Tufahamu kuhusu ectopia cordis

Tufahamu kuhusu ectopia cordis

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,387
Reaction score
4,881
Kwa wale wataalamu wa Afya haya maneno Mawili yani Ectopia na Cordis sio mageni kwao.
Ectopia-likimaanisha Kuwa Mahali Pasipotakiwa/Abnormal Position na Cordis Likimaanisha Moyo.

Basi ECTOPIA CORDIS...Ni Hali ya Mtu kuzaliwa na Kupata Sehemu Ndogo ya Moyo Au Moyo wote Kuwa Nje Ya Kifua.kawaida Moyo Unatakiwa uwe Ndani ya Mifupa ya Kifua ila kwa Ectopia Cordis Moyo Unakua Nje ya Mifupa ya kifua.

Mpaka sasa wataalamu hawajajua nini hasa chanzo cha tatizo hili hivyo wanaita ni Congenital yani Kitu cha Kuzaliwa Nacho ni Kisababishi Ni Idiopathic/hakijulikani.

Ila kwa Utaalamu Wangu Mdogo Juu ya Mambo Ya Afya Nahisi hii yaweza kutokana na Mama Kutopata Dawa za Madini chuma Kabisa au Kwa kiasi kidogo yani FOLIC ACID/FA na Ferrous Sulphate/FEFO kwani dawa hizi husaidia kuimarisha Mifupa ya kiumbe Kilichomo Tumboni.
Kwa wenzetu wazungu wakijua mama anakaribia/yupo kwenye Mpango wa Kubeba Ujauzito wanamwanzishia hizo dawa ila Kuepukana na Vilema Vingi kwa watoto kama vile Spinal Bifida/Mgongo wazi, Gastrochisis/Tumbo wazi, cleft&lil palate/mdomo Sungura...nk

Baadhi ni Vema pia Na kwetu Dada zetu/mama zetu kuanza Kliniki mapema pale unapojigundua tu Mjamzito.

Muwe na Jumapili Njema

Screenshot_20200329-162352.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom