Toyota Duet

Msingida

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
10,567
Reaction score
12,206
Wanajamvi,
Nipo mbioni kumiliki gari aina ya Toyota duet,ninaomba kwa wazoefu waliokwisha litumia gari hilo wanijuze ufanisi wake pamoja na mapungufu yake.
Nawakilisha.
 
ni nzuri hasa kwa mafuta haili sana ila spare zake ghali kidogo.ila kwa ujumla ni nzuri inanisaidia kubana matumizi
 
ni nzuri hasa kwa mafuta haili sana ila spare zake ghali kidogo.ila kwa ujumla ni nzuri inanisaidia kubana matumizi

Na ikibadilisha mlio kwenye engine basi tupa ununue nyingine kwani hainaga fundi
 
Umenikumbushia toyota duet yangu niliyoiuza kutatua shida kubwa iliyonikabili. Niliipendea kwa ulaji mdogo wa mafuta na stability barabarani. Rafiki yangu aliyeinunua sijamsikia akilalamika.
Mshikaji wangu, kama wataka kumiliki hiyo gari endelea tu ila angalia shape yako isikaribie ya yule mzee wa mbamba bay!
 
Mimi nimetumia hizo Gari sana na hadi sasa natumia Duet toleo la zamani ambalo lilijulikana kama Daihatsu. Hii ni Gari ya tatu ya aina hio naitumia bila shaka. Inakimbia balaaa na ina stability ya kufa mtu. Fuel consumption Ndio usiseme. Inatembea hadi 14km/L. Hizi Ndio Gari nzuri unaweza kukimbia hadi 160km/hr na upishane na Malori wala isitikisike. Naongea from experience

Niliyonayo sasa hivi naiuza pia. Namba na CLS km 20,000
 
ni nzuri hasa kwa mafuta haili sana ila spare zake ghali kidogo.ila kwa ujumla ni nzuri inanisaidia kubana matumizi

Nitajitahidi kuifanyia service kwa wakati na sitakaa nayo sana.
Nashukuru kwa ushauri.
 
Nashukuru kwa ushauri,ningekuungisha lakini yangu nimeshailipia tayari.
 
Umenichekesha sana,ninaenda gym sidhani kama yule jamaa naweza mfikia.Nashukuru kwa ushauri.
 
gari ya mahouse gal kwendea markit ongeza kidogo tafuta corola hivi vigari visivyo na boot nyuma mimi huwa naona vimekaa kitoto au kihouse gal siwezi kuendesha bora nipande taxi
 
Duet inaboot kubwa sana na so spacious. Tatizo ninaloliona mie ni kelele za engine halaf take care wakati wa kufanya service filter imejificha fundi asipokuwa makin anaweza kupukutisha nyaya za ac kwenye compressor themn itakuwa majanga. Otherwise ni kweli spare zake ni ghali kidogo but now naona ziko nyingi bei itapungua.
Kuna wengine wamebadilisha rim size from 13 to 14 kweli inapendeza but kumbuka unapunguza stability halafu wear and tesr inaongeza so as fuel.
Ningekushauri tembelea kama ulivyoinunua from Japan....period
 
gari ya mahouse gal kwendea markit ongeza kidogo tafuta corola hivi vigari visivyo na boot nyuma mimi huwa naona vimekaa kitoto au kihouse gal siwezi kuendesha bora nipande taxi

heshima yako kwanza mkuu :A S 27::A S 103: hivi hapo sasa hivi unatumia gari gani vileee?
 
gari ya mahouse gal kwendea markit ongeza kidogo tafuta corola hivi vigari visivyo na boot nyuma mimi huwa naona vimekaa kitoto au kihouse gal siwezi kuendesha bora nipande taxi

Eti mtu anatafuta pesa hadi kufoji imprest ili kununua Duet! Kama pesa ya kununua gari zuri huna,bora upande Bodaboda
 
heshima yako kwanza mkuu :A S 27::A S 103: hivi hapo sasa hivi unatumia gari gani vileee?

toyota carina,naishi kimara shida ya maji kila siku naweka madumu manne nikienda kazini nakuja na maji ya kuoga na kupikia ,ingekuwa hiyo duet si itakuwa majanga
 
toyota carina,naishi kimara shida ya maji kila siku naweka madumu manne nikienda kazini nakuja na maji ya kuoga na kupikia ,ingekuwa hiyo duet si itakuwa majanga

Nina bomba linatoa maji saa 24,na tank ya maji ya akiba.Gari hii nafikiri kwa uwezo na mahitaji yangu naona inaweza kunifaa.
 
gari ya mahouse gal kwendea markit ongeza kidogo tafuta corola hivi vigari visivyo na boot nyuma mimi huwa naona vimekaa kitoto au kihouse gal siwezi kuendesha bora nipande taxi

Mdukuzi,Duh!Umeongea kwa madharau sana,kumbuka tunatofautiana kwa kipato.Heri yako unayetembelea gari za ma-officer.Uwezo wangu kwa sasa ni hapo (magari ya mahouse girl)
 
Eti mtu anatafuta pesa hadi kufoji imprest ili kununua Duet! Kama pesa ya kununua gari zuri huna,bora upande Bodaboda

Nashukuru kwa kashfa georgeallen,Mie mtoto wa mkulima na sitegemei imprest.Nimeuza bodaboda na nimeongezea kidogo nianzie hapo kwenye Duet.Ushauri wako siufanyii kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…