Kwa kila Mtanzania mwenye uchungu wa nchi yake, anayeona aibu umaskini uliozagaa na hali tuna utajiri kila pembe, anayewahurumia wazee na watoto wanaokufa kwa kukosa huduma za kawaida, anayependa kuona mateso, udhalili, kiburi, ulafi, rushwa, uongozi mbaya na uhalifu wa viongozi unatoweka kabisa nchini mwetu, anayependa kuona alfajiri mpya inachomoza Tanzania ambapo kila mtu anaishi kutokana na jasho la kazi yake halali.......
Napendekeza:
Tuanzishe data base ya viongozi wote na maovu wanayoyafanya tangu uhuru hadi leo.
Data base hii itaorodhesha maovu, mali zilizoibiwa na matendo mengine ya jinai yaliyofanywa na viongozi hao.
Kwa sharti : kila linaloorodheshwa liwe na ushahidi wa kutosha.
Hii data base itakuwa ni hoja kuuu ya viongozi waadilifu wanaokuja ya kuwafuatia watu hao na mali zao kwa shabaha ya kuwaadhibu na kutaifisha mali hizo, nje na ndani, muda tu atakapofika madarakani (kipindi cha siku 100)
Endapo watu hawa hawataadhibiwa, Tanzania haitajikwamua katika hali hii milele. Inabidi viongozi hawa waovu wajue tangu sasa kuwa kuna watu wanaofuatia na kusajili wanayoyafanya, kwa shabah ya kuwaadhibu. HALI HII HAITADUMU.