Tra,hili halikubalik!!!!

Tra,hili halikubalik!!!!

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,114
Reaction score
5,114
Nipo Morogoro na nimebahatika kuangalia Abood TV asubuhi na kukutana na kituko hiki.
TRA wanakusanya kodi kwa waendesha bodaboda na kijana mmoja aliyekuwa akiwakimbia alifukuzwa na gari la TRA na kutumbukizwa mtaroni kisha gari lile likakimbia.
Mku wa TRA anaeleza kuwa watu watii sheria za nchi akijitahidi kutetea kitendo hicho.
Je TRA wanruhusiwa kufanya haya?
Nimeliweka jambo katika siasa kwani juzi tu hapa Masasi kulichafuka na kuitia serikali hasara kwa upuuzi wa trafiki mmoja aitwae Komba.
TRA tafuteni njoa mbadala za kuwabana bodaboda kuliko kufukuzana nao barabarani,nchi ina watu ambao wamekata tamaa na wanaweza wakatutia katika doa kwa jambo dogo.
 
nakuunga mkono ndugu yangu nami boda boda langu limekutana na kadhia hiyo hapo moro
 
1. Nyie wamiliki wa bodaboda mmewafundisha madereva wenu maadili ya kuendesha hizo pikipiki barabarani, huo ni ujinga wa dereva wako kujichukulia sheria mkononi, si angesimama na kupewa maelekezo.
2. Mnajua hizo kadhia wanazosababisha pindi ikitokea ajali hata kama wanamakosa.ni vifo vingapi wamesababisha pindi wakumbwapo na ajali. acha kusahabikia ujinga wa madereva wa bodaboda!
 
wewe sasa upo nje ya mada, TRA wanatakiwa wchukue polisi ili dereva akikimbia polisi ndo anafatilia na sio TRA, mbona TRAmigodini hawaendi kuchukua MABILIONI yetu yatokanayo na biashara ya rasilimali zetu, badala yake wanafukuzia elfu hamsini.
 
is TRA a law enforcer organisation??......tukijibu hili swali, tutajua kama TRA wana haki ya kufanya hivyo!!!!!
 
nakuunga mkono ndugu yangu nami boda boda langu limekutana na kadhia hiyo hapo moro Kwa hiyo wewe ulitaka TRA wamkimbie huyo mwendesha bodaboda wasitekeleze majukumu yao mara baada ya kutimua mbio?.Acha ushahabiki shauri watu wafuate sheria za nchi.
 
1. Nyie wamiliki wa bodaboda mmewafundisha madereva wenu maadili ya kuendesha hizo pikipiki barabarani, huo ni ujinga wa dereva wako kujichukulia sheria mkononi, si angesimama na kupewa maelekezo.
2. Mnajua hizo kadhia wanazosababisha pindi ikitokea ajali hata kama wanamakosa.ni vifo vingapi wamesababisha pindi wakumbwapo na ajali. acha kusahabikia ujinga wa madereva wa bodaboda!
Umekuwa nje ya maada lakini si kitu ngoja tujaribu tena.Suala kubwa ni kuwa TRA wan haki ya kumgonga mtu kwa kuwa kawakimbia?
Jambo la pili ni kuwa TRA hawawezi kubuni nia ya kupata kodi bila kufukuzana barabarani?Tumeona fire extinguisher sasa inakatwa wakati unakata road licence.
 
siungani nawe, sheria ziko wazi..kama kila mtu atakimbia hao tra wataitoa wapi hiyo kodi, tatizo hapa si madereva tu bali hata wamiliki..tutii sheria
 
TRA wana kitengo cha Enforcement and Compliance kwa watu makaidi kama hao wa bodaboda kwani wakati anakimbia hakujua kama atapata ajali? kama angekuwa hana kosa alikuwa anakimbia nini?
 
Bado nayakumbuka sana maneno ya baba wa Taifa!!:nanukuu!(Nchi corrupt hazikusanyi kodi,zinabaki kufukuzana na vitu vidogo mabarabani basi)mwisho wa kunukuu!!
Sina hakika sana kama wafanya biashara wakubwa wanaweza kufanyiwa kitu kama hicho!!
Lakini cha msingi hapa ninachoshauri ni kwamba,si vizuri tunapowaona waliopewa dhamana ya kukusanya kodi
kuwakimbia!!dawa ni kulipa ili kufanya biashara kwa uhuru,na kwa uhakika!!
Ni ushauri tu!!
 
TRA wana kitengo cha Enforcement and Compliance kwa watu makaidi kama hao wa bodaboda kwani wakati anakimbia hakujua kama atapata ajali? kama angekuwa hana kosa alikuwa anakimbia nini?
hapo kwenye red mkuu! hiyo idara kwa mujibu ya tra act ya mwaka 1996 iliyoanzisha mamlaka! inatakiwa ifanywe na customs department! ila kwa uroho wa tra watu wa domestic revenue mbao ndio tupo nao wengi huku wilayani! wanawatishia mpaka bastola wafanyabiashara iliwatoe kodi!
kwa upeo wangu! doestic revenue ndio wanahusika na usajili na kodi za vyombo vya moto! sasa wamefanya hiyo ndio kama kazi ya ku deal na magari !ambapo utafiti uliofanywa na World Bank ilishauri hiyo idara wafanyakazi wapunguzwe! kasababu inachangia 18% ya pato la taifa na inawafanya kazi zaidi ya 1900,wakati idara mbili zingine za TRA zilikusanya 82% na zina wafanyakazi 400 tu
 
siungani nawe, sheria ziko wazi..kama kila mtu atakimbia hao tra wataitoa wapi hiyo kodi, tatizo hapa si madereva tu bali hata wamiliki..tutii sheria
Sidhani kama uko Tanzania hii inayoelezewa hapa ni kweli ziko wazi lakini suala ni nani anazisimamia ili zitende haki.Dunia kote raia wanalipa kodi kwa serikali zao kwa hiari pale tu wanapoona haki inatendeka.Haiwezekani watu na Makampuni yenye uwezo wa kulipa kodi wapewe Misamaha isiyoelezeka halafu Mamlaka za kukusanya kodi ziingie barabarani kufukuzana na waendesha Pikipiki.
Kwanza gharama za kukusanya kodi za aina hizo TRA anazirudishaje?.
 
Back
Top Bottom