Trafiki wa ubungo mataa

Siku hizi nikiwa na safari za kupita ubungo ni bora nikodi bodaboda
 
Mkuu keypad ya kichina nisamehe bure Ila utakuwa umenisoma
Nimekusoma mkuu ila hukanitendea haki kuniambia hata ukinielewesha sitaelewa...ni kweli naweza kuwa kilaza ila ungeniambia tu huende ningeelewa!kwa ufahamu wangu kuna peak hours za magari kwa njia fulani fulani hivyo trafiki wakiingilia huwa ni kwa sababu wanajua kuna njia zina magari mengi muda fulani hivyo kuyapa kipaumbele. Kama zikiachiwa taa hakika hazitajua kama kuna barabara zinahitaji kupewa kipaumbele!
 
japo mwanza nmji mdogo ila taa zilizo wekwaa naoma.kama.ziko kisasa zaidi maana wanaziongezea mda wa kuruhusu upande unao.kuwa na magari mengi
 
Happy palihitaji taa tu ziongoze maana trafiki ubu go amekuwa no kero Sana anaruhusu magari yanayotoka manzese tu na Kimara ukitoke Riverside imekuka kwako. Hatuelewi kwanini taa zisiachwe zijiongoze zenyewe. Hi imekuwa kero kubwa
 
Yaa hii ndio sababu halisi ya kuwepi askari kwenye mataa
 
Mmnafanya nn barabarani wakati taa zinafanya kazi? Kwa 100% foleni mnasababisha nyie..
Huku kwetu Chato.mbona tunapeta tu kwenye mataa hakuna cha askar wala nini muda mwingine unafika kwenye mataa uko peke yako hakuna gari hata moja unakatisha tu hata kama taa hazijaruhusu...
 
Mi nashangaaga why trafiki wasipokuwepo kwenye mataa ....ni no foleni kabisa!

Kumbe watu wanaweza jiongoza wenyewe tu bila wao!
 
Kuna Trafiki yupo maeneo ya Jangwani ile njia ya nyuma ya ofisi za Mabasi ya Mwendokasi ipo siku yako utatrend kwenye social networks!!.
Anapenda chapaaa?
 
Mara chache lakini mkuu!
 
Siku hizi kupita Ubungo tokea External imekuwa issue sana....inabidi wahusika waangalie namna ya kutatua tatizo hilo.
Hivi pale pana nini?[emoji15]

Wiki iliyopita niligandishwa 2 hrs na nilikuwa navuka tu hapo naingia makaburini nitokezee sinza! Jamani nilijuuta!
 
Kweli aisee huku kwetu traffic anaruhusu magari kwa kuangalia uzuri wa gari ,Mfano kama ktk foleni gari lililo tangulia ni vits daah mutachelewa kutoka ila kama kuna v8 imetangulia mapema tuu hata sec 10 hamkai.Pkpk ndo usiseme ,mutachoma mahindi
Haaahaaaa[emoji23] [emoji23]

Hiyo iko hata ktk kusimamishwa na trafiki anaangalia gari na gari....
 
Mimi nauliza ka swali wote tunaolalamika tuna magari au ata kwenye daladala tunalalamika??

Nijue tu basi usiniulize kwanini nataka kujua.
 
japo mwanza nmji mdogo ila taa zilizo wekwaa naoma.kama.ziko kisasa zaidi maana wanaziongezea mda wa kuruhusu upande unao.kuwa na magari mengi
Kwa Mwanza,bado hali ya magari ni manageable, taa ni rahisi kujiongoza. Hata kwa hapa Dar maeneo ambayo hayana msongamano wa magari taa zinafanya vizuri tu. Mfano ni Sokota na Chang'ombe- Serengeti!
Na kwa sasa,eneo la Ubungo hasa ukitokea upande wa Buguruni hali ni tete,na kwa maoni yangu,imesababishwa na mambo yafuatayo:-
1. Ujenzi mpya wa Barabara za juu pale Ubungo Junction(Ita ni Flyover,Grade interchange,Underpass/Overpass au vyovyote)
2. Kwisha kwa foleni pale Tazara ambapo magari makubwa ya Mizigo yanavuka TAZARA bila kuchukua muda mrefu na kujikuta yamewahi kufika Ubungo na hivyo magari kuelemea upande mmoja.
3. By Default,Ubungo Junction ndiyo hasa makutano makubwa ya Magari kutoka Mikoa mbalimbali Tanzania yanapoingia Dar kwa Mara ya kwanza na hivyo pana mkusanyiko mkubwa wa Magari tuseme kuliko popote Tanzania na kwa Dar Es Salaam ni Main Entrance Gate to and fro upcountry.
 
Happy palihitaji taa tu ziongoze maana trafiki ubu go amekuwa no kero Sana anaruhusu magari yanayotoka manzese tu na Kimara ukitoke Riverside imekuka kwako. Hatuelewi kwanini taa zisiachwe zijiongoze zenyewe. Hi imekuwa kero kubwa
Hiyo route ndo maana siipendi...ukiongezea na machokoraa wa kuiba side mirror ndo kabisa sithubutu!
 
Kweli aisee huku kwetu traffic anaruhusu magari kwa kuangalia uzuri wa gari ,Mfano kama ktk foleni gari lililo tangulia ni vits daah mutachelewa kutoka ila kama kuna v8 imetangulia mapema tuu hata sec 10 hamkai.Pkpk ndo usiseme ,mutachoma mahindi
oops
 
Mimi nauliza ka swali wote tunaolalamika tuna magari au ata kwenye daladala tunalalamika??

Nijue tu basi usiniulize kwanini nataka kujua.
Hata daladala mkuu nayo gari
 
Kusema ukweli trafik wanatakiwa wawe wanawapa nafasi Watu wote pasipo upendeleo Kwa mzunguuko ulio Sawa !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…