua tunaumia wote ,

Ni Nani anayefaa kutuongoza Tena kwa miaka mongine mitano mbele uchaguzi wa 2020 na kwanini ? Nitatoa majina yanayojitokeza kugombea uraisi kwa vyama kadhaa Ila na wewe urataja wa kwako kama humu hawamo

CCM
1. John magufuli
2. Bernad membe

CHADEMA

1. Tundu Lissu

ACT
1. Zitto
2. Maalim Seif

CUF
1. Lipumba

Mitazamo wangu:

Mimi nàona JPM bado tunamhitaji Sana kwa miaka mingine mingi ijayo, kwakuwa pamoja na kwamba irani ya chama inasisitiza viwanda lakin kajitahidi kuboresha barabara, umeme , Huduma za kijamii, kuwajali wafanyabiashara , ufisadi umeisha, amefufua ndege , anatengeneza reli ya kisasa, maisha mazuri yanakuja tuwe wavumilivu , nk

Je , wewe una mtazamo gani ??
 
Vladimir Lenin

Vladimir Lenin

JF-Expert Member
2,733
2,000
Still, nakushauri wewe na familia yako pamoja na watanzania wote kumpigia kura Magufuli. Kama uliweza vumilia ujinga uliofanywa na marais waliopita kwa miaka 30 basi utaweza funga mkanda kwa utawala huu bora chini ya Magufuli, sawa?
Unawashwa kinyeo bila shaka, nakuja na dudukila mkuu.
 
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
4,497
2,000
Kuna reli inamilikiwa na mtu binafsi? Hii mikopo kwa ajili ya hiyo miradi ina mkakati mzuri wa kulipa au tunakopa tu kusaka polical millage? Kama SGR ya Kenya inaendeshwa kwa hasara, hii yetu tuna uhakika gani itakuwa na manufaa?
Afrika tuna ubinafsi sana hasa wanasiasa.
Hakuna tafiti zinazofanyika kabla ya kuchukua hatua na maamuzi ya kitaifa.

Uchumi kwa wananchi ni dhoofu ili hali. Na makusanyo ya kodi yanaongezeka kutokana na ukweli kuwa fedha zote zimepelekwa hazina.
Hela za Halmashauri na makusanyo mengine kipindi cha JK zingepelekwa zote hazina nadhani angekusanya zaidi ya Tri.2 kwa mwezi.

Pesa nyingi sana enzi za JK zilikua zinaachwa kwenye ngazi zingine ili zisaidie kutatua matatizo yanayojitokeza kwa ghafla.
Watu wachache Kule Halmashauri na kwinginepo walikosa tu uadilifu lakini JK alikua ni habari nyingine kwenye uchumi na Diplomasia.

Makampuni Mengi yana Magari yao Binafsi ndio maana sula la treni lilihitaji pia wawekezaji washirikishwe ili tusirumie kodi yetu yote na mikopo ambayo haitaweza kulipwa kwa faida ya miradi hiyo Hata miaka mia ijayo.

Mabasi yanakuja ya kisasa na mazuri sana watu bado watapenda usafiri wa mabasi hasa kama treni itaendeshwa kama Mradi wa Mwendokasi unavyokuwa na huduma Mbovu.

Hawajui kuwa Basi moja likitika Mwanza mpaka DSM linalipa ushuru kila Halmashauri ya kiwango kisichopungua Sh.3000/- .Ukifanya utafiti utagundua kuwa Basi Moja kwa Mwaka linachangia mamilioni ya fedha kwa serikali kuliko wanavyodhani kuwa matajiri wanapata tu kwenye mabasi hayo na Mara nyingine wanajaribu kuwakwamisha tu.
Wanalipa kila Halmashauri.
Wanalipa Sumatra.
Wanalipa Kodi ya mapato.
Wananunua mafuta ambayo yanakatwa kodi ,Eura, tarura, rea, motor vehicle License,n.k.
Yote hayo ni mapato yanayotokana na Basi moja.

Kwa wenzetu wameendelea sana hayo matreni yanakua kama huduma tu kwa jamii sio kwa ajili ya biashara.
Kwetu bado tunahitaji fedha za kujenga uchumi mana ni nchi tegemezi.
Kuanzisha mradi ambayo hauna faida ni mzigo mkubwa usio na maana yoyote zaidi ya kiki za kisiasa na hasara kwa taifa.

