Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Wakuu, nchi yetu ya Tanzania inaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi kwa miaka takribani 25 sasa. Kwa upande wa upinzani, CHADEMA na CUF vimekuwa vyama vikubwa vya upinzani kwa muda mrefu sana.Hili ni kheri.
Agenda kubwa ya vyama vya upinzani imekuwa ni kuwaletea wananchi maendeleo mazuri bila kujali ukabila, udini na uvyama.Sasa basi, hivi vyama vya upinzani vimekuwa vikiongoza majimbo mbalimbali hapa nchini kupitia uchaguzi mkuu. Bunge limekuwa na wabunge wa upinzani wengi tu, karibu wabunge sabini (70) na pia vyama vyao vimekuwa vikipata ruzuku toka serikalini, watu binafsi wa ndani na nje ya nchi.
Katika swala zima la maendeleo, maeneo (majimbo,halmashauri,majiji) yanayoongoza na aidha CCM au Upinzani, nini tofauti ya kimaendeleo intems of:
1. Upatikanaji wa maji safi na salama
2. Huduma za afya, shule
3. Upatikanaji wa ajira kwa vijana
4. Kuwaunganisha wakulima na kukuza kilimo
5. Mikopo kwa vikundi vya ujasiliamali
6. Miundombinu ya barabara, umeme nk?
Kuna haja ya kuwa na CCM au Upinzani? Isije ikawa watu wanapiga dili tu lakini huko walikoshika majimbo hakuna lolote.