mzee wa liver
JF-Expert Member
- Dec 14, 2014
- 83,441
- 431,885
Wadau naomba kuuliza hivi ziara ya kwanza nje Marekani tangu awe rais wa Marekani Donald Trump ameamua kuchagua Saudi Arabia hii ina maana gani kwa siasa za dunia hii na mashariki ya kati
Sipingi inawezekana ikawa kwelimafuta mkuu!
Sipingi inawezekana ikawa kwelimafuta mkuu!
Asante kwa taarifa hii nazidi kuelimikaSaudi Arabia ni mmoja wa washirika wa nguvu sana wa US na wa miaka mingi. Kuanza na huko kunaonesha ushirikiano wao kuwa ni mkubwa.
Pia ukumbuke kiongozi wa kwanza kukutana na Trump alikuwa Waziri Mkuu wa Israel. Ndio wakaja wakina May wa Uingereza , Xi Jin Ping wa China na Al sisi wa Misri.
Angalia hayo mataifa vizuri .
Kama ni mfatiliaji wa siasa za kimataifa wala sio mageni yote hayo
Nimeona mkuu kwenye media jamaa amepewa hospitality ya hali ya juu kibaya zaidi naona hata mtoto wake Ivanka amechukua headlines sana kwenye ziara hii huyu jamaa kweli hajawahi kushindwa kwenye maisha yakeTembelea mitandao wamejadili kwa kina sana. Mosi, Trump na hela huwatenganishi. Pale Saudia pana hela ya bwerere mamwinyi wale hawajui waifanyie nini. Trump atawajengea maviwanda ya silaha ili wachinjane vizuri ukanda huo dili lenye thamani ya USD 350bn. Haijapata kutokea. Kwa dili hili hata kwa Shetani binadamu yeyote angeenda sembuse Saudia.
Pili, is more or less political. Eti wanasema anataka kuprove wrong wanaodai yeye ni adui wa Uislamu. So amechagua kuanzia Uislam ulipoanzia, the ataelekea nyumbani kwa Uyahudi (Israel); then home to Christianity (Vatican). He is strategic.
Tatu, ni onyo kali kwa Iran na program zake za kijinga. Anajaribu kuwagawa makundi; Iran and her allies vs Saudia and her allies. Hope umesikia mapendekezo yake huko.
All in all, haijawahi kiongozi yeyote wa dunia kupokewa kwa heshima na hadhi aliyopewa Trump huko Saudia.