Kuna mahali tunakosea na hatutaki kurekebisha zaidi ya kujifariji kwa imani kuwa mambo mazuri yanakuja.
 
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
4,497
2,000
Kwa wanasiasa wa hapa Tanzania for the next 30 years anayefaa kuongoza nchi yetu ni Magufuli tu, hao wengine ni waganga njaa. Angalia maendeleo anayoleta Magufuli toka aingie madarakani na ujinga walioufanya marais vinyago waliopita katika utawala wao wa miaka 30. With Magufuli, tutafika mbali sana ila hao vinyago uliowataja hapo juu watarudisha kule kule kwa marais wasanii waliopita.
Acha dharau kabisa.

Nchi sio reli wala ndege.
Nchi ni stability ya kiusalama.
Kuna watu wametumia akili nyingi sana na maarifa makubwa kuijenga nchi hii ikawa na Jeshi imara sana Afrika na Dunia kwa ujumla unatambua hilo.

Hivi huyo unayemtukuza na kuwaita waliomfikisha hapo angekuta wanajeshi hawana uniform,vifaru vya kusasa,manowari,ndege vita za kisasa, makombora, helkopta, nyumba za kisasa za kuishi,mishahara na pisho nzuri, wanapata mikopo kwenye mabenki kwenye mazingira mazuri na masharti mazuri. Majenerali wamewekewa utaratibu mzuri wa kimaslahi n.k ,angeweza kukimbilia kununua ndege ya abiria?

Acha dharau na kutoa maneno ya kashfa kwa watu walioliletea taifa hili heshma kubwa sana kwa sababu ya kusaka vyeo mana ndiyo kilichobaki sasa.
Kwa sasa ili ule ni lazima usifie Hata makosa.
Wengine walikubali kukosolewa ndio maana unaona makosa yao.
Mwinyi alikaa kimya akakosolewa na Mstaafu Hayati Mwl. Nyerere na hakuwahi kumtisha wala kumwambia afunge mdomo japo angeweza kufanya hivyo. Aliimarisha demokrasia na Uhuru wa maoni mana ndio hekima ilivyo.

Mfalme aliyetajwa sana kwenye vitabu Vya dini kuwa Mwenye Hekima ,busara na maarifa kuliko wote waliowahi kuishi duniani aliitwa Suleiman . Wakati wa utawala wake dunia nzima ilikua na amani na utajiri na maisha bora na hukumu za haki kwa kila mtu.

Mfalme Suleimani Hakuwa anatumia maguvu Bali hekima. Akaunganisha Taifa lake na mataifa mengine yote yalikua yanajifunza kwake.

Tusiwadharau watu walioongoza nchi hii kwa weledi mkubwa na busara nyingi kwa uvumilivu mkubwa.
Amani unayoiona ilijengwa tangu Mkoloni mpaka sasa inaanza kujikita kwenye kudharauliana kimakabila na kivyama na kimadaraka. Hata wakuu wa mikoa sasa tunaona wanadharauliana kwa wengine kujiona bora zaidi huku wakitembelea magari magari ya kifahari kuliko Hata mawaziri kwa sababu tu ya kujiona bora kuliko wengine.

Nchi nzuri ni ile yenye usawa mbele ya sheria bila kijali MTU.
Hapo ndipo viongozi wengi wa Afrika wanaposhindwa Hata unayemsifia anashindwa hapo kwenye kusimamia haki kwa usawa bila kujali itikadi na urafiki .
 
Chamoto

Chamoto

JF-Expert Member
5,493
2,000
Kuna reli inamilikiwa na mtu binafsi? Hii mikopo kwa ajili ya hiyo miradi ina mkakati mzuri wa kulipa au tunakopa tu kusaka polical millage? Kama SGR ya Kenya inaendeshwa kwa hasara, hii yetu tuna uhakika gani itakuwa na manufaa?
Kazi moja ya serikali ni kutengenza mazingira mazuri ya kukuza uchumi. Miradi kama barabara, reli n.k inachochea maendeleo ambayo huwezi kuyaona moja kwa moja.

Mhandisi akiumia akiwa site na akaweza kukimbizwa hospitali ya karibu (serikali iliyojenga) haraka kwa kuwa pia barabara ni nzuri (serikali iliyojenga), maisha ya jamaa huyo yatakuwa yameokolewa na hivyo kuokoa pesa na muda (miaka) ambayo serikali ilitumia kumsomesha mtaalam huyo.

