Tujadili kuhusu maisha baada ya Chuo

Hizo programming language unawezaje kutengeneza hela mtaani?


Am curious to know.
 
Kiukweli hili jambo ni gumu sana, pia ni rahisi kulielezea kwa mdomo, kiufupi ni muda vijana tujifunze kuendena na mazingira na kukubari ukweli kuwa ajira ni mtiti kwani hii itapunguza expectations ambazo mara nyingi ndio zinatesa.

Tuache kujifariji uongo sijui kilamtu na bahati yake, sawa kuna bahati lakini ukweli nao huwa unasimama vile vile ajira ni tatizo ni tatizo basi.

Ni muda wa vijana kujifunza mbinu mpya na skills ambazo hazifundishwi mashuleni ila zinamake pesa mtaani, Mfano hivi sasa mtandaoni kuna fursa kibao sana, kama

1. Designing & graphics, sasa kama una pc afu unachekia movies tu basi endelea, vizuri.

2. Copywriting, ujuzi wa kuuza kupitia maandishi, ingia youtube search hilo neno utaelewa nini kinafanyika, kama ukiwa na ujuzi huu basi utauza kitu chochote mtandaoni kwa urahisi hivyo hata kama huna mtaji wa fedha unaweza kuuza bidhaa ya mtu mwingine na ukapata kamisheni

2. Affiliate Marketing, uuzaji wa ushirika ( udalali mtandaoni) huna haja ya kuwa na bidhaa hapa wewe ni kuuza bidhaa za watu wengine kisha unapata kiasi chako. Pia Google utaelewa vizuri inavyofanya kazi,

3. Elimu ya matangazo ya Sponsored[Facebook & Instagram] hii naweza sema kila siku inashika kasi wafanyabiashara wengi sikuhizi wanataka watu wakuwawekea matangazo. [ nimesoma Journalism lakini hii ndio kazi yangu kwa sasa sikosi hela ya kula]

4. Video editing, hii sina haja ya kuelezea sana

Kiufupi skills zipo nyingi ila hizo ni chache kwa haraka haraka nimezitaja, mwingine pia anaweza kuongezea.


Uzuri ni kwamba hivyo vyote unaweza kujifunza bure mtandaoni na kama ni garama ni ndogo sana.

Shida vijana wengi bongo tunaingia Youtube kuangalia udaku. Wakati youtube ni darasa zuri sana. Ila maisha pia ni kuchagua[emoji6]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…