Tuifanye miji yetu iwe misafi

mdau wetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Posts
548
Reaction score
62
Mji wa Moshi ulioko katika mkoa wa Kilimanjaro Kaskazini mwa Afrika unasifika kwa usafi. Waliotembelea mji huo wanatuhadithia kwamba, mji huo ni msafi licha ya udogo wake na bustani zake zina mandhari ya kuvutia. Sifa nyingine ni kwamba, wahusika wameweza kudumisha sheria za usafi katika mji huo na hivyo kumfanya kila mwananchi kufahamu jukumu lake. Kwa nini miji kama Dar na mingineyo isiige mfano huu. Utakuta mtu yuko ndani ya daladala akimaliza kunywa maji yake ya uhai anarusha chupa ile barabarani, akimaliza kuandika tarakimu na vocha yake ya simu anaitupa popote alipo, matokeo yake Dar leo imejaa vyupa vya maji, manailoni na makaratasi ya vocha hapo bila kujali taka zingine zilizozagaa kwa wingi. Maeneo ya katikati mwa Jiji kidogo kuna juhudi za usafi zinafanyika lakini maeneo mengine ya jiji hili yanasikitisha. Moja ya haiba ya mtu ni usafi hebu kila mtu na aazimie kuanzia leo kwamba, hatatupa taka ovyo na tuone jiji letu litakuwa katika hali gani.Kutokana na mazoe mabaya hata sehemu ambazo kuna madebe ya taka mtu utamuona anatupa taka chini.
 
Usisahau kunakipindi Jiji la dsm lilipata tuzo ya Jiji safi kuliko yote Africa mashariki na kati.Najiuliza labda hao wakaguzi walitembezo baadhi ya maeneo machache city centre! Usafi wa mji hujengwa na mazoea na desturi za jamii iliyolizunguka.Kazi ya serikali za miji ni kutengeneza policy na Sheria zitakazosimamiwa kuhusu usafi wa mji.Usafi pia huanzia kwa mtu mwenyewe binafsi kabala ya mazingira yanayomzunguka
 

Kama Moshi wameweza ambayo ni sehemu ya Tanganyika, ina maana sehemu nyingine pia inawezekana. Miji na Majiji wawekeze sana katika kutoa elimu kwa wananchi wasitupe taka hovyo. Vilevile sheria ziwe kali kwa yeyote atakayepatikana anatupa taka hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…