hewamkaa
Member
- Mar 30, 2023
- 96
- 135
Haya ni mambo kama una mpango wa kwenda USA kama mtalii/visitor
1) Lazima upate visa kwa kufuata mchakato maalum uliowekwa
2) Ukipata visa, let's say ya mwaka mmoja, ndipo unapoweza kuanza safari.
3)Epuka kubeba vitu visivyoruhusiwa kwenye mizigo yako.
4)Usibebe mimea au mbegu hasa zilizokuwa packed special.
5)Zawadi za vyakula kama mchele, na nafaka zingine, zinakaguliwa sana wakati wa arrival. Kama kuna wadudu au uchafu ambao haueleweki, vitazuiliwa na kumwagwa.
6)Uwe na ufahamu wa nini kiko kwenye mabegi yako muda wote, kwani unaweza kuulizwa na afisa yeyote wa usalama.
7)Kwenye port of arrival, afisa uhamiaji atakuuliza nia ya safari yako na muda unaotarajia kukaa. Mwisho atagonga mhuri passport yako na kuandika yeye mwenyewe, kwa mkono, tarehe yako ya kuondoka Marekani. Afisa ana uhuru wa kukupa siyo zaidi ya miezi sita. Chunga sana hii tarehe.
Ndani ya USA
1)HUTAWEZA kufanya ajira bila Social Security. Japo kuna baadhi ya maeneo utaweza kwa kujifichaficha. Hutakuwa huru. Unaweza kufanya kwa jina la mtu mwingine, lakini wengi wametapeliwa. Na ikitokea ukaulizwa vibali na afisa wa usalama, unaweza kuingia kwenye matatizo. Kumbuka, wazungu ni wanoko sana.
2)Barabara zao wanaendesha kulia.
-wako makini sana kwenye Road crossing na njia za reli. Hata kama utajikuta peke yako kwenye crossing, lazima u-behave.
-Ukikutana na gari la polisi lenye king'ora au fire na ambulance, sheria inakutaka u-park pembeni. Hii ni lazima.
-Makosa yoyote ya barabarani, faini yake ni kubwa.
-Ukisimamishwa na polisi wakati unaendesha gari unafanya yafuatayo->
---Simama na usitoke ndani ya gari
---Weka mikono yako juu ya stearing.
----Jibu maswali yote utakayoulizwa. Usijaribu kubishana na security officer.
----Kama ukiombwa leseni, na iko mfukoni au kwenye pochi, lazima umuombe security ruhusa ili uweke mikono mfukoni au ushike pochi yako. Kufanya hivyo bila ruhusa, unaweza kuhatarisha maisha yako.
Tutaendelea kuelimishana