Hahahah pengine bwana aspirin swala linalokukwaza ni neno mpya kama lilivyotumika. Lakini kuna concern moja tu katika ununuaj wa magari kwa hapa tanzania huwa tuna terminology za kugawa magari ktk makundi mawili kwa kuzingatia kuwa asilimia 95 ya magari yanayotembea hapa nchini yalinunuliwa katika masoko ya magari japan au dubai au uk au sehem zingine kama hizo yakiwa na hali ya kutumika huko. Na inapofika hapa likaanza kutumiwa na owner hapa tz mfano kwa mwaka na muda ukawa umesonga baso hilo kwa kibongo bongo tunaliita used na linapoingia na halijatumika hapa tanzania basi hilo tunaliita jipya kwa msingi si wa ziro km kutoka kiwandani bali ni kwa msingi wa kutumika hapa tanzania. Naamini wajua kuwa hata vits ambayo inauzwa 6m imported from japan basi ulipaswa kuinunua kwa dola 29000 kama ingekuwa ni straight from industry na ukawa the very first user after the technicians. Sasa basi kuhitimisha ningependa tafsiri ya mwaka 2002 izingatiwe kuwa ni mwaka wa gari kutengenezwa na kwa anayenunua magari ama aliyewah kununua magari analijua hili at first eye. Nawasilisha.