Transfer Window 2014/2015, Special thread

kichwat

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2010
Posts
1,819
Reaction score
591
YALIYOJIRI DIRISHA LA USAJILI 2014/15 - BIG SIGNINGS


MANUTD
- Hatimaye KILLER Radamel Falcao (28) ametua ManUtd kwa mkopo wa msimu mmoja, kwa dau la £6m na mshahara wa £350,000 kwa wiki (£184,000 baada ya kukatwa kodi). ManUtd itaruhusiwa kumnunua jumla kwa kitita cha £74m.
- Javier Hernandez (CHICHARITO, 26) ametua Real Madrid kwa mkopo.
- Playmaker Shinji Kagawa (25) amerudi Borrusia Dortmund kwa dau la £8m.
- Beki Daley Blind (24, Holland) ametua ManUtd kwa dau la £13.8m
- Winga anayetisha Angel Di Maria (26) amekamilisha usajili Old Trafford kwa dau la £59.7m.
- Mkoba Marcos Rojo (16) ametua ManUtd kwa dau la 16m kutoka Sporting Lisbon, huku Winga Nani akielekea upande wa pili kwa mkopo.
- Mlinzi Rio Ferdinand (35) amehamia QPR kwa mkataba wa mwaka 1.
- Beki kinda Luke Shaw (19) ametua ManUtd kwa dau la £27m, kwa mkataba wa miaka 5 na mshahara wa £100,000 kwa wiki. Luke Shaw anakuwa kinda ghali zaidi ndani ya EPL.
- Kiungo wa Athelic Bilbao Ander Herrera (25) ametua ManUtd kwa dau la £29m kwa mkataba wa miaka 5.

ARSENAL

- Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti huenda akatua ARSENAL msimu ujao kuchukua nafasi ya Arsene Wenger ambaye anaviziwa na Monaco ya Ufaranza kwa dau NENE.
- Mshambuliaji Danny Welbeck (23) ametua Arsenal kwa dau la £16m.
- Beki wa Arsenal Thomas Vermaelen (28) ametua Barcelona kwa dau la £15m.
- Beki kinda wa kulia Carl Jenkinson (22) amekwenda Westaham kwa mkopo.
- Beki kinda wa Southampton Calum Chambers (19, England) ametua Arsenal kwa dau la £16m.
- Golikipa wa Nice ya Ufaransa David Ospina (25, Colombia) ametua Arsenal kwa kitita cha £3.2m.
- Beki wa kulia wa Newcastle Mathieu Debuchy (28) ametua Arsenal kwa mkataba ambao haujawekwa wazi.
- Mshambuliaji wa Barca Alexis Sanchez (25) ametua Arsenal kwa kitita cha £35m.
- Golikipa Lukasz Fabianski (29) amehamia Swansea kama mchezaji huru.

CHELSEA
- Hatimaye mshambuliaji Loic Remy (17, France) ametua Chelsea kwa dau la £10.5m na mkataba wa miaka 4.
- Mkongwe Samuel Eto'o (33) amehamia Everton akiwa mchezaji huru.
- Kinda Romelu Lukaku (21, Belgium) amehamia Everton kwa dau la £28m kwa mkataba was miaka 5.
- Mkongwe Didier Drogba (36) ametua darajani kwa mkataba wa mwaka 1.
- Mshambuliaji Demba Ba (29) amehamia Besiktas kwa kitita cha £8m.
- Beki wa kushoto Filipe Luis (28, Brazil) ametua darajani kutoka Atletico Madrid kwa kitita cha £16m.
- Mshambuliaji anayetisha duniani kwa sasa Diego Costa (25) ametua Chelsea kwa dau la £32m.
- Kiung) ao mshambuliaji Cesc Fabregas (27) ametua Chelsea kwa dau la £30m, kwa mkataba wa miaka 5! Atavaa jezi namba 4.
- Beki anayepanda David Luiz (27) ametua PSG kwa kitita cha £40m, kwa mkataba wa miaka 5.
- Mkongwe Frank Lampard (35) amehamia New York City ya MLS, USA. Atachezea ManCity kwa miezi 6 kwa mkopo akisubiri MLS.

LIVERPOOL
- Mario Balotelli (24) ametua Liverpool kwa dau la £16m na mshahara wa £110,000 kwa wiki. Atavaa jezi namba 45.
- Kipa Victor Valdes (32) amekamilisha usajili wa kuhamia Liverpool. atatua Anfield mwezi Novemba.
- Beki wa kushoto Alberto Moreno (22, Spain) wa Sevilla ametua Liverpool kwa dau la £12m.
- Mshambuliaji kinda
Divock Origi (19, Belgium) amehamia Liverpool kwa dau la £10m. Lakini atabaki Lille kwa mkopo.
- Beki 'mkoba' Dejan Lovren (25, Croatia) wa Southampton ametua Liverpool kwa dau la £20m. Ujio wa Lovren umemwondoa Daniel Agger (29) ambaye amerudi kwao Denmark kujiunga na timu yake ya zamani Brondby.
- Winga kinda Lazar Markovic (20) ametua Liverpool kwa dau la £20m kutoka Benfica.
- Luis Suarez amehamia Barcelona kwa tita la £75m, mkataba wa miaka 5.
- Kiungo Adam Lallana (26) amehamia Liverpool kwa mkataba wa miaka 5 kwa dau la £25m na mshahara wa £100,000 kwa wiki.
- Mshambuliaji wa England Rickie Lambert (32) ametua Liverpool kwa mkataba wa miaka 2 kwa dau la £4m.

