TTCL acheni kutudanganya kuwa nyumbani kumenoga wakati hakujanoga

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,464
21,945
Msema kweli siku zote ni mpenzi wa Mungu maana Mungu hapendi uongo sasa hawa TTCL kila siku na mabango yanayosomeka nyumbani kumenoga rudi nyumbani!

Kiukweli kati ya makampuni ya simu yasiyojali wateja TTCL wameshika namba moja duniani hawajui wafanye nini ili wateja tufurahie huduma zao. Network ipo slow sana na haipo kabisa kwa maeneo kama Makabe, Msakuzi, Bunju Gezaulole nk.

T-Pesa nayo haina mawakala kila mtaa, mbaya zaidi computer za kampuni zinapoteza PIN namba za wateja hivyo ikitaka kutoa pesa zinajibu invalid pin number.

Mnakwama wapi enyi wazalendo TTCL? Mabeberu wapo vizuri kuwahudumia na kuwajali wateja wao.

Hakika nyumbani hakujanoga mie nimerudi kwa mabeberu endeleeni kuwadanganya wapenda mteremko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani me sina hamu nao ..Huduma kwa wateja mpaka leo wameshindwa kureset account ya t pesa, Licha ya kwenda shop yao pale nyamagana kilichonishangaza kbla ya kwenda niliwapigia huduma kwa wateja wakasema niende shop lao ndio watashungulikia. Nmeenda pale muhudumu nae ananambia hebu tupige makao makao makuu yeye hawezi kunisaidia kwani yeye ni kama wakala tu.
Nilimind sana yaani t shop kabsa afu muhudumu nae anasema eti ni wakala
Haya huduma kwa wateja huko makao makuu hawajafanya chochote kwa tatizo langu

-all is well-
 
Pole
 
Kwa upande wa internet wako best sana!! Kama mimi sijui kwa sababu labda niko town ila vifurushi vyao ni cheap na 4G

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa ni cheap...ila 4G yao ya hovyo kuliko. Mie niko dar hapa na nishawaacha..yani upo kwenye 4G lakini whatsapp voice call tabu..video call ndio usiseme. Nimehamia voda..gharama ni almost mara mbili ya ttcl lakini 4G ya quality. Hata 3G ya voda inazidi 4G ya ttcl
 
Back
Top Bottom