Pettymagambo
JF-Expert Member
- Aug 21, 2017
- 1,532
- 8,280
- Thread starter
-
- #721
Kumekuchaa...109
Mke wa huyu mzee inaonekana amehusika na upotevu wa mjukuu wao na kifo cha kutatanisha cha kijana wao wa kiume.
Lakini dira zikaeleza sababu ya mama yule kumwua mwanae ni baada ya kijana yule kumwona mama yake akifanya kitendo cha kinyama kwa mjukuu wake ambae juzi alikamatwa na fisi mapema jioni, alieleza mzee yule na kuendelea,
Kilichotuleta hapa, dira yetu imekuona wewe ndo umesababisha ugonjwa wa huyu mama na mzee mwingine hapa kijijini kwa pigo ulilowapa, naam tunaomba utueleze bila kuficha chochote yale ambayo uliyaona mpaka kupelekea vita na wewe kuwaumiza hawa wau, alimaliza mzee yule.
Nashindwa hata nisemeje wazee wangu, yaani yote mloyaongea hapa hakuna hata moja nalolijua, nipo hapa leo siku ya 4 tu, na nimekuwa mtu wa kukaa hapa nyumbani bila kutoka, na kuhusu mambo ya nguvu za giza sijui hata dawa moja, nilijitetea kwa kujiamini.
Hapana mwanangu, tunaomba utusaidie ili tumsaidie kijana mwenzio ambae yupo katika hali mbaya na tunahitaji uthibisho wako kwa aliyosemani eti mamaye mchawi?
Dah umewapatia pigo la haja...111
Huku nje nilibaki na yule mzee mme wa yule mwanamke mchawi ambae ilisemekana yu hoi kitandani kutokana na pigo nililowapatia.
Mwanangu unanafasi ya kumsaidia kaka yako ambae ilikua azikwe jana, lakini kutokana na hali aliyokuwa nayo ya kutokwa damu puani, masikioni na mdomoni ingali akiwa amekufa ilitushtua na nikakata shauli asizikwe ili niite wataalam ambo walifika muda si mrefu na kufanya utaalam wao uliopelekea kijana wangu akarudiwa na pumzi...!
Babu na wale wazee wawili walitoka ndani mwangu huku wakionekana kukosa tumaini lolote.
Hakuna tulichokipata ndani ya nyumba ya huyu kijana, japo naamini kuna kitu anatuficha lakini hatuna namna zaidi ya kuondoka tukashuhulike na mgonjwa wetu, alisema mzee mwongeaji.
Wazee wenzangu, kijana wangu huyu katoka mjini juzi tu, hajui chochote huyu, alinitetea babu yangu.
Anaweza akawa hajui chochote lakini akapelekwa kwenda kuoneshwa mambo ya giza na anayejua kama ilivyotokea kwa huyu kijana ambae amenusurika kufa, alisema mzee mwongeaji huku wakiondoka.
Halafu wewe ndo Yunge mkubwa sasa... Au bibi yake Jamaa? Mchana unajifanya mtu mwema kumbe usiku kigagula.Wachawi hawataki mambo yao yawekwe wazi,bila shaka huyu Chizi ni dada ake Yunge mdogo
Yunge mdogo atakuwa anataka kupasuka baada ya kusikia haya maneno...112
Huyu binti ni kiboko yao, sasa kama upembe tu umewalaza vitandani wale wachawi wawili, je akiamua kunigeuza bundi si itakuwa kufumba na kufumbua tu? Niliwaza sana.
Nilijikuta nammis sana yunge mkubwa, kitendo cha kuwajeruhi washirika wake kisa wasiniguse mimi kilinipa kichwa na kujiona kweli mzee mzima napendwa.
Hisia nzuri za kimapenzi juu yake ziliniijia kichwani na kujikuta natabasamu mwenyewe.
Kupendwa raha jamani, yaani mtu anakuwa tayari kuumiza wengine kwa ajili ya ampendae tu, hapa niliamini maneno alonambia kwamba hakuna mtu atakugusa nzehe.
Mbona unatabasamu mwenyewe huku umetizama juu, kuna malaika unaongea nae nini, ilikuwa ni sauti ya yunge mdogo akishangazwa na ninavyotabasamu mfululizo bila uwepo wa mtu mwingine.
Basi tu! Nilijibu.
Vipi umemmisi bi mkubwa nini? Aliuliza yunge mdogo.
Kiukweli nimemmisi yunge mkubwa, nimemmisi sana, natamani nimkumbatie, nahisi ananipenda sana yule msichana, hata mimi nampenda pia, ndio nampenda mno, niliongea mfululizo kwa hisia kali sana.
Vipi bado umesimamia kauliyo?Una uandishi mbovu kinoma yaaani hadi kero
Hivi unatumia Simu ya kitochi kuandika? Mbona unaandika fupifupi sana mzee mchawi kwanini?Vipi bado umesimamia kauliyo?
Tulia we mku ndu guWewe mdogo usie na kiherehere cha kunijibu na umeelewa nambie top 20 ilikua saangapi na sports round up ikafuatia ikiwa saangapi? Kama ni facts basi ziwe facts