Tatizo kubwa ni milolongo mirefu ya maamuzi serkalini. Ukiwa serikalini hata kununua karatasi tu kuna mchakato wa kutisha, mafaili yanatembea kwa watu kibao. Pia tatizo lingine ni kuwa serikali ukiwa mbunifu au mchapakazi sana hakuna anayekutambua au hata kuthamini juhudi zako, mwisho wa siku wote mnakula ongezeko moja la mshahara na ikiwezekana mwenzako mzembe mzembe tu anapanda cheo kwa kufaamiana na watu huko juu. Mwisho wa siku kila mtu anafanya kazi kwa average performanceKwa nini watanzania hao hao wakiwa kwenye sekta binafsi wana perform kuliko wakiwa serikalini? Shida ni nini hasa?
Kama umewahi kutumia mtandao wao utakubaliana na mimi kuwa wapo vizuri hasa kwenye network ya internet.Duh, yaani ukiweka line nyingine ndo ushawapoteza! Yawezekana ndo sababu wanapanga eti watengeze simu za TTCL tu.
Nimeupenda sana utaratibu wa uwasilishaji. Naamini wamekusikia. Wafuate nyayo za HALOTEL, walianza kufungua milango ya nyumba za vijijini kabisa walivyotokea mjini wala hawakupata tabu ya kujitangaza, kazi hyo tuliifanya ssi wateja.Kiukweli nimekubali kuwa mzalendo na kurudi nyumbani ila sasa milango yenu bado umefungwa, kwa nini hamtaki kutufungulia Milango wakati Mmetuita wenyewe?
1. Nilirudi nyumbani pale arusha mjini na mambo yalikuwa poa sana tena nikapewa chakula kitamu cha 4G na mboga za kutosha yaani bundle za maana, kwakuwa natumia line ya chuo nikasema isiwe tabu ngoja nikale na masela wangu.
2. Nikatoka mjini kwenda tu USA river sikuamini macho yangu, nyumba ya Tengeru imefungwa, nyumba ya USA ndio hata kuruka ukuta huwezi, nikaona isiwe tabu, nikaja kwa Mromboo, nako hivyo hivyo, Unga limited nako hivyo hivyo, njiro nako hivyo hivyo dah nikachoka....
3. Kazi yangu ikaisha nikapanda bus, njia nzima toka Arusha mpaka Mwanza hakuna hata nyumba ya kuchimba dawa zote zimefungwa, labda mpaka ukifika stand kuu za mikoa, toka Mwanza kuja Mkoani kwangu ndio hata Nyumba ya kupata chakula cha mchana aipo kabisaaa....
4. Nimerudi wilayani kwangu uku Mkoa mmoja karibia na Burundi, hata kipeperushi cha Rudi nyumbani kumenoga sikioni, zaidi zaidi najifariji na tangazo la kwenye Azam Tv tu.
5. Hivi kwa style hii TTCL mtatushawishi turudi nyumbani, kama nyote mmeamua kuishi mjini tu, nyumba za pembeni mwa mji mmezifunga, au mnategemea wote tuhamie mjini kwenye nyumba moja, tutatosha kweli.
6. Hapa nipo Wilayani na Line yangu kwenye wallet, hata sijui nitarudi lini mjini ili nikafaidi TTCL, kiukweli ampo makini au mna kasi ya konokono, sidhani kama mna wilaya hata moja ya mikoani ambayo mmefika.
7. Mnashindwa na Halotel kampuni ya juzi? Wapo mpaka uku ndani kabisa kijijini kwetu tena tunapata H+, hacheni utani jipangeni
8. Nyumba yenu ya hapa wilayani imefungwa, mimi nipo nje hapa nasubiria mnifungulie, kwa kifupi siwezi kuwaangusha, nimeamua kurudi nyumbani ila mlango bado ina kufuli la chuma SOLEX
9. Tena hapa kwetu kuna mashirika mengi ya wakimbizi, mnaweza hata kujenga nyumba nyingine ikajaa wateja tena wateja wanaolipa kwa fedha za kigeni,
10. Fanyeni haraka mimi nipo hapa mlangoni la sivyo nitalala nje ya nyumba mpaka mtakapokuja kunifungulia, mmeniita wenyewe Nirudi nyumbani, kwanini hamfungui milango hasa nyumba zenu za wilayani? Tupeni taarifa ni Nyumba zipi zipo wazi za wilayani ili tusije lala nje tukienda uko.
RUDI NYUMBANI KUMENOGA
Nisaidie kushangaa!! Watanzania tumekuwa watu tunaoshindwa kabisa kuzijua na kuzikubali weaknesses zetu, sasa sijui tutajirekebishaje.Alafu akija CEO wa kenya mnamkataa eti ni mgeni mnasahau kwamba ana ujuzi wa kutosha. Huyo CEO wenu Omari Nundu ana matatizo gani?
ccm NI janga kama ilivyo UKIMWI wakiingia mahali wanakudhoofisha mpaka unakuwa kirusi.
They are not serious. Yes thats the truth.TTCL ni yetu ila hata ukiingia msalani unakuwa offline! Tatizo nini hasa? Nimerudi nyumbani ila wenyeji wananikimbia
Jaribu ISP wanaitwa habari node. Trust me hautajutia. This guys wana service nzuri ya internet, na bei nafuu kabisa.Si hayo tu Mimi nimeomba waje wanifungie huduma ya internet kwenye ofisi yangu, nimepeleka barua ya maombi kwenye ofisi yao iliyopo morogoro town sasa yapata mwezi sijawaona wakija hata kufanya savey ya eneo.Hawa watu bado sana ndio maana tunaenda kwenye mashirika binafsi
Tatizo kubwa ni milolongo mirefu ya maamuzi serkalini. Ukiwa serikalini hata kununua karatasi tu kuna mchakato wa kutisha, mafaili yanatembea kwa watu kibao. Pia tatizo lingine ni kuwa serikali ukiwa mbunifu au mchapakazi sana hakuna anayekutambua au hata kuthamini juhudi zako, mwisho wa siku wote mnakula ongezeko moja la mshahara na ikiwezekana mwenzako mzembe mzembe tu anapanda cheo kwa kufaamiana na watu huko juu. Mwisho wa siku kila mtu anafanya kazi kwa average performance
Kuripua.Ukisikia kocha ka-bet ndo hiyo, haiingii akilini mitandao inayochukulia kwao internet ni stable kuliko wao wanaoitoa. Nafikiri kuna kuripua flani wanafanya.
Natumia TTCL hiko ndicho ninacho kiona kwenye simu yangu aina ya CX air techno nikaisi labda haina ya simuPia nashindwa kuelewa kwa nini hawa TTCL wame-opt 3G na 4G wakaacha 2G, hadi sasa sielewi sababu za msingi za wao kutokuwa na 2nd generation. Simu ndogo huwezi access mtandao wao, ukibadilisha settings za network kwenye simu yako na kuweka line nyingine kutumia 4G Ile ya TTCL inakuwa kasha haina network.
Mkurugenzi wa TTCL ajitathmini coz hicho walichoamua hawatawafikia watu wa vijijini, lakini pia watalazimika kufunga 3G network systems nchi nzima(which is costly).
Walikuwa wanatest Maiki{Mike} hawana uwezo wa kushindana na Tigo na Voda comTTCL ni yetu ila hata ukiingia msalani unakuwa offline! Tatizo nini hasa? Nimerudi nyumbani ila wenyeji wananikimbia