Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,913
Wewe ndio mwenyekiti wa kijiji ila kiumri inabidi baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji wakupe "shikamoo" kwanza ndio waanze mazungumzo ya kukushauri katika kikao chenu cha serikali ya kijiji.
Katika mazingira kama haya na kwa kuzingatia mila na desturi zetu,hali hili inaweza kuwa ni mojawapo ya chanzo cha mwenyekiti kuwa mzito kupokea ushauri kutoka kwa wasaidizi wake anaoona kawazidi umri ingawa kasoro hili inaweza ikawa haionekani kirahisi machoni pa watu.
Tofauti hujitokeza pale tu panapokuwa na mtoto anaependwa na baba (kiongozi) maana anaependwa siku zote husikilizwa na kuaminiwa na mzazi wake hata kama yeye ni mtoto na hata ushauri wake mara nyingi huzingatiwa kuliko wa watoto wengine ila hapo sasa iwe bahati tu mtoto mwenyewe anaependwa nae awe na akili vinginevyo ni majanga.
Ukweli ni kuwa, kwa mila na desturi zetu, ni rahisi kwa watu wa rika moja kushauriana na anaeshauriwa akawa tayari kupokea ushauri anaopewa kuliko ilivyo kwa watu wa rika tofauti hasa pale mmoja(mshauriwa) anapokuwa katika rika la baba na mshauri anpokuwa katika rika la mtoto(mmoja kiumri ni kama baba na mwingine ni kama mtoto)
Tatizo huwa kubwa zaidi pale boss wako huyo wa rika la baba yako anapokuwa mkali/hashauriki na anajisahau kabisa kuwa yupo kazini na kwamba anadili na mambo ya kiofisi na huyo anaemshauri ni msaidizi wake na wala si mwanafamilia wake.
Nayasema haya kwasababu inawezekana kabisa baadhi yao kutokana na kupishana sana umri na kiongozi wao mkuu(mwenyekiti) kunawagharimu wanapotoa ushauri kuliko wale walio sawa au karibu sawa kiumri na mwenyekiti.
Vile vile tusisahau pia kuna watu wana kasumba ya kupenda zaidi kusikiliza na kuamini ushauri au mawazo ya watu wanaolingana nao kielimu au wale wanaowazidi wakiamini mtu mwenye elimu kama yake au kumzidi ndio ana mawazo mazuri kuliko yule mwenye shule ndogo kitu ambacho si kweli.
Hali hii japo haionekani lakini huenda ipo na ni chanzo kimojawapo cha matatizo tunayoyaona katika kijiji chetu.
Ni mtazamo tu.