Trafiki mkoa wa Pwani tendeni haki

mwanamapinduko

Senior Member
Jan 24, 2011
178
41
Leo nilikuwa natoka Dar nakuja huku Morogoro, nilipofika Kiluvya kuna sehemu trafiki wanaka sana, zamani ilikuwa ni shamba ya Dr. Hashim, nikasimamishwa na trafiki kwamba nimetembea spidi ya 71. Nikamuuliza anionyeshe akanimbia kuna mwenzao kajificha kwenye mtelemko ndio anatumia taarifa. Nikamwambia aje huyo anionyeshe hiyo camera nikalazimishwa tu, kulipa faini na kunyang'anywa leseni yangu. Haki iko wapi hapa?

Nilipolipa sikupewa risiti, nakaambiwa risiti inatolewa kituoni tu.
Je ni halali kulipa faini faini kwa fedha taslim bila kupewa risiti ya GRR.
Hili ni jipu, huenda ni mradi wa vigogo fulani.
 
pwani inaanzia pale kwenye daraja kabla hujafika kibaha mizani pili hukutakiwa kuzidisha mwendo kasi tatu kuna namba za malalamiko zinatangazwa kila siku na za ma rto kwa kweli hawaonei mtu kwa msaada zaidi jiunge na kundi la facebook linaitwa road safety ambassador RSA hili kundi lina viongozi wengi waandamizi wa kikosi cha usalama barabarani akiwemo Kamanda Mpinga ukipata tatizo unatuma picha za ushahidi na tatizo lako linashughulikiwa.
 
Pole ila kwanza kabisa kiluvya sio pwani pwani inaanzia pale kwenye daraja kabla hujafika kibaha mizani pili hukutakiwa kuzidisha mwendo kasi tatu kuna namba za malalamiko zinatangazwa kila siku na za ma rto kwa kweli hawaonei mtu kwa msaada zaidi jiunge na kundi la facebook linaitwa road safety ambassador RSA hili kundi lina viongozi wengi waandamizi wa kikosi cha usalama barabarani akiwemo Kamanda Mpinga ukipata tatizo unatuma picha za ushahidi na tatizo lako linashughulikiwa.
Hapo ni pwani labda kama haujui nini unaongea. Kiluvya ni wilaya ya kisarawe jipange.
Kazi ya usalama barabarani haifanywi kwa kujificha. Na mhusika akikosea ni haki aonyeshwe ushaihidi wa kosa. Na akilipa faini lazima apewe risiti halali ya serikali.
Illegal immigrant uliza mpaka wa mkoa wa pwani sio unakurupuka tu
 
Kumradhi kweli kiluvya ni kibaha sasa kwa nini uli over speed mkuu?
 
Hapo ni pwani labda kama haujui nini unaongea. Kiluvya ni wilaya ya kisarawe jipange.
Kazi ya usalama barabarani haifanywi kwa kujificha. Na mhusika akikosea ni haki aonyeshwe ushaihidi wa kosa. Na akilipa faini lazima apewe risiti halali ya serikali.
Illegal immigrant uliza mpaka wa mkoa wa pwani sio unakurupuka tu
Sasa ni kwa nini ukitoka maili moja Kibaha kibao cha karibu wilaya ya Ubungo kipo pale darajani kwenye mpaka wa Kiluvya na Kibaha?

Naomba ufafanuzi.
 
Kweli traffic wanamapungufu yao lakini nawaza kwanini ulikubali kulipa bila kuonyeshwa "tochi" siku nyingine piga namba hii 0682887722 ila hakikisha kweli hujafaanya kosa, kwenye spidi ni ngumu sana kumuonea mtu....pole jua haki zako usigombane nao waombe wakuelekeze
 
Leo nilikuwa natoka Dar nakuja huku Morogoro, nilipofika Kiluvya kuna sehemu trafiki wanaka sana, zamani ilikuwa ni shamba ya Dr. Hashim, nikasimamishwa na trafiki kwamba nimetembea spidi ya 71. Nikamuuliza anionyeshe akanimbia kuna mwenzao kajificha kwenye mtelemko ndio anatumia taarifa. Nikamwambia aje huyo anionyeshe hiyo camera nikalazimishwa tu, kulipa faini na kunyang'anywa leseni yangu. Haki iko wapi hapa?

Nilipolipa sikupewa risiti, nakaambiwa risiti inatolewa kituoni tu.
Je ni halali kulipa faini faini kwa fedha taslim bila kupewa risiti ya GRR.
Hili ni jipu, huenda ni mradi wa vigogo fulani.
Siku ya kurudi soma vizuri vibao vya speed, kwenye 50 tembea chini ya 50 na usiovertake kwenye miinuko ukiona mule imechorwa mistari miwili myeupe hata ya njano.

Hiyo njia traffic wanahamahama hujui watakubambia wapi, anayekupiga tochi siyo anayekusimamisha anarushiwa tu picha na speed yako.

Siku nyingine unaposafiri mikoani na gari punguza uchoyo ukisimamishwa wape 5000 yao ya shoeshine wala hutopata kero na utazoeana nao tu.

Sisi wenzako wenyeji wa hiyo njia tukipungukiwa hela huwa tunachukuwa pesa kwa haohao traffic.
 
Ok hiyo 5000 ni rushwa?
Hapana siwezi kutoa hiyo, kama nitakosea nitawajibika.
 
Siku ya kurudi soma vizuri vibao vya speed, kwenye 50 tembea chini ya 50 na usiovertake kwenye miinuko ukiona mule imechorwa mistari miwili myeupe hata ya njano.

Hiyo njia traffic wanahamahama hujui watakubambia wapi, anayekupiga tochi siyo anayekusimamisha anarushiwa tu picha na speed yako.

Siku nyingine unaposafiri mikoani na gari punguza uchoyo ukisimamishwa wape 5000 yao ya shoeshine wala hutopata kero na utazoeana nao tu.

Sisi wenzako wenyeji wa hiyo njia tukipungukiwa hela huwa tunachukuwa pesa kwa haohao traffic.
Tehe tehe...inachukua hela kwa traffic?
 
Back
Top Bottom