By; RASHID S. MBEGU
“Sasa nafurahi mkoa wangu ndo umekuwa wa kwanza kutekeleza, katika matembezi yangu haya wamenipeleka katika shule moja ya msingi pale chang’ombe. Nikafurahi sana kwa yale niliyoyaona. Na nina uhakika hawakunidanganya, wangenidanganyaje? Nimekuta wanafunzi wanashona nguo za watoto wadogo nzuri sana” maneno ya Mwalimu J.K Nyerere rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia viongozi wa chama na serikali wa mkoa wa Dar es salaam ukumbi wa diamond jubilee Juni, 25, 1976. Ni zama ambazo mwanafunzi wa shule ya msingi alifundishwa stadi za maisha, ili ajitegemee ili atapomaliza shule ajiulize “Nimeifanyia nini Tanzania?
Zama zimebadilika sana, yakale hayajatupendeza mbele ya macho yetu tumeachana nayo. Sasa mtoto wa shule ya msingi anafundishwa stadi za kazi darasani tena kwa peni na karatasi. Anajengewa fikra za kuja kuwa mwajiliwa toka anapoanza mtaala wake wa masomo na akimiliza shule anafikiria “Tanzania imenifanyia nini?” Hili ndilo lililonipelekea kuandika yote haya maana hakuna jibu sahihi wanalopewa wakalielewa. Taifa linandaa waajiriwa, halafu haliwaajiri.
Wakiwa katika lindi la mawazo na tafakuri, wanasikia sauti katika habari za siku kuwa waziri wa viwanda na biashara anawaomba vijana wawe WAJASIRIAMALI na wasibweteke na kusubiri kuajiriwa. Wakati wanajiandaa kulala wanasikia “malumbano ya hoja” na wenye dhamana ya nchi wanawaambia vijana njia ya kuwa mjasiliamali ni ndogo, kwanza kuwa na “wazo la biashara” pili aende kakope pesa benki upate “mtaji” alafu atakuwa ameshakuwa mjasiliamali. Vijana wanazima radio na kuanza kufikiria ni kiasi gani wamekosa upeo na kuwa wapumbavu kwa kutokuwa na “wazo la biashara” na kushawishi benki impe mkopo ilia pate “mtaji” wanapitiwa na usingizi katikati ya lindi la mawazo.
Hizi ndo zama M/Mungu ametupangia tuishi mimi na wewe, mtaji ni hela (money=capital). Inabidi watawala wajue kuwa “pesa” imekuwa sehemu ya maisha ya mwanadamu kwa takribani miaka elfu tatu sasa (karne 30), na neno “mtaji” (capital) limetokana na neno “ubepari” (capitalism) ambao umeingia katika sura ya dunia karne ya kumi na sita (16th century). Wanawezaje kulinganisha pesa na mtaji? Kwa nini pesa toka miaka elfu tatu iliyopita haikuitwa mtaji? Pesa sio mtaji kama inavyodhaniwa na wengi. Pesa kwenye minajiri ya biashara hutumika kununua bidhaa/malighafi na huduma ajiri ya matumizi na mtaji ni kitu kinachoishi kwa muda mrefu na kinachotumika kuzalisha mali kupitia uwekezaji.
Kwa dhana hiyo, hata muongozo na elimu wanaopewa vijana kuhusu ujasiliamali wanapotoshwa na sio ya kweli. Kumeibuka mtindo wa kukusanya vijana na kuwataka wawe wajasilimali na kuwapa semina elekezi za ujasiliamali. Je tumefanikiwa kwenye hilo? Unapomfundisha mtu biashara na kumwambia ni ujasiliamali ni kupoteza muda. Ndio usishangae biashara sio ujasiliamali. Hata kwenye semina hizo utakuta wanakupa mifano ya watu walioendelea kwa ujasiliamali alafu wanakutajia wakina Warren Buffet, Dr. Mengi, S.S Bakhresa kuwa ni wajasiliamali sio kweli na tuache kuwapotosha vijana, hawa ni wafanyabiashara na sio wajasiliamali.
Tumeshindwa kuwaeleimisha vijana biashara ni nini na ujasiliamali ni nini? Juhudi za serikali na taasisi binafsi za kufanya vijana wawe wajasiliamali zimeshindwa. Turudi kwenye mafunzo ya STADI ZA MAISHA kwa vijana maana tulifanikiwa. Turudishe mafunzo ya stadi za maisha mashuleni na kwa wale watakao faulu vizuri kwenye masomo ya kawaida tuwaache waendelee na elimu za juu lakini kundi litakaloshindwa endelea tuwaendeleze na ufundi stadi, tutakuwa tumelipunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa asilimia kubwa sana. Lakini kama tutendelea kuwaletea dhihaka za “ujasiliamali”. Kipawa cha ujasiliamali hajazaliwa nacho kila mtu, elimu ya biashara sio kila mtu anaweza kuitekeleza ila kufanya kazi kila kijana analiweza hilo.
Naona serikali imejifunza na juzi Mei 9 rais Dr. J.P Magufuli aliamuru mifuko ya hifadhi ya jamii iache kuwekeza kwenye majengo na iwekeze kwenye viwanda, huu ni ushindi ulio dhahiri kwa vijana. Kwa nijuavyo kila mfuko wa hifadhi ya jamii unawekeza zaidi ya bilioni 200 kwenye majengo na ardhi kwa mwaka, huu ni ushindi wa dhahiri kwenye sekta ya uzalishaji na sekta ya ajira. Haya ndio mambo ambayo vijana wanataka kuyasikia kwenye habari za siku na “malumbano ya hoja. HII NI NCHI YA WA WAFANYAKAZI NA WAKULIMA NA SI VINGINEVYO.