Wanajamvi,
Nipo mbioni kumiliki gari aina ya Toyota duet,ninaomba kwa wazoefu waliokwisha litumia gari hilo wanijuze ufanisi wake pamoja na mapungufu yake.
Nawakilisha.
Mdukuzi,Duh!Umeongea kwa madharau sana,kumbuka tunatofautiana kwa kipato.Heri yako unayetembelea gari za ma-officer.Uwezo wangu kwa sasa ni hapo (magari ya mahouse girl)
toyota carina,naishi kimara shida ya maji kila siku naweka madumu manne nikienda kazini nakuja na maji ya kuoga na kupikia ,ingekuwa hiyo duet si itakuwa majanga
kwa style hiyo nina uhakika una no za maduka ya spare za magari kama 20 hivi, lazma uwe mteja wao mkubwa wa kununua showcups :smile-big:
mh humu ndani unaweza usiombe msaada! hahahahhaa
Kuna jirani yangu mmoja hapa anayo tangu mwaka jana june gari inakua na miss mpaka AC hawezi kuwasha, na kashazunguka sana kwa mafundi kila wakipima diagnosis inasema plague, lakin akibadili plague mziki ni hule hule.......na watu wengi niliojaribu kuwauliza wanasema zile gari nzuri lakin ukishaanza kuigusa engine ujue itakuua na mawazo,
So far chukua kama ndio umeshailipia maana hata tukikwambia ni kimeo haitasaidia
gari ya mahouse gal kwendea markit ongeza kidogo tafuta corola hivi vigari visivyo na boot nyuma mimi huwa naona vimekaa kitoto au kihouse gal siwezi kuendesha bora nipande taxi
mkuu chukua tu hiyo gari mimi mwenyewe walinitisha sana wadau wa humu jf lakini ubishi wangu ulinifanya niagize na huu ni mwaka unaenda wa tatu, nilikuwa natumia chevrolet suv nilinunua ughaibuni nimetumia kama miezi sita hapa bongo kwa safari za mjini na nyumbani lakini nikaona nalifanyia kazi gari kwani lilikuwa linakula sana mafuta,nikaamua niwe nalitumia kwa safari za mbali sana na nikanunua Duet, niliifanyia modifications kama kuinyanyua juu pamoja na kuifunga sports tires na rims za size kumi na nne,uwezi amini nasafiria Tanga kila week ends na gari iko stabble barabarani hata ukipishana na roli haiyumbi na ulaji wake wa mafuta ni mzuri sana,km 14 hadi 20 kwa lita moja, cha muhimu ni service tu na spare zake zinapatikana sana siku hizi tofauti na zamani.
Wa Carina anaweza kumcheka wa Duet!