Trump afanikiwa kubadilisha huduma ya Obamacare Bungeni

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
  • Rais Trump amesema kuwa ana matumaini makubwa kwamba sheria itakayochukua mahala pake huduma ya afya ya Obamacare itapitishwa katika bunge la seneti, baada ya kuidhinishwa na bunge la uwakilishi.

Trump aliyasema hayo wakati alipokuwa akisherehekea ushindi wa kura hiyo.

Wanachama wa Republican wanawapiku wenzao wa Democrat kwa wingi katika bunge la seneti, ikiwemo baadhi ya maseneta ambao wanataka mabadiliko muhimu katika sheria hiyo.

Mwandishi wa BBC mjini washington anasema kuwa muswada huo uliharakishwa ili kuzuia gharama yake ,na idadi ya watu watakaopoteza bima zao za afya haijulikani.

=====

Washington (CNN): In a major victory for President Donald Trump, the House has voted to dismantle the pillars of the Affordable Care Act and make sweeping changes to the nation's health care system.

The bill now heads to the Senate where it faces daunting challenges because of the same ideological splits between conservative and moderate Republicans that nearly killed it in the House.

Trump said he is confident the bill will pass the Senate, calling Obamacare "essentially dead."

"This is a great plan. I actually think it will get even better. This is a repeal and replace of Obamacare. Make no mistake about it," Trump said at a celebratory White House appearance with House Republicans.

After a dramatic week of negotiations, lobbying from Trump and Republican leaders, the vote ended with 217 GOP lawmakers backing the measure. Twenty Republicans opposed it, as did all House Democrats.

Trump argued the health care process has unified the GOP. "We've developed a bond," he said. "This has really brought the Republican Party together."

"As far as I'm concerned, your premiums are going to come down," Trump said.

Democrats were unable to stop the GOP vote aimed at President Barack Obama's signature legislative achievement. But after the final vote was cast, they chanted "nah nah nah nah hey hey hey goodbye" to their Republican colleagues, with a few members waving, as they believe the vote will lead to many GOP lawmakers losing their seats in the November 2018 midterms.

Thursday marks a political milestone -- one that has painfully eluded Trump and House leaders for months. The controversial health care bill delivered Trump the biggest political defeat of his short presidency in March, when the legislation had to be yanked from the House floor because it simply didn't have enough support.

Under pressure from an antsy Trump looking to score a big political victory, Republican leaders tried again last week, hoping to to get to 216 votes ahead of the President's symbolically important 100-day mark in office. That effort, too, failed.

Source: CNN
 
Ukakasi wa Obamacare ni pamoja na jina lake.
Bima nzuri lakini kwa jina lako?
Obama nae hapo alibugi step sana.

Unataka uwe una "jibosti" na vijukuu vyako
Jina la sheria hiyo ni Affordable Care Act. Jina la "Obamacare" HALIKUTOKA KWA OBAMA AU WASHIRIKA WAKE. Lilitoka kwa wapinzani wake wa Republican Party. Ndiyo hapo tunasema kuna lugha ya ishara ambayo ni lazima uichunguze kwa ndani zaidi kuielewa. Republicans walitohoa jina hilo si kwa kumsifia Obama, la hasha. Walitoa jina hilo kama ishara kwa wale wabaguzi wote ambao walikasirishwa na mtu mweusi kwenda White House. Hivyo basi wakisikia tu jina hilo wanakereka. And it worked beautifully. Kuna watu wengi ambao wanaipenda sana ACA lakini hawaipendi Obamacare, ilhali ni kitu kile kile. Unaona eh? Habari hizi unaweza kuzipata hata Wikipedia.
 
Sasa wale wabadili jinsia na watoaji mimba watafute bima zao..
Kwa maana bima mpya hakutakuwa na vipengele hivyo
Kama kweli Obamacare au ACA ilikuwa kwa ajili ya watoaji mimba na kubadili jinsia, basi kweli sasa wana taabu kubwa. Lakini nachelea kwamba ukweli wa mambo uko mbali kabisa na hisia zilizoelezwa hapa. Wikipedia inaweza kueleze kwa kifupi vizuri zaidi. Taabu kubwa au athari kubwa ya kufutwa kwa Obamacare ni watu zaidi ya milioni 24 kukosa bima. Samahani hawa si wabadili jinsia au watoa mimba. Ni watu wa kipato cha chini. Kwa mfano watu wanaofanya kazi za kima cha chini wengi huajiriwa kwa masaa. Hao hawalipiwi bima na waajiri. Obamacare ilikuwa njia ya kuwalipia. Athari nyingine kubwa inayolalamikiwa ni wale wenye pre-existing conditions. Kwa mfano ikigundulika kwamba una hitilafu fulani ya kiafya katika mwili wako (km kisukari, ugonjwa wa kuzaliwa nao, nk), bima za afya zinakataa kukuandikisha. Obamacare ilifuta zuio hilo na kuzitaka bima kuwahudumia watu wote bila kujali matatizo ambayo wanayo. Sasa hiyo itapotea na kurudi kule kwa zamani. Kuna majimbo mengi makampuni ya bima yalikuwa yanaweza kufuta bima baada ya kugundua kwamba sasa una ugonjwa utakaohitaji tiba za muda mrefu. Obamacare ilipiga marufuku hilo na kuweka pesa za ruzuku kusaidia watu hao. Mifano mingi inaonekana sehemu zile zenye machimbo ya makaa ya mawe ambako kuna ugojwa wa "black lungs." Watu hao waliomchagua Trump kwa wingi sasa wanahaha kwa sababu matajiri wanaotetea biashara zao za bima sasa wamerudi kwa nguvu nyingi na kuivunja Obamacare. Si jambo la kushangilia hata kidogo kwa mtu mwelewa.
 
