Top state officials own firms in sh133 billion theft

Mimi nasema tena kwamba JK hana uwezo wa kumshitaki mto yeyote.JK ni mnafiki na anahusika moja kwa moja na upotevu wa mapesa haya .
 
Jamani hapa JF siku zote naamini kuna vichwa,hivi kweli hamuwezi kuinama na mtakapoinuka muwape watanzania mbinu za namna ya kuhakikisha hawa mabaradhuli hawatelezi akiwamo JK mwenyewe.
Jamani msinifanye nikaamini humu hatuna mbinu.
 
Jaribu Rift valley style, ila tu tatizo la mafisadi hata kwenye vita huwa hawafi. Wana magate makubwa, walinzi wengi na vyote vikishindwa wanaweza hata kuwahonga wanaotaka kuwaua.

Naona njia salama ni ile ya kura tu hata kama na zenyewe wanaiba.
 

Hewalaaah maalim Mtanzania

Hiyo ndiyo shida, wamezoea kuiba kiasi cha kuona wizi ni sawa na kujikuna, sawa na aliyezoe kuwibia mkewe, anaanzia gesti eventually anapangisha nyumba, mwishoni anahamia kabisa nyumba ndogo. Siku akifumaniwa na bi mkubwa basi teena mzee mzima anaanza kutafuta wabaya wake.

Othman is a very intelligent guy, anajua nani bosi wake, na ni kijana wa mjini - he is a survivor. Apson alipompendekeza alidhani Othman atakuwa kibaraka wake hata ninasikia mzee wa watu analalama kuwa Othman hamweshimu etc. Wakati kijana wake alipogombea nafasi ya CC na NEC through CCM inasemekana alimwomba Othman awatumie vijana wa "system" kumsaidia. Inasemekana Othman kamtolea nje kiasi ambacho mzee kipara hana hamu hadi leo. Tena wakati wa mchakato wa mgombea urais toka CCM inasemekana alikuwa ameiweka system kumkandia JK. Mzee Upara akubali kuwa enzi zake basi tena,amevuta vya kutosha atulie na totos zake kama bado michuuzi ipo, ila akubali era yake imepita.

Kama kuna watu walioitumia CCM na at the same time kuimarisha ufisadi ni Mzee Kipara. Hayo yoote ya TISS kuonekana kwenye bank transactions, mambo ya Kagoda, Excellent Services etc yoote ni creation za huyo mzee. He was the Invincible. Ndiyo maana kwenye kesi hii ya BOT watakaofungwa = 0; na pesa zitakazorudishwa = 0.

Mbona Tony Blair baada ya kufanya uchunguzi kuhusu uuzwaji wa silaha Saudi Arabia na kugundua kuwa ufisadi/hongo ulitumika akasitisha uchunguzi kwa sababu za Usalama wa Taifa. Hapa kwetu Usalama wa Taifa = Usalama wa CCM.
 
Sina la ziada ktk hoja hii na ninamshukuru mwenyeji mungu kwa ajili ya wale watu wake wema hapa duniani.Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…