Tubadili mitazamo katika ajira

bank

Senior Member
Joined
Jan 9, 2011
Posts
158
Reaction score
24
Nimeona watu wengi wanalalamika sana kuwa ajira ngumu katika hii forum

KATIKA YOTE AJIRA NI NGUMU SANA KUPATA SIKU HIZI NA NI BAHATI AU NI KWA NEEMA YA MUNGU TU HATA KAMA
UNA SIFA KIASI GANI.KWANI UNAKUTA NAFASI MOJA TU INAHITAJIKA WATU WANAOMBA 1500;SASA HATA KAMA WEWE NDIO HR UTAFANYAJE SASA,UNABAKI KUCHAGUA SAMPLE NDOGO NA KUITISHA USAILI.

UFUMBUZI NI KUWA: Wote tujiajiri na tuweke hali za shule pembeni tuache kusingizia mitaji.mtaji ni akili yako mwenyewe na TUACHE kujifanya kuwa kuna kazi za graduate na wasio hivyo.

Mfano ukiazima laki 2 ukienda kuchukua nanasi za laki moja ndani ya wiki uatakuwa umeingiza laki 2 nyingine ya ziada na tayari umerudisha deni na umepata mtaji wako.
Mimi mwenyewe ni graduate na nimefanya biashara ya mitumba mwenge stendi kwa mtaji wa laki na nusu tu ndani ya mwezi unaweza kukuza mtaji hadi laki 9.
Pia Pale kwenye mashamba ya umwagiliaji Ruvu-kwala unakodi shamba kwa elfu 50 unalima matikiti mfano garama ya eka 1 hadi unavuna ni 350,000/= na hapa ukiyauzia shambani unaingiza kuanzia shilingi milioni 1.5 hadi 2 kama utayeleta mwenyewe buguruni au kwingineko.Hapa pia nimelima mpunga mwaka jana na nimevuna na nategemea kupanda tikiti masika hii hivyo naongea vitu halisi.

Zipo kazi nyingi tu Hivyo tubadili mitazamo na tuache aibu wenzangu watanionaje fursa zipo na kutoka sio lazima ajira ya kuajiriwa tu
 
kweli mkuu hongera kwa kuwa na mawazo chanya na kuyafanyia kazi!!! kwa suala la kungoja kuajiriwa tutasubiri saaaana!!
 
Nilimalza chuo nikawa na pc yangu tu, nkaenda shule za kata na s/msingi, kumbe walimu cku hz nao mitihani hawapend kuandka ubaon kama kijijin kwetu hata test, NKAONGEA NA MKUU KUWA WANPE DILI LA KUTYPE NA KUPRINT, THANK MUNGU WAKANPA ILA WAKANIONYA USIR WA MITIHAN, HEEE KUMBE INADILI HIVI,nkanunua printer(3 in 1) hee page 1 ni buku. alafu bajet ya 4m1 tu ni kama kilo 4/5 ukipga had 4m4, niliwapga had sasa namilik kastastionary kangu,dogo anakapga kaz mm nazungusha bahasha wala cna presha.
 
Ila pia inategemea uko eneo lenye setting gan kimazingira na kibiashara kaka.
 
Well said mkuu,but ni wangapi wana idea kama yako,je elimu katika nchi zetu hizi inatuandaa katika hayo?,wewe ulipata hata wakukuazima iyo laki mbili je watu wote wapo tayari kukukopesha kama hukopesheki?
 
Nina degree ila kuna siku ntaacha kazi nijiajiri naona ata mwenye tigo pesa ananizid kimapato
 
Big up mwana ntakutafuta kaka nije kuona michakato ya Ruvu usihofu ntaweka wese kwenye gari private hadi Ruvu.
 
Bad enough unakuta mtu kasoma kilimo SUA ila analalama ajira ni ngumu huku akiwa hana hata bustani ya mboga kupractice alichokisoma kwenye hortculture chuoni,huu ni ukosefu wa ajira au akili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…