Ukakasi wa Obamacare ni pamoja na jina lake.
Bima nzuri lakini kwa jina lako?
Obama nae hapo alibugi step sana.

Unataka uwe una "jibosti" na vijukuu vyako
Sioni ubaya wa jina "Obama care" ilikuwa ni Sera tu
 
Hivi Obamacare ina ubaya gani? mbona inachukuliwa na Trump kuifuta ni kama ukombozi flani ningependa mtu yeyote mwenye kuelewa kiundani anieleweshe pls.
Maana nnavyojua huku ulaya huduma ya afya ni bure kila mtu lazima awe na bima ya afya nashangaa inakuaje ni kitu kibaya kwa U.S
 
Trump amethibitisha bila kuacha shaka kuwa yeye ni mbaguzi ila ametumia ujanja wa kisiasa kuficha ila wengi wameelewa ni mbaguzi mkubwa anataka kuhakikisha anaondoa athari ya obama marekani.anaondoa kitu ambacho yeye lazima akifanye sasa ni nini kama sio roho mbaya ya kizungu
 
Kama kweli Obamacare au ACA ilikuwa kwa ajili ya watoaji mimba na kubadili jinsia, basi kweli sasa wana taabu kubwa. Lakini nachelea kwamba ukweli wa mambo uko mbali kabisa na hisia zilizoelezwa hapa. Wikipedia inaweza kueleze kwa kifupi vizuri zaidi. Taabu kubwa au athari kubwa ya kufutwa kwa Obamacare ni watu zaidi ya milioni 24 kukosa bima. Samahani hawa si wabadili jinsia au watoa mimba. Ni watu wa kipato cha chini. Kwa mfano watu wanaofanya kazi za kima cha chini wengi huajiriwa kwa masaa. Hao hawalipiwi bima na waajiri. Obamacare ilikuwa njia ya kuwalipia. Athari nyingine kubwa inayolalamikiwa ni wale wenye pre-existing conditions. Kwa mfano ikigundulika kwamba una hitilafu fulani ya kiafya katika mwili wako (km kisukari, ugonjwa wa kuzaliwa nao, nk), bima za afya zinakataa kukuandikisha. Obamacare ilifuta zuio hilo na kuzitaka bima kuwahudumia watu wote bila kujali matatizo ambayo wanayo. Sasa hiyo itapotea na kurudi kule kwa zamani. Kuna majimbo mengi makampuni ya bima yalikuwa yanaweza kufuta bima baada ya kugundua kwamba sasa una ugonjwa utakaohitaji tiba za muda mrefu. Obamacare ilipiga marufuku hilo na kuweka pesa za ruzuku kusaidia watu hao. Mifano mingi inaonekana sehemu zile zenye machimbo ya makaa ya mawe ambako kuna ugojwa wa "black lungs." Watu hao waliomchagua Trump kwa wingi sasa wanahaha kwa sababu matajiri wanaotetea biashara zao za bima sasa wamerudi kwa nguvu nyingi na kuivunja Obamacare. Si jambo la kushangilia hata kidogo kwa mtu mwelewa.
Wamarekani wamezidi ubepari yani U.S ndio kwenye reality ya Capitalism ndio Maana always nawakubali wafaransa when it comes to social services they are the best
 
Hivi Obamacare ina ubaya gani? mbona inachukuliwa na Trump kuifuta ni kama ukombozi flani ningependa mtu yeyote mwenye kuelewa kiundani anieleweshe pls.
Maana nnavyojua huku ulaya huduma ya afya ni bure kila mtu lazima awe na bima ya afya nashangaa inakuaje ni kitu kibaya kwa U.S
Kwa watu wa Ulaya, Canada na Australia, mambo ya Marekani ni ya kustaajabisha kabisa. Watu wengi Marekani, hasa kama hawajawahi kusafiri nje ya Marekani, hudhani kwamba hapa duniani Marekani ni namba wani katika kila kitu. Hata Obamacare ilipita kwa mbinde huku wengine wakisema waziwazi kwamba "sasa mnataka kuifanya Marekani iwe kama Ulaya." Kana kwamba hicho ni kitu kibaya. Republicans wanapenda sana kutumia ignorance ya watu.
 
Ukakasi wa Obamacare ni pamoja na jina lake.
Bima nzuri lakini kwa jina lako?
Obama nae hapo alibugi step sana.

Unataka uwe una "jibosti" na vijukuu vyako
Inaitwa Affordable Health Care Act. Obama care ni jina la kiutani.
Hii mpya inaitwa Trump Care. Kiutani.
 
Kwa watu wa Ulaya, Canada na Australia, mambo ya Marekani ni ya kustaajabisha kabisa. Watu wengi Marekani, hasa kama hawajawahi kusafiri nje ya Marekani, hudhani kwamba hapa duniani Marekani ni namba wani katika kila kitu. Hata Obamacare ilipita kwa mbinde huku wengine wakisema waziwazi kwamba "sasa mnataka kuifanya Marekani iwe kama Ulaya." Kana kwamba hicho ni kitu kibaya. Republicans wanapenda sana kutumia ignorance ya watu.
Kweli kabisa hilo ni tatizo la watu wengi ambao marekani ndio inakuwa nchi yao ya kwanza kufika wanaona hakuna nchi kama ile ila ukweli ni kwamba serikali za nchi za ulaya Australia na Canada ziko juu sana kwenye nyanja nyingi kihuduma kwa wananchi wao kuliko U.S
 
Back
Top Bottom