Tofauti ya asili ya kijinsia. Siasa isifos tufanane

Zambotti

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,639
2,000
Salam sana wandugu, matumaini yangu mko poa.

Hiki ni kipande cha maandishi kutoka kwenye kitabu cha Why Men Cant Listen, And Why Women Cant Read Maps kilichoandikwa na mwandishi Allan Pease na mkewe Barbara Pease.
Tafsiri ni ya kwangu mwenyewe.


Makubaliano ya ubaguzi wa kijinsia

Tangu mwishoni mwa miaka ya 1980s, kulikuwa na mlipuko wa tafiti katika kuangazia tofauti ya kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke na tofauti ya ufanyaji kazi wa akili zao. Kwa mara ya kwanza kabisa, kifaa cha kompyuta kilichoboreshwa katika kupima ufanyaji kazi wa ubongo kilitupa nafasi kushuhudia mfumo wa ufanyaji kazi wa ubongo kwa ukaribu na kujionea kile kiwango cha juu cha utendaji wa ubongo wa mwanadamu, ilitoa majibu mengi ya maswali kuhusu tofauti ya mwanaume na mwanamke. Utafiti unaozungumzwa katika kitabu hiki umekusanywa kutoka kwenye vyanzo tofauti tofauti ikiwemo sayansi ya tiba,saikolojia na vyanzo vya sayansi ya sosholojia na vyote vinaelekeza nguvu katika sehemu moja inayofanana, nayo ni: vitu vyote haviko sawa; wanaume na wanawake pia wako tofauti.

Katika karne ya 20 tofauti ya mwanaume na mwanamke ilikuwa ikielezewa kwa kuzingatia hali zao za kijamii; kwamba, tupo hivi tulivyo kwasababu ya hali ya wazazi na waalimu wetu, ambazo mrejesho wake unaathiri hali ya jamii zao. Watoto wa kike walivalishwa nguo za pinki na walipewa vinyago na madoli ya kuchezea; watoto wa kiume walivalishwa nguo za buluu na midoli ya kijeshi, mipira na jezi za mpira kuchezea. Wasichana walibembelezwa na kuliwazwa na wazazi wao wakati wavulana walisuguliwa na kupigwa pigwa mgongoni na kuambiwa waache kulia. Mpaka sasa, ilikuwa inaaminika kwamba pindi mtoto anapozaliwa akili yake inakuwa ni kama daftari lililoachwa wazi ambako mwalimu wake atakuja aandike mapendekezo na machaguo yake. Kwa sasa ushahidi wa kibaolojia unapatikana, hata hivyo, inaonyesha ni kwaa jinsi gani mwanadamu