chimela
Member
- Jul 14, 2016
- 63
- 142
Maisha ya jana na leo yanatofautiana tarehe tu
Tunalazimika kuandika mengi kuhusu serikali hasa yale ya kuikosoa kwa kiwango kikubwa serikali. Sio kwamba mazuri yanayofanywa na serikali hayapo,La hasha yapo na ni mengi. Hatukosoi kwa kutaka kupata political popularity na hatunufaiki wala hatulipwi chochote tunapoikosoa serikali inapokosea. Tunaikosoa serikali kwa kuionyesha mapungufu yote ambayo yanatakiwa kutiliwa mkazo ili leo na kesho zisitofautiane tarehe tu, hata unafuu wa maisha unatakiwa utofautiane. Moja ya watu waliolijenga kwa ufasaha neno demokrasia duniani Bwana Robert Dahl aliwahi kuandika kwamba "Demokrasia ni pale ambapo kundi kubwa la watu linatea kipande kidogo cha miongoni mwao kuweza kusimamia maslahi ya kundi zima". Hii inamaanisha ni lazima wale wachaguliwa au wateule hao wasimamie kwa kiwango kikubwa maslahi ya kundi kubwa wanalowakilisha. Mapinduzi ya kidemokrasia yamefanya watu wengi waweze kuomba nafasi ya kuwakilisha kundi kubwa kwa minajiri ya kuwakilisha misimamo chanya ya kundi kubwa. Tanzania ni taifa ambalo lina mwelekeo wa siasa za kiliberali ambazo kwa kiwango kikubwa zimetufikisha hapa tulipo.Siasa zilizojaa rafu nyingi, figisu nyingi ,Rushwa iliokithiri na hata Wizi mkubwa wa kura na machafuko kwenye baadhi ya maeneo. Sasa tafsiri halisi ya demokrasia inapoteza maana yake ambayo ilitakiwa itumiwe na watawala kuwawakilisha watu wao. Viongozi wengi hawaoni umuhimu wa dhamana waliopewa na watu wao, Hawaoni majukumu waliopewa kama dhamana. Mtukufu anasimama hadharani na kusema kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe wakati yeye na serikali yake wameshindwa kuubeba mzigo wao wenyewe. Miundombinu ilioharibiwa na Tetemeko imejengwa kwa pesa za misaada lakini serikali haijaona sababu za kuwasaidia wahanga. Dalili za njaa kulikumba taifa kwa miezi 16 ijayo hazijachukuliwa kwa uzito unaotakiwa. Bado mtukufu haoni umuhimu wa kuliondoa taifa na watu wake kutokana na baa hilo. Utetezi mkubwa ni kwamba eti watu hawakutunza chakula cha kutosha. Ni uhaba mkubwa wa maarifa kuamini kwamba serikali iliowekwa na watu kukwepa majukumu ambayo ni lazima iyabebe iwe inataka au haitaki. Wapinzani tunatukanwa kwamba tumegeuza swala la njaa kama ajenda ya kisiasa. Ni ufinyu mkubwa wa mawazo,Njaa haitawapiga wa Chadema na Ukawa pekee njaa itawapiga Watanzania wote bila kujali chama. Kama kawaida ya Tanzania tumezoea matatizo yatokee ndiyo tuanze kuchukua hatua wakati muda wa kuzuia tatizo tunao wa kutosha. Hakuna mtu anaetakiwa kuombewa wala taifa halitakiwi kuombewa na mtu yoyote yule. Ukame ni janga la asili ambalo halitatatuliwa kwa kumuombea mtu fulani au kuliombea taifa, ni lazima tutumie njia zozote zile kukwepa kukumbana na hali hii ambayo kuna uwezekano ikawakuta watanzania wengi. Ni viongozi wachache sana duniani wanaofurahia Inflation(Kupanda kwa bei za bidhaa). Jpm anafurahia kuona bei za mazao zinapanda eti kisa tu wakulima walilima kwa nguvu zao. Kuna vitu vinachekesha huku machozi ya uchungu yakitoka, Hivi hii kauli ilitakiwa kutolewa na Mtu kama yeye? Na wajinga walio wengi walishangilia kauli hio. Debe la mahindi kwa mikoa ya Songwe na Mbeya ina range kati ya 15,000 -18,000 bei ambayo haijawahi kutokea tokea Tanganyika imekua huru mwaka 1961 na mikoa hio ndiyo imekua leading food crop producers nchini, lakini Mheshimiwa bado hashangazwi na hali hio.Pesa imekua adimu kwenye mzunguko bado wakubwa tuliowachagua hawaoni nafasi yao katika kuirudisha hali ya kiuchumi katika hali yake ya kawaida. Kwa mwezi huu wa kwanza shilingi ya kitanzania imeporomoka thamani yake kwa kasi ya ajabu lakini hakuna dalili zote zinazoonyesha serikali inapigana kuiwezesha shilingi iimarike.Tunaishi na uchumi ambao sio viongozi tu hata Watanzania wenyewe hatujui kama ni demand side economy au Supply side Economy.Kama Taifa Tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuongeza idadi kubwa ya wafungwa wa kisiasa hata kama hawana makosa yenye tafsiri pana kisheria. Tumeweza kwa kiwango kikubwa kuvitishia vyombo vya habari ambavyo kwa kiwango kikubwa vimekua muhimili pekee unaofichua kwa kiwango kikubwa uhalifu na madudu yanayopatikana ndani ya serikali na nje ya serikali. Tujivunie utanzania wetu kwa kuamini kwamba habari za magazeti na mitandaoni ndiyo zinazozuia kwa kiwango kikubwa tusitoke hapa tulipo.Kama bado watu wanaamini CCM iliotufikisha hapa tulipo ndio itatutoa hapa tulipo wanajidanganya wenyewe. Kila baada ya uchaguzi kupita tutaendelea kuamini kua bora raisi aliepita kuliko wa sasa.
Drastic times calls for Drastic Measures