Trafiki Morocco jirekebisheni, mnakamata watu kwa kuwabambikizia makosa

Mulama

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
3,018
1,791
Jamani Trafiki ebu tuoneeni huruma jamani doh mtatufirisi kama mkiendelea hivi, mnakaa kwenye mataa hasa pale Morocco mnakamata gari za watu kwa kuwabambikia makosa ya kupita taa nyekundu, na mtu asipowapa ya kubrashi viatu mnatwanga ya kwenye hiyo mashine zenu?

Mafuta yameshapanda jamani inatosha mtuache tuchangie sirikali kupitia huko.

Nawasilisha kama mtasoma mkaelewa jirekebisheni kwakweli.
 
Traffic wengi wao sio waaminifu, wanabambikia sana watu makosa, unaweza kuwakuta wawili wakakusimamisha afu wanakwambia umeovertake kwenye straight line (Japo hujaovertake hata gari moja) ukigoma kuwapa ya kubrashia viatu wanakwambia twende kituoni, ukifika kituoni mmoja anajidai ndo aliyekukamata na yule mwingine shahidi, mkuu wa kituo anamwambia yule mwingine athibitishe, akisema ndio (HAPO NI LAZIMA ASEME NDIO) yule mkuu anatumia kama judgement kwa sababu tu hao traffic walikula kiapo cha utii kwa hiyo wanakulazimisha ulipe fine, ukigoma unaambiwa upelekwe mahakamani ambao ni usumbufu mwingine usiouhitaji.
Hii imenitokea juzi tu, niliwambia wanipeleke mahakamani wakaniweka kituoni hadi jioni wakaamua kuniachia.
 
Wengine wapo kwenye Toyota corola Nyeupe mwanzo mwa barabara ya Morogoro Road(bandarini), wanakaa wanne. Kama ni kutoa ada ya kiwi na brashi basi ni kwa wote wanne.

Weninge wpo daraja jipya la kigamboni, wanajificha kwenye zile nguzo.Wanaangalia spidi yako. Huna kosa la spidi au vibali, utasimamishwa kwa muda mrefu ili ujenge mazingira ya kununua haki zako.

Sasa yote tisa ni Tazara!!! naomba nisiseme
 
  • Thanks
Reactions: 4wd
Hivi teknolojia hii ya sim ni kwa kutizama porn tu au?
Kwanini usiwakamitishe,maana sim ina Camera,au funga Car mini Camera ambapo ukibambikiwa na wewe unawabambikia.
Tatizo ukiwa una Driver nyumba ya Driver kichaa basi akitoka tu na wewe unaibia eti zile seconds za taa unachomoka,hapo ndio janga sasa.
Mie siwezi kuisahau JF,maana nimefanikia kimaisha kwa kadri mungu alivyonijaalia kupitia humu kwa maoni ya watu na kupeana moyo kwa wana Jf.Maana mpaka sasa kuna zaidi ya miradi 32 ambayo nimeitoa hum na bado sijaifanya kazi nasuburia muda na kuzichanga,ila mpaka sasa nimesimama na miradi 5.
Mungu awabariki walioanzisha Jf na atubariki Members woote na atusamehe pale tunapozinguana
 
Jamani Trafiki ebu tuoneeni huruma jamani doh mtatufirisi kama mkiendelea hivi, mnakaa kwenye mataa hasa pale Morocco mnakamata gari za watu kwa kuwabambikia makosa ya kupita taa nyekundu, na mtu asipowapa ya kubrashi viatu mnatwanga ya kwenye hiyo mashine zenu?

Mafuta yameshapanda jamani inatosha mtuache tuchangie sirikali kupitia huko.

Nawasilisha kama mtasoma mkaelewa jirekebisheni kwakweli.
Acha malalamiko, fuata sheria, msomi kama ww nani akusaidie kusikitika? Shame!
 
Wengine wapo kwenye Toyota corola Nyeupe mwanzo mwa barabara ya Morogoro Road(bandarini), wanakaa wanne. Kama ni kutoa ada ya kiwi na brashi basi ni kwa wote wanne.

Weninge wpo daraja jipya la kigamboni, wanajificha kwenye zile nguzo.Wanaangalia spidi yako. Huna kosa la spidi au vibali, utasimamishwa kwa muda mrefu ili ujenge mazingira ya kununua haki zako.

Sasa yote tisa ni Tazara!!! naomba nisiseme
Na wengine wanasema eti zile mashine sijui efd walizopewa hazitakiwi kulala njaa! Au ya kiwi au ya mashine.
 
Back
Top Bottom