Trump Ataka Urusi Irejeshwe G8

Trump Ataka Urusi Irejeshwe G8

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,957
44141716_503.jpg

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa wito mpya wa kuirudhisha Urusi katika kundi la mataifa yaliostawi zaidi kiviwanda duniani, licha ya kukumbana na upinzani mkali kwa pendekezo lake kutoka kwa wenzake nchini Canada.
"Nadhani ingekuwa jambo la manufaa kuirejsha Urusi," Trump aliwaambia waandishi habari kabla ya kuondoka kwenye mkutano wa kilele wa kundi la mataifa saba yalioendelea zaidi kiviwanda.

"Nadhani ingekuwa vizuri kwa Urusi, Nadhani lingekuwa jambo zuri kwa Marekani, nadhani ingekuwa vizuri kwa mataifa yote ya kundi la sasa la G7. Nadhani G8 ingekuwa bora. Nadhani kuirudisha Urusi lingekuwa jambo zuri. Tunatafuta amani duniani. Hatutafuti kucheza michezo."

Pendekezo la Trump la kuirejesha Urusi ndani ya kundi -- ambalo alilitolea mjini Washington muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda Canada -- lilikataliwa mara moja na wanachama wa G7 kutoka barani Ulaya, zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Ujerumani katika siku ya kwanza ya mkutano huo.

Urusi ilitimuliwa katika kundi lililokuwa wakati huo G8 baada ya hatua yake ya kulitwaa kimabavu eneo la Crimea mwaka 2014, hatua iliolaaniwa pakubwa kama shambulizi dhidi ya mamlaka ya kujitawala ya Ukraine.
DW
 
Ha haha haha wataelewa tu "" kwanni Ikulu ya Kremlin ilitumika kudukua uchaguzi wa USA ""...
 
Trump anaogopa Putin asiendelee kuchukua maeneo ya Ukraine
 
Hivi Nini faida ya G7.....mbona mataifa mengi tu yanaishi vzr bila hata kufuatilia habari ya G8 siju G7....
 
Safi sana mzee wa wigi,Putin Yuko poa mrudisheni faster
Nalog off
 
Back
Top Bottom