Tofauti ya Viongozi Vijana wa Mwl Nyerere na wale wa Rais Magufuli

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Amani iwe nanyi!
Leo nakuja kivingine, kivingine kabisaa. Ni kuhusu wavulana wa JPM. Viongozi vijana walikuwepo toka enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mifano ni mingi ila leo nitatoa michache.Awamu ya kwanza, Mwalimu alikuwa na vijana kwenye uongozi wake kama Salm Ahmed Salm,Edwawrd Lowassa, William Lukuvi na wengine wengi tu.

Awamu ya tano kila kona kumejaa viongozi vijana tena vijana kwelikweli.Tofauti ya vijana hawa wa JPM na Mwalimu ni kwamba hawa wamebaki kuwa wavulana na hawajui thamani ya nafasi walizo nazo. wanafurahi kuwa viongozi lakini hawajui majukumu yao. wengine wamelewa madaraka kupita kiasi, na wengine wanadhani wapo madarakani kupambana na Mbowe au CHADEMA.

Mkuu wa mkoa wa Arusha kuwepo kwake kule kumepunguza kwa kiasi kikubwa walio kuwa wanakipenda chama cha Mapinduzi.Kuna uwezekano mkubwa chama chake kisipate hata Diwani mmoja kwenye uchaguzi mkuu 2020. Kuna huyu wa jijini Dar, kifupi ni kwamba amechokwa na kila mtu na hivyo kusababisha chama chao kuchokwa pia.Kimsingi opposition wana nafasi ya hadi asilimia mia kutwaa jiji lote la Dar ifikapo 2020.

Baadhi ya wavulana hasa wakuu wa Wilaya na mikoa wamejifunza kitu kutokana na udhaifu wa wenzao, lakini inaonekana bado hawajajua njia sahihi ya kuchukua kwasababu mkubwa kabisa hatabiriki.Mawaziri wamemjua vilivyo mtu wanae msaidia kuwa hapendi msaidizi wake awe mashuhuri kuliko yeye, wanatekeleza majukumu yao kimyakimya.

Kama mikoa yote ingekuwa na viongozi aina ya Gambo au makonda, au huyu msemaji wao, basi 2020 uchaguzi utakamilika saa nne asubuhi. kujua kwingi...........
 
Nakuunga mkono. Yaani hao wavulana ni aibu tupu lakini sasa kama ndiyo malezi wanayopata toka kwa baba yao wafanyeje?
 
wanatakiwa wajiongeze! ni kama wametosheka kuwa na vijipesa walivyo navyo bila kuangalia safari ndefu iliyo mbele yao.
 
Mkuu utatekwa.
lakini ukweli lazima tuuseme. Salm Ahmed Salm alipata uongozi akiwa na umri wa miaka 22 tu lakini miaka yote alitumikia umma bila dharau na kujisikia kama wafanyavyo hawa wavulana wa milele.
 
Inapotokea Umri Ukau-overtake Akili, Muhusika Huongozwa Na Mihemuko Kuliko Fikra. Hapo Ndipo Uongozi Unapogeuka Kuwa Utawala.
 
Tatizo ninalo liona wengi baada ya kuteuliwa na kushika Madaraka hawapelekwi kwenye kozi maalumu za kuwajengea uwezo na kujitambua. kila mmoja anajiona ni Mungu mtu! Mtu unatumiaje rambirambi kwa shughuli isiyo husiana na msiba au kuwafariji wafiwa halafu nafsi isikusute?
 
Kama sio ushetani ni ushenzi wa karne pesa ya rambi rambi kufanyia miradi yao
 
Amani iwe nanyi!
Leo nakuja kivingine, kivingine kabisaa. Ni kuhusu wavulana wa JPM. Viongozi vijana walikuwepo toka enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mifano ni mingi ila leo nitatoa michache.Awamu ya kwanza, Mwalimu alikuwa na vijana kwenye uongozi wake kama Salm Ahmed Salm,Edwawrd Lowassa, William Lukuvi na wengine wengi tu.

Awamu ya tano kila kona kumejaa viongozi vijana tena vijana kwelikweli.Tofauti ya vijana hawa wa JPM na Mwalimu ni kwamba hawa wamebaki kuwa wavulana na hawajui thamani ya nafasi walizo nazo. wanafurahi kuwa viongozi lakini hawajui majukumu yao. wengine wamelewa madaraka kupita kiasi, na wengine wanadhani wapo madarakani kupambana na Mbowe au CHADEMA.

Mkuu wa mkoa wa Arusha kuwepo kwake kule kumepunguza kwa kiasi kikubwa walio kuwa wanakipenda chama cha Mapinduzi.Kuna uwezekano mkubwa chama chake kisipate hata Diwani mmoja kwenye uchaguzi mkuu 2020. Kuna huyu wa jijini Dar, kifupi ni kwamba amechokwa na kila mtu na hivyo kusababisha chama chao kuchokwa pia.Kimsingi opposition wana nafasi ya hadi asilimia mia kutwaa jiji lote la Dar ifikapo 2020.

Baadhi ya wavulana hasa wakuu wa Wilaya na mikoa wamejifunza kitu kutokana na udhaifu wa wenzao, lakini inaonekana bado hawajajua njia sahihi ya kuchukua kwasababu mkubwa kabisa hatabiriki.Mawaziri wamemjua vilivyo mtu wanae msaidia kuwa hapendi msaidizi wake awe mashuhuri kuliko yeye, wanatekeleza majukumu yao kimyakimya.

Kama mikoa yote ingekuwa na viongozi aina ya Gambo au makonda, au huyu msemaji wao, basi 2020 uchaguzi utakamilika saa nne asubuhi. kujua kwingi...........
Huwezi kulazimisha maoni yako yawe maoni ya wote
 
Back
Top Bottom