Tuendelee kumchangia Lissu tuachane na CCM

Maneno mengi wakati msaada mnataka....hela ya kumtibu marekani kamwe hamna ndio maana mliandika barua umoja wa ulaya....
Ujinga tuu ndio mwajua..
 
Ni kweli kabisa. Na tulishawapuuza hao ccm. Mimi nimeishachanga na napanga tena wiki ijayo nikachange nyingine na ntaendelea kuchanga.
 
Hata wasemeje sisi tutachanga tu.
 
Ni kwel kabisa,Ccm ni wanafiki sijapata ona,maombi yenyewe yamezuiwa sembuse gharama za matibabu,hayo ni maaigizo
 
Kwa niaba ya waziri ummwi, nawatakieni usiku mwema
 
Kukubali kusaidia na adui yako ni kukubali kwamba kakushinda kwa kila kitu. Je ni kweli ccm imetushinda kwa kila kitu?? Tukatae hapana tena big HAPANA
 
Maneno mengi wakati msaada mnataka....hela ya kumtibu marekani kamwe hamna ndio maana mliandika barua umoja wa ulaya....
Ujinga tuu ndio mwajua..
Mnatukera sana nyie watu, yaani ni kama vile serikali ni mali ya hicho chama chenu. Hivi huwa hamjui kama na sisi tusio CCM huwa tunalipa kodi?
 
CCM wanaendelea na mission yao kuhakikisha Lissu anakufa kwa namna yoyote wanayoona inafaa.
Lissu atauawa kwa michango yenu ya jero jero.Kubalini mlikosea sana kukataa matatibabu ya serikali kwa kisingizo cha kuwa atauawa.
Sasa hivi hali imekua ngumu,mgonjwa anahitajika kusafirishwa nje,uwezo wa madaktari wa kenya umefika ukomo,bili inazidi kupaa,badala ya hata mkakope benki au mtumie ruzuku kumpeleka ughaibuni,mnafanya siasa
 
Lissu atauawa kwa michango yenu ya jero jero.Kubalini mlikosea sana kukataa matatibabu ya serikali kwa kisingizo cha kuwa atauawa.
CCM inamuona Lissu ni msaliti na kila mara mnauliza "msaliti huwa anafanywa nini" na kila mtu anajua nini mnachomaanisha.

Sasa hivi hali imekua ngumu,mgonjwa anahitajika kusafirishwa nje,uwezo wa madaktari wa kenya umefika ukomo
Madaktari hawajafikia ukomo bali hamu ya CHADEMA ni kutumia teknolojia ya juu zaidi iliyopo duniani kwa sasa kuhusu watu walioshambuliwa na risasi. Hata kama mnafurahia kwa mateso ya Lissu lakini jueni kwamba mmemfanyia jambo baya sana binadamu mwenzenu!

bili inazidi kupaa,badala ya hata mkakope benki au mtumie ruzuku kumpeleka ughaibuni,mnafanya siasa
Hoja yako hii inaleta mkanganyiko, tatizo ni hela ama madaktari wa Kenya wamefikia ukomo wa utaalamu wao kwenye kumtibia Lissu!?
 
Hoja yako hii inaleta mkanganyiko, tatizo ni hela ama madaktari wa Kenya wamefikia ukomo wa utaalamu wao kwenye kumtibia Lissu!?
Mgonjwa anahitajika kupelekwa ughaibuni,uwezo wa madaktari wa kenya umefikia ukomo,pesa ndio shida,chadema wanaona aibu kurudi serikalini kwa sababu walitukana sana na kashfa kibao.
Dawa ni kumkabidhi mgonjwa kwa familia yake,Chadema wanamshikilia mgonjwa kwa kupata kiki ya kisiasa tu,ndio maana kila aendae kumuona mgonjwa lazima apige picha
Hivi watu wote wanaokwenda kuona wagonjwa wao muhimbili wakiamua kupiga selfie kila mtu na mgonjwa wake mitandaoni kutakuaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…