Tuanze mkakati huu

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,583
1,675
Kwa kila Mtanzania mwenye uchungu wa nchi yake, anayeona aibu umaskini uliozagaa na hali tuna utajiri kila pembe, anayewahurumia wazee na watoto wanaokufa kwa kukosa huduma za kawaida, anayependa kuona mateso, udhalili, kiburi, ulafi, rushwa, uongozi mbaya na uhalifu wa viongozi unatoweka kabisa nchini mwetu, anayependa kuona alfajiri mpya inachomoza Tanzania ambapo kila mtu anaishi kutokana na jasho la kazi yake halali.......

Napendekeza:

Tuanzishe data base ya viongozi wote na maovu wanayoyafanya tangu uhuru hadi leo.

Data base hii itaorodhesha maovu, mali zilizoibiwa na matendo mengine ya jinai yaliyofanywa na viongozi hao.
Kwa sharti : kila linaloorodheshwa liwe na ushahidi wa kutosha.

Hii data base itakuwa ni hoja kuuu ya viongozi waadilifu wanaokuja ya kuwafuatia watu hao na mali zao kwa shabaha ya kuwaadhibu na kutaifisha mali hizo, nje na ndani, muda tu atakapofika madarakani (kipindi cha siku 100)

Endapo watu hawa hawataadhibiwa, Tanzania haitajikwamua katika hali hii milele. Inabidi viongozi hawa waovu wajue tangu sasa kuwa kuna watu wanaofuatia na kusajili wanayoyafanya, kwa shabah ya kuwaadhibu. HALI HII HAITADUMU.
 
I beg to differ on tufanye nini. tujipange tutengeneze katiba ambayo ni kwa faida ya nchi na c makundi machache ya watu. katiba ambayo taasis zitakuwa huru na zenye kufanya maamuzi kwa haki bila ya kukwazwa kwa namna yoyote. katiba ambayo watawala wana madaraka machache sana na bunge na mahakama viko huru kabisa. katiba ambayo tume za uchaguzi ziko huru na hazijali kushindwa kwa mtawala aliye madarakani. katiba ambayo CAG ana nguvu na ana wajibika kwa watu kupitia kwa wawakilishi wao, bunge. Bunge ambalo haliangalii chama kilicho madarakani bali maslahi ya taifa. katiba ambayo DPP anakuwa na mamlaka ya kumshtaki hata rais wa nchi bila woga wala hofu. tukiipata hiyo, hizo data zitafanyikwa kazi na Tz itaondokana na umasikini tuliyomo
 
Nadhani tukifanya hivi vyote hata data base anayozungumzia mtoa mada itakosa au itakuwa haiongezeki,lakini ni great thinker anayefikiri namna mbadala ya kuisaidia tz yetu,kama hatutafanikiwa kuyafanya haya basi data base itafaa na itajaa sana,ingawa itatusidia kuwajua wezi lkn hatutaweza kuwafanya chochote kama ilivyo sasa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom