true story:wanaume sisi ni waajabu sana

appoh

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
5,259
2,166
WANAUME TUNATIA AIBU SANA WAKATI
MWINGINE HEBU TUJIREKEBISHE
Mwanaume mmoja hapa mtaan kwetu aliwatongoza wanawake
watatu tofauti na nia yake ni kufanya upembuzi
yakinifu ili mmoja wao awe mkewe. Hivyo jamaa
aliamua kuwapa jaribio kwa kuwapa Tsh.
500,000/= kila mmoja huku akitaka kujua ni
namna gani watazitumia.
Mwanamke wa kwanza alitumia pesa yote
kununua vipodozi. Alitembelea duka la vipodozi
na urembo akajikwatua sawa sawa! Alivyorudi
kwa mchumba wake akamwambia,
"nimeamua kutumia pesa yote kwa ajili ya
kujipamba ili nizidi kukupendeza
machoni pako na kukuvutia maana nakupenda
sana."
Hakika yule mwanaume akapendezwa sana na
mpenzi wake.
Mwanamke wa pili alinunua zawadi kwa ajili ya
bwana wake. Alinunua simu mpya kwa ajili ya
bwana wake, saa ya kisasa, nguo na viatu vizuri.
Alivyofika kwa bwana wake alimwambia,
"pesa yote nimeitumia kununua hizi zawadi zako
maana nina kupenda sana."
Jamaa akafarijika sana
Mwanamke wa tatu aliwekeza zile pesa kwenye
soko la hisa na baada ya muda fulani alipata
faida ya shilingi 2,000,000/=. Mwanamke yule
aliamua kumrudishia bwana wake ile pesa
aliyokuwa amepewa yaani laki 5 na pesa
iliyokuwa imebakia alifungua akaunti ya pamoja
na bwana wake. Kisha yule mwanamke
akamwambia yule jamaa,
"nahitaji kuwekeza na kuhifadhi kesho yetu kwa
sababu nakupenda sana."
Hakika yule mwanamke alimfurahisha sana
jamaa.
Jamaa akatafakari sana yale ambayo yalikuwa
yamefanywa na wale wanawake baada ya kupewa
laki 5. Lakini mwisho wa siku jamaa aliamua
kumwoa mwanamke mwenye makalio makubwa!
na kumuacha aliyemrudishia pesa kweli Wanaume
tutabakia kuwa wanaume tu
 
Back
Top Bottom