white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,618
- 13,891
Jana nimekwenda ofisi ya TRA, kwa ajili ya kukata TIN, nafika nakutana na mkadiliaji kodi, ana kadilia kodi ninayotakiwa kuilipa, nakubaliana nayo tena kwa kuvutana kweli, Ngoma ikaja anataka mkataba wa pango, nikampa anasema kuwa eti hiyo kodi ya pango ambayo kwa mwaka na 1.2 milioni, natakiwa nilipe asilimia 10!!!! Ambayo ni 120,000!! Nikamwambia mi hiyo pesa nimemlipa mwenye nyumba na yeye ndio anatakiwa kulipa kodi kwenye pesa hiyo sio mimi tena nimlipie?? Anasema eti kwa wenye nyumba imekuwa ngumu kulipa kodi hiyo, hivyo mi ndio nilipe kisha nikamwambie mwenye nyumba anirudishie!! Jamani huu si uhuni, serikali inaogopa kukusanya kodi hiyo toka kwake mi ndio niwakusanyie?? Tumebishana sana nikaona ngoja niondoke zangu kwani naweza leta balaa jingine tena nikampa sifa MGONJA!!! Kweli hii nchi ni shidaaa!!! Wanashindwa kukusanya kodi huko IPTL, Sisi ndio watukamue, haya mambo ndio yanasababisha mtu akwepe kulipa kodi kabisa !!! Hata hicho kidogo kinakosekana kabisa!! Kwani hii sheria imekaaje na mbona huko nyuma haikuwepo??? Yaani mapato amepata mwenye nyumba kodi nilipe mimi jamani!!!! Kisa wenye nyumba huwa hawakubali wanapofuatwa na mamlaka ya kodi!!!
kakuona zuzu.....
Ndio utatatibu wanaotumia mkuu, no way you can escape that.
anashindwa kumdanganya kua hiyo sehemu hakupanga!
kakuona zuzu.....
mkuu, sio kwamba kamuona zuzu. hiyo kodi inaitwa stamp duty. ni kodi ambayo wananchi wengi hawana uelewa nayo. ni 1% ya monthly rental price.
Ndio utatatibu wanaotumia mkuu, no way you can escape that.
Mkuu hivi ni 10% au 1% kwani kuna mfanyakazi wa tra nimemuuliza kuhusu kiwango hicho akasema ni asilimia 1, ya stamp duty na sio asilimia kumi, asilimia kumi ni withholding tax?? Sasa kipi sahihi?? Hata kama ni asilimia moja, sitakiwi kulipa mimi.
Jana nimekwenda ofisi ya TRA, kwa ajili ya kukata TIN, nafika nakutana na mkadiliaji kodi, ana kadiria kodi ninayotakiwa kuilipa, nakubaliana nayo tena kwa kuvutana kweli, Ngoma ikaja anataka mkataba wa pango, nikampa anasema kuwa eti hiyo kodi ya pango ambayo kwa mwaka ni 1.2 milioni, natakiwa nilipe asilimia 10!!!! Ambayo ni 120,000!! Nikamwambia mimi hiyo pesa nimemlipa mwenye nyumba na yeye ndio anatakiwa kulipa kodi kwenye pesa hiyo sio mimi tena nimlipie?? Anasema eti kwa wenye nyumba imekuwa ngumu kulipa kodi hiyo, hivyo mi ndio nilipe kisha nikamwambie mwenye nyumba anirudishie!! Jamani huu si uhuni, serikali inaogopa kukusanya kodi hiyo toka kwake mi ndio niwakusanyie?? Tumebishana sana nikaona ngoja niondoke zangu kwani naweza leta balaa jingine tena nikampa sifa MGONJA!!! Kweli hii nchi ni shidaaa!!! Wanashindwa kukusanya kodi huko IPTL, Sisi ndio watukamue, haya mambo ndio yanasababisha mtu akwepe kulipa kodi kabisa !!! Hata hicho kidogo kinakosekana kabisa!! Kwani hii sheria imekaaje na mbona huko nyuma haikuwepo??? Yaani mapato amepata mwenye nyumba kodi nilipe mimi jamani!!!! Kisa wenye nyumba huwa hawakubali wanapofuatwa na mamlaka ya kodi!!!
MkuU KaSome sHerIa kwaNza ndo Uje haPa kUlaLaMika. maLipo Ya pango yanaYozidi shilingi 500,000 hupigwa kodi kwa asilimia kumi na ukusanyaji wake huwa katika mfumo wa withholding. Sheria ya kodi ya mapato inasema wewe mpangaji ndo utakuwa withholding agent wa mpangishaji waKo iki mAaniSha kwaMba UnaTaKiwa kUkAta Asilimia KuMi ya MaLipo kAbla uJamlipa MpaNgisHaji waKo nA kuPeleKa T.R.A as witholding tax. Hapo afisa wa T.R.A yuko sahihi sema ni wewe kama taxpayer unatakiwa uwe na elimu ya kodi au tafuta consultant awe anasimamia mambo yako yote yahusiaNaYo nA koDi.
Hapo ni sawa,
kodi za majengo zinaangukia katika kipengele cha "Withholding Tax". Hii ni aina ya kodi ambayo hukatwa from "the source". Kwenye fungu hili hata kodi kutokana na mishahara-PAYE zinaangukia humu.
Yaani mlipa hela (Mpangaji au Mwajiri) anamkata kabisa kodi mlipwa hela (Mwenyenyumba au Mfanyakazi) na kuipeleka TRA.
Ukitaka wewe ulipe rent kisha Mwenyenyumba ndio akalipe kodi, vipi waajiri nao wakitaka wawalipe mishahara mizima mizima wafanyakazi wao kisha wao wafanyakazi ndio wakalipe kodi wenyewe?