Trump ashutumiwa

joo_73

Member
Feb 8, 2017
88
67
Viongozi wa chama cha Democratic nchini Marekani wamemshutumu Rais wa Marekani Donald Trump kuandika kwenye Twitter akishutumu maduka ya jumla ya Nordstrom kwa kuacha kuuza nguo za kampuni inayomilikiwa na bintiye.

Bw Trump aliandika kwenye Twitter kwamba "Ivanka ameonewa sana" na maduka hayo.

Seneta mmoja wa chama cha Democratic amesema hatua hiyo "haifai" naye afisa mmoja wa zamani wa maadili katika ikulu ya White House alisema "ni ya kushangaza".

Mapema mwezi huu, maduka ya Nordstrom yalikuwa ya tano kuacha kuuza mavazi ya kampuni ya Ivanka Trump, kwa walichosema kuwa ni kushuka kwa mauzo.

Wasifu wa Trump, rais wa MarekaniPicha tano za kusisimua mkutano wa Trump na ObamaWatakaoumia na watakaofaidi chini ya Trump Marekani

Hatua hiyo imechukuliwa huku baadhi ya watu wakiwasihi wateja kususia bidhaa za Trump.

Wanahakati wamepatia kampeni yao jina [HASHTAG]#GrabYourWallet[/HASHTAG] (Twaa pochi lako), wakirejelea matamshi ya Bw Trump mwaka 2005 kuhusu wanawake.

Msemaji wa seneta wa Pennsylvania Bob Casey alisema seneta huyo "anahisi ni ukiukaji wa maadili na hatua isiyofaa kwa rais kushambulia kampuni ya kibinafsi kwa kukataa kutajirisha familia yake".

Norm Eisen, ambaye alihudumu kama afisa wa maadili katika ikulu ya White House chini ya Rais Barack Obama, alisema hatua hiyo ni "ya kushangaza" na akawashauri Nordstrom kumfungulia kesi Bw Trump chini ya sheria za California kuhusu ushindani kibiashara.
 
Ethicaly kama rais alikosea,
man!! Huyu jamaa hajawahi hata kuchaguliwa kuwa monitor darasani. Hajui siasa zinaendeshwaje bado.nashangaa waandishi wa habari hasa wa CNN walishangaa utadhani yesu karudi kumbe ni ishu ndogo tu
He'll learn mbel kwa mbele though i doubt if he will.
 
Back
Top Bottom