Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Pamoja na kufundishwa kwamba historia ni tunu inayotuonyesha tulikotoka, tulipo na tunakoelekea, pia hutupa mantiki ya wakati na matukio mbalimbali yanayojitokeza katika jamii.
Kwa muktadha huo nimejaribu kuchunguza na kugundua kwamba Mhe.Jakaya Kikwete alikuwa na wakati mzuri pia mahusiano mazuri na raia wote wakiwemo wapinzani.
1. Miezi saba ya awali ya awamu ya kwanza, Mhe. Jakaya Kikwete alikuwa bado ana mvuto mkubwa kwa wananchi jambo lililowapa wakati mgumu wapinzani kwenda kinyume nae kwa maana alikuwa akiwaheshimu na wao walikuwa wakimheshimu japokuwa baadaye mambo yalienda mrama kidogo na hatimaye kundi kubwa la wakosoaji wa utawala wake likaibuka.
KWANINI MHE. KIKWETE ALIJIKWAA KISIKI CHA KUANZA KUKOSOLEWA NA HATIMAYE IMANI YA WANANCHI KUPUNGUA JUU YAKE?
Sababu kubwa inayotajwa ni kwamba Mhe. Kikwete aliangushwa na wana mtandao wenzake waliompigania kuingia ikulu jambo lililopelekea wakati mwingine kuwalipa fadhila badala ya kuzingatia katiba, sheria, kanuni na taratibu za nchi hivyo alitajwa mara kadhaa kukumbatia ufisadi.
Pamoja na hayo yote, tunu kubwa inayofanya Watanzania wamkumbuke alikuwa na kifua kipana cha kukubali kukosolewa na kuyafanyia kazi maoni mengi ya wapinzani kwa maslahi ya nchi.
2. Miezi saba ya Mhe. Rais John Magufuli imekuwa na tofauti kubwa hususani katika muktadha wa kidemokrasia. Pamoja na Rais Magufuli kufanya vema katika kudhibiti rushwa, ufisadi, uhujumu uchumi, nidhamu kwa watumishi wa umma na mengineyo; Rais Magufuli amekuwa mwiba kwa demokrasia ya vyama vingi na uhuru wa kujieleza.
Sasa wadadisi wa mambo ya kisiasa na wachunguzi wa mambo wameanza kuweka bayana juu ya udhaifu mkubwa wa serikali ya awamu ya tano. Serikali inayotaka kusifiwa bila kukosolewa. Inakuwaje, serikali yenye kutenda mema kwa wananchi inawaogopa wapinzani wakati tumesikia kwamba kwa kuwa serikali inatenda mema kwa raia basi wapinzani hawana hoja?