Tuamkeeee

mdiwani

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
236
186
Nilikuwa najaribu kutafiti ni faidi au hasara kwa Tz kuwanyima haki wazazi wa wenye passport za kigeni (Desporas). Niliangalia mfano mmoja, kila mtu anapostahafu hufikiria kurudi kwao na kuishi uzeeni. Nikichukua sehemu ndogo tu ya Desporas Uk utaona wako kati ya laki 3 mpaka 5. Kiwango cha pension kwa mwezi kiko kati ya 400 to 1000 £. Mfano ikiwa wastani ni 500£ kwa.mwezi hii ni 3000£ kwa mwaka x 300,000 inakuwa ni 900 million £ kwa mwaka. Hii ni hard cash itakayoingia Tz na kubadilishwa na kutumika ndani ya nchi.
Ndio maana nchi zote mpaka china huangalia vizazi vyake, wao husema passport ni kwa mahitaji lakini mchina ni mchina.
Tz itatupa pesa na nguvu zake bila kupata faidi kwa vizazi ilivolea.
Hiyo ni mfano wa uk pekee, je ukichukua wa tz wote dunia nzima ? Kiasi gani kitapotea? ?,
Uk watacheka sababu pesa hiyo itabaki kwao na kutumika kwao.
Hii ni moja tu ya faida zake lakini ziko nyingi ...
Tuangalie nchi kama philippines inao wazaliwa zaidi ya milioni 3 wenye passport za kigeni na wote karibu wanajenga nchi yao .
Pesa inayoingizwa ni big boost kwa economy ya nchi.
 
Back
Top Bottom