Trump: I will make Americans great, Magufuli: Nitawafanya muishi kama mashetani.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,812
48,995
Hii ndiyo tofauti ya kiongozi na mtawala.

Wengi wanalaumu jinsi Trump anavyoongoza wanasema kuwa ana ubaguzi. Lakini mimi naona ubaguzi wake ni wa kuwafanya wananchi wake (indigenous citizens) waishi kwa usalama, wapate kazi.

Tofauti yake na rais wetu, yeye anataka wananchi wake waishi kwa shida, kama walijitajidi kujenga kajumba anakabomoa, kama ulikuwa na shamba utanyang'anywa au utaambiwa usilime, na kama ulijitahidi kupata mali atahakikisha unafilisiwa uishi kama mashetani (wananchi) wengine wanavyoishi.
 
Kauli ya kusema watu waishi kama mashetani hakumaanisha wenye vipato halali
Aliitoa wakati akipamba na wapiga dili wala rushwa na wakwepa kodi hasa kipindi anafuatilia ukwepaji kodi bandarini
 
Huyu Rais wetu inaweza kuwa tulimtenda Mungu dhambi sasa katuadhibu kwa kupitia yeye
 
Yeye alisema mafisadi na mapiga dili yalikuwa yanaishi kama malaika kwa kuiba mali ya watanzania ndiyo atayafanya yaishi kama ibilisi
 
Two countries two different philosophies, na kwa kuwa wote wawili JPM na the Trump watarudi kilingeni kwenye uchaguzi 2020; tusubiri tuone nani atakuwa amefanikisha sera yake vizuri zaidi ya mwenzie!
 
Yeye alisema mafisadi na mapiga dili yalikuwa yanaishi kama malaika kwa kuiba mali ya watanzania ndiyo atayafanya yaishi kama ibilisi
Kingsharon92 huyo fisadi ni nani? Ww unamjua? Tumekupa mapolisi,Jeshi na hela zetu zote unashindwaje kumkamata huyo fisadi? "Hakuna kitu kibaya kama kuendesha nchi kwa chuki"" Siyo maneno yangu maneno ya Hashim Rungwe(CHAUMA).
 
Kadhi are you sure of your statement? Unajua kuna kijiji kimoja musoma baba aliwatoroka mama na watoto na baadaye mama naye akasepa? Hatimaye watoto wakaamua kumchinja mbwa ambaye walimkausha na kumla. Lakini your president does not care
 
Acha upotoshaji! Magufuli alimanisha wapiga dili ndio wataishi kama mashetani! mambo mengine yanayotokea kama ukame ni vitu vya kumuomba Mungu atusaidie! tusipende kulaumu!
 
Back
Top Bottom