Baada ya TTCL kunizungusha miezi mi4 nikaona nichukue Supakasi sasa hivi nimeanza kuona umuhimu wa kufuatilia Fiber tena maana nimeanza kula latency ya hovyo sana nikiwa nacheza game.
Rocket league halihitaji hata bandwidth kubwa 1Mbps inatosha lakini huwezi amini nikiwa nacheza game na mtu pembeni anatumia net tu kawaida hafiki 5Mbps huku kwenye game napata ping ya 450ms hadi 900ms, muda huo huo nikisema nidonwload kitu kwenye device nyingine speed inacheza kwenye 12Mbps hadi 17Mbps.
Ila nikidisconnect device zote napata latency ya 77ms hadi 98ms