MANCITY
- Beki Micah Richards (26) ametua Fiorentina kwa mkopo kwa dau la £3.5m.
- Mshambuliaji Alvaro Negredo (29) ametua Valencia kwa mkopo.
- Mkoba kisiki wa Porto Eliaquim Mangala (23) ametua ManCity kwa dau la £32m.
- Kiungo mkongwe Frank Lampard (35) ametua ManCity kwa mkopo wa miezi 6 ili kujikeep fit akisubiri msimu wa MLS.
- Full Beki JEMBE Bacary Sagna (31) amesaini mkataba wa miaka 3. Atalipwa £140,000 kwa wiki.
- ManCity wametega dau la £53m kumng'oa kiungo kinda anayetisha duniani Paul Pogba (21) kutoka Juventus.

ULAYA
- Kiungo wa Real Madrid Xabi Alonso (32) ametua Bayern Munich kwa dau la £5m.
- Kiungo Alex Song (29) ametua Westham kwa mkopo kutoka Barcelona.
 
Adnaj Januzaj (19) anawindwa na PSG kwa ahadi ya mshahara mnono.
 
Real Madrid wametenga kitita cha £70m ili kumng'oa Luis Suarez (27) kutoka Liverpool.
 
Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani (27) anayechezea PSG amesema anatamani kutua Old Trafford msimu ujao. hii ni kutokana na kutoiva na kocha wake Laurent Blanc.
 
Karim Benzema (26) anawindwa na timu kibao za EPL, bei yake sokoni ni £40m. Chelsea, Arsenal, ManUtd wamo kwenye list.
 
Wayne Rooney (28) ameuomba uongozi wa ManUtd kuachana na kocha Van Gaal sababu ya ufundishaji wake 'mgumu'.
Van Gaal amesema kama atatua ManUtd atamchagua Van Persie kuwa captain wa timu (badala ya Rooney).
 
Wayne Rooney (28) ameuomba uongozi wa ManUtd kuachana na kocha Van Gaal sababu ya ufundishaji wake 'mgumu'.
Van Gaal amesema kama atatua ManUtd atamchagua Van Persie kuwa captain wa timu (badala ya Rooney).

Rooney ndo mwenye timu. Tusubiri kuona jinsi Rooney atakavyoanza kununa kama mtoto aliyenyimwa andazi.
 
Chelsea wanajipanga kumchukua mshambuliaji Diego Costa (25) kwa dau la £32m ambalo ni kianzio cha ada ya uhamisho kwenye mkataba wake.
 
Manchester City wametega dau la £53m kumng'oa kiungo kinda anayetisha duniani Paul
Pogba (21) kutoka Juventus.
 
mshambuliaji Hatem Ben Arfa wa Newcastle huenda akatua Liverpool kwa dau la £6m.
 
Frankie Domayo ametua Azam fc kwa dau ambalo halijawekwa wazi,!

Azam fc wanamnyemelea kwa ukaribu mkongoman wa ndala fc Mbuyu Twite kwa ada ya tsh 2000/=
 
PSG wametayarisha dau la £35m kwa ajili ya kumng'oa Wayne Rooney (28) kutoka ManUtd. Rooney ameonesha kutofurahia ujio wa kocha Van Gaal.
 
Kocha David Moyes huenda akatua Newcastle msimu ujao, endapo Alan Pardew atafukuzwa.
 
Kocha Arsene Wenger anajipanga kutumia £40m kuimarisha kikosi cha the Gunners kwa kuwasajili beki wa ManCity Micah Richards (25) na mshambuliaji aliyefanya kweli msimu huu Wilfried Bony (25) wa Swansea.
 
Bei ya MKALI Lionel Messi (26) sasa ni £164m kwa mujibu wa dau lililotengwa na Mancity ili kumng'oa Barcelona.
 
Barcelona imekamilisha uhamisho wa beki/kiungo mkabaji wa Chelsea David Luiz kwa mkataba wa miaka 5.
 
Beki na kepteni wa ManUtd Nemanja Vidic (32) atahamia InterMilan msimu ujao kwa uhamisho huru.
 

Naomba chanzo cha hii habari ya David Luiz
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…