Awamu hii inachokifanya ni kuwekeza katika miundombinu itakayochochea uchumi wetu huko mbeleni.
 
tindo

tindo

JF-Expert Member
28,547
2,000
Kazi moja ya serikali ni kutengenza mazingira mazuri ya kukuza uchumi. Miradi kama barabara, reli n.k inachochea maendeleo ambayo huwezi kuyaona moja kwa moja.

Mhandisi akiumia akiwa site na akaweza kukimbizwa hospitali ya karibu (serikali iliyojenga) haraka kwa kuwa pia barabara ni nzuri (serikali iliyojenga), maisha ya jamaa huyo yatakuwa yameokolewa na hivyo kuokoa pesa na muda (miaka) ambayo serikali ilitumia kumsomesha mtaalam huyo.
Ni hivi, Magufuli arudi kuwa waziri wa miundombinu, kwenye urais hana uwezo.
 
Ndachuwa

Ndachuwa

JF-Expert Member
5,883
2,000
Tundu Lissu anawazidi hao wote. . IQ 148
IQ 148; hilo ndilo kosa kubwa; kiongozi anatakiwa ambaye atasikiliza ushauri wa wataalamu/wasaidizi wake; chambua hizo shauri na kufanya maamuzi yeye kama kiongozi mkuu. Kumchagua mtu eti ana akili kuliko sisi wote maana yake mawazo yake yatamtosha ahitaji baraza la mawaziri wala wataalamu wa kumshauri.
 
Chamoto

Chamoto

JF-Expert Member
5,493
2,000
Ni hivi, Magufuli arudi kuwa waziri wa miundombinu, kwenye urais hana uwezo.
Ni wewe tuu usieona lakini sisi tuliojaaliwa "macho" tunaona viashiria vizuri vya uongozi wake si Tanzania tuu mpaka IMF, the economist, share za ACACIA n.k
 
tindo

tindo

JF-Expert Member
28,547
2,000
Ni wewe tuu usieona lakini sisi tuliojaaliwa "macho" tunaona viashiria vizuri vya uongozi wake si Tanzania tuu mpaka IMF, the economist, share za ACACIA n.k
Hivyo viashiria viko toka enzi za Nyerere. Kwahiyo kama ni hadithi ya viashiria vitabakia hivyo hivyo na ataingia rais mwingine hadithi itakuwa ni hiyo hiyo.
 
mbongo_halisi

mbongo_halisi

JF-Expert Member
4,663
2,000
Hastahili kuwa rais kwani amejikita tu kwenye miundo mbinu, ila kwenye uchumi kaharibu, ajira zimemshimshinda, kwenye demokrasia ndio sifuri kabisa, amegeuza nchi ya uonevu huku akiminya uhuru wa kujieleza. Akae pembeni aingie rais anayeweza kufanya vyote kwa uwiano sahihi.

Kunywa maziwa kwanza, huyu ndiye rais bora inabidi achwe anyooshe nchi ili wazururaji wakimbie jiji warudi vijijini kulima.
 
mbongo_halisi

mbongo_halisi

JF-Expert Member
4,663
2,000
Acha dharau kabisa.

Nchi sio reli wala ndege.
Nchi ni stability ya kiusalama.
Kuna watu wametumia akili nyingi sana na maarifa makubwa kuijenga nchi hii ikawa na Jeshi imara sana Afrika na Dunia kwa ujumla unatambua hilo.

Hivi huyo unayemtukuza na kuwaita waliomfikisha hapo angekuta wanajeshi hawana uniform,vifaru vya kusasa,manowari,ndege vita za kisasa, makombora, helkopta, nyumba za kisasa za kuishi,mishahara na pisho nzuri, wanapata mikopo kwenye mabenki kwenye mazingira mazuri na masharti mazuri. Majenerali wamewekewa utaratibu mzuri wa kimaslahi n.k ,angeweza kukimbilia kununua ndege ya abiria?

Acha dharau na kutoa maneno ya kashfa kwa watu walioliletea taifa hili heshma kubwa sana kwa sababu ya kusaka vyeo mana ndiyo kilichobaki sasa.
Kwa sasa ili ule ni lazima usifie Hata makosa.
Wengine walikubali kukosolewa ndio maana unaona makosa yao.
Mwinyi alikaa kimya akakosolewa na Mstaafu Hayati Mwl. Nyerere na hakuwahi kumtisha wala kumwambia afunge mdomo japo angeweza kufanya hivyo. Aliimarisha demokrasia na Uhuru wa maoni mana ndio hekima ilivyo.

Mfalme aliyetajwa sana kwenye vitabu Vya dini kuwa Mwenye Hekima ,busara na maarifa kuliko wote waliowahi kuishi duniani aliitwa Suleiman . Wakati wa utawala wake dunia nzima ilikua na amani na utajiri na maisha bora na hukumu za haki kwa kila mtu.

Mfalme Suleimani Hakuwa anatumia maguvu Bali hekima. Akaunganisha Taifa lake na mataifa mengine yote yalikua yanajifunza kwake.

Tusiwadharau watu walioongoza nchi hii kwa weledi mkubwa na busara nyingi kwa uvumilivu mkubwa.
Amani unayoiona ilijengwa tangu Mkoloni mpaka sasa inaanza kujikita kwenye kudharauliana kimakabila na kivyama na kimadaraka. Hata wakuu wa mikoa sasa tunaona wanadharauliana kwa wengine kujiona bora zaidi huku wakitembelea magari magari ya kifahari kuliko Hata mawaziri kwa sababu tu ya kujiona bora kuliko wengine.

Nchi nzuri ni ile yenye usawa mbele ya sheria bila kijali MTU.
Hapo ndipo viongozi wengi wa Afrika wanaposhindwa Hata unayemsifia anashindwa hapo kwenye kusimamia haki kwa usawa bila kujali itikadi na urafiki .

We mbona mpuuzi kihivyo, nimemkashifu nani ama nimesema maneno gani yasiyo ya ukweli?
 
N

ngalanga

JF-Expert Member
871
1,000
Umeanza vizuri tu ,kumbe umeingia kwenye mjadala huu ukiwa na jina mfukoni kabisa kutushawishi,ilitakiwa uwe msikilizaji kwanza kupima upepo,sasa wewe ghafula umeanza kupiga mapambio lol
Nimeona thread nyingi zikimponda huyu na kumsifia yule kuhusu uchaguzi wa uraisi 2020..

nikapata wazo , kwanini tusijadili bila ushabiki wa vyama vyetu , kwa maslahi ya taifa letu kwanza kwani tukikosea kuchagua tunaumia wote ,

Ni Nani anayefaa kutuongoza Tena kwa miaka mongine mitano mbele uchaguzi wa 2020 na kwanini ? Nitatoa majina yanayojitokeza kugombea uraisi kwa vyama kadhaa Ila na wewe urataja wa kwako kama humu hawamo

CCM
1. John magufuli
2. Bernad membe

CHADEMA

1. Tundu Lissu

ACT
1. Zitto
2. Maalim Seif

CUF
1. Lipumba

Mitazamo wangu:

Mimi nàona JPM bado tunamhitaji Sana kwa miaka mingine mingi ijayo, kwakuwa pamoja na kwamba irani ya chama inasisitiza viwanda lakin kajitahidi kuboresha barabara, umeme , Huduma za kijamii, kuwajali wafanyabiashara , ufisadi umeisha, amefufua ndege , anatengeneza reli ya kisasa, maisha mazuri yanakuja tuwe wavumilivu , nk

Je , wewe una mtazamo gani ??
 
Chamoto

Chamoto

JF-Expert Member
5,493
2,000
Hivyo viashiria viko toka enzi za Nyerere. Kwahiyo kama ni hadithi ya viashiria vitabakia hivyo hivyo na ataingia rais mwingine hadithi itakuwa ni hiyo hiyo.
Tulisifiwa sana kipindi cha Mkapa na kikwete kwa kuuza mali za watanzania leo hii tunaandikwa vibaya kila kukicha, kisa tumepata mtu anayesema hapana. Wenye akili hapa wataweza kuchambua mchele na chuya.
 
mbongo_halisi

mbongo_halisi

JF-Expert Member
4,663
2,000
Pole kwa kushindwa kujua tofauti ya ubora na ukatili.

Katili ni yule auae watu kama Iddi Amini au Sadam Hussein, bora ni mtu kama Magufuli anyoshaye nchi. Upo hapo kijana alosto?
 
Forum statistics

Threads
1,424,986

Messages
35,078,036

Members
538,184
Top Bottom