kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,839
- 20,285
Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kutuma vikosi vya jeshi la nchi hiyo nchini Mexico.
Shirika la habari la Associated Press, limevujisha sehemu ya mazungumzo ya simu kati ya Trump na Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto wiki jana, ambapo rais huyo wa Marekani alitishia kuishambulia kijeshi jirani yake Mexico, iwapo nchi hiyo itashindwa kukabiliana na 'watu wabaya'.
Haijabainika iwapo Trump alikusudia wakimbizi au walanguzi wa mihadarati kwa kutumia neno 'watu wabaya; katika mazungumzo yake na Rais wa Mexico.
Aidha Ikulu ya Marekani ya White House imekataa kutoa taarifa kuhusu ripoti ya mawasiliano ya simu kati ya marais hao wawili, ambayo pia imechapishwa katika mtandao wa Mexico wa Aristegui Noticias.
Hii ni katika hali ambayo, wananchi wa Mexico wameanzisha kampeni maalumu ya kususia bidhaa za Marekani na wamefanya maandamano mbele ya ubalozi wa Marekani huko Mexico City, mji mkuu wa Mexico, kulaani hatua ya Donald Trump ya kuamua kujenga ukuta kwenye mpaka wa nchi hizo mbili ili kuzuia wakimbizi kuingia Marekani.
Rais Enrique Peña Nieto wa Mexico amewashukuru wananchi wa nchi hiyo kwa kuonesha mshikamano na mapenzi makubwa kwa nchi yao na kusema kuwa, hatua hiyo inapaswa kuwa jiwe la msingi la hatua za kiistratijia za ndani na nje ya Mexico.
Hivi karibuni Rais wa Mexico alifuta safari yake ya kwenda Marekani kukutana na Trump, katika kile kinachoonekana ni kuzidi kuingia doa uhusiano wa nchi mbili hizo, baada ya Trump kusema kuwa Mexico italipia gharama za kujengwa ukuta kati ya nchi mbili hizo.
RADIO TEHRAN