Nimekuwa msomaji ktk JF kwa muda mrefu sana. Na hii ni kati ya posts zangu za mwanzo kabisa. Ombi langu kwa wasomaji wa JF ni moja:- Kwa kuwa CCM wanamzungumzia sana mgombea urais kupitia UKAWA yaani Mh. Lowasa hasa kwa mabaya yake, basi na wanaomuunga mkono Lowasa nao waongee mambo mabaya ya Mh. Magufuli tuyasikie.
Nimeandika hivi kwa sababu kubwa mbili:- kwanza, naona wapinzani wanatumia nguvu nyingi kumchafua Rais Kikwete na familia yake ambaye amebakiza mwezi mmoja amalize kazi yake, pia wanapoteza mda mwingi kumponda Dr Slaa ambaye si mgombea urais, mambo ambayo kwangu naona hayana faida na ni kupoteza muda wao bure!
Sababu nyingine ni, mnatunyima wananchi haki ya kujua mabaya ya Magufuli maana yale mnayotuambia ya kuuza nyumba inaelekea sio yake bali la baraza zima akiwemo Lowasa na Waziri mkuu ​Sumae pia.
Wana UKAWA tajeni ubaya wa Magufuli tusikie maana kwa kuacha kuyataja mnatufanya tuamini kuwa Dr Magufuli ndiye anayefaa kuwa rais wetu wa awamu ya tano!