hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,253
- 26,641
TRUMP KAANZISHA MSALA MZITO-HORMUZ
Rais wa Marekani, Donald Trump ametoa kauli kali kuhusu nchi zinazotegemea lango la Hormuz.
Awali, aliwataka washiriki kulinda njia hiyo muhimu ya mafuta duniani, lakini wengi wao wakagoma kushiriki.
Sasa, Trump ameonyesha wazi kutoridhishwa na hali hiyo, akisema Marekani haitabeba mzigo huo peke yake, huku akiwataka wale wanaotumia njia hiyo kuchukua jukumu lao.
Katika hatua nyingine, mvutano umeongezeka baada ya mashambulizi dhidi ya miundombinu ya Iran, jambo linalovuruga utaratibu mzima wa biashara ya mafuta katika eneo hilo. Trump kasema baada ya mashambulizi:
“Najiuliza nini kingetokea kama tungeimaliza kabisa Iran iliyobaki, halafu tukawaacha wale nchi zinazotumia njia hiyo sisi hatuitumii wajibike kulinda mlango huo? Hiyo ingewalazimisha washirika wetu ambao hawachukui hatua kuamka haraka sana.”
Trump anamaanisha kuwa jeshi la Marekani lina uwezo wa kufuta kabisa kile kilichobaki cha miundombinu ya kijeshi na kiserikali ya Iran (ambayo tayari imedhoofika baada ya vifo vya Khamenei, Larijani, na Khatib). Hii ni tishio la kutumia nguvu ya mwisho ya kijeshi ili kuondoa utawala wa sasa mazima.
Anasema, "Sisi Hatuitumii Njia Hiyo" (We don't use it)
Hapa Trump anazungumzia Mlango-bahari wa Hormuz (Strait of Hormuz). Hoja yake kuu ni kwamba,
Marekani sasa hivi inajitosheleza kwa nishati (Energy Independent) na haitegemei mafuta yanayopita Hormuz kwa kiasi kikubwa kama zamani. Nchi zinazotegemea njia hiyo ni washirika wake (kama Japan, South Korea, na nchi za Ulaya) pamoja na mshindani wake mkuu, China.
"Wajibike Kulinda Mlango Huo" (Responsible for the so-called 'Straight'). Trump anamaanisha hawezi kulinda kwa damu na pesa njia ambayo faida yake kubwa inaenda kwa nchi nyingine. Kumbuka Trump ni mfanyabiashara, hapendi hasara.
Maana yake, anataka nchi kama China, Uingereza, Ufaransa, na Japan zitume manowari zao za kivita kulinda meli zao za mafuta badala ya kuitegemea Marekani pekee.
Anawasilisha ujumbe kuwa, kama washirika hawataki kusaidia kulinda meli zao, basi Marekani inaweza "kumaliza kazi yake" na kuondoka, kisha kuziacha nchi hizo zihangaike zenyewe na vurugu zitakazobaki hapo. Na zaidi amesema akuwaita waisaidie Marekani bali wajisaidie wao, hivyo haitaji msaada wao.
WATEGEMEZI WA MLANGO WA HORMUZ
Marekani: takriban 5%
Israeli: karibu 0%
Ulaya: 20% – 25%
ASIA (NDIO WAKUBWA)
China: takriban 40%
India: hadi 80%
Japan: 85% – 90%
South Korea: 70% – 80%
Pakistan: 60% – 70%
Thailand: 50% – 60%
Philippines:40% – 50%
Korea kusini na Japan wao wametangaza kuwa wanayo akiba kubwa ya mafuta.
Hakika kama Tanzania tungekuwa tumechimba mafuta na gesi ingekuwa katika utaratibu mzuri, huu ndio ulikuwa muda wa kutengeneza pesa za kutosha. Kufa kufaana, wahenga wanasema. Lakini ndio hivyo tena.
Na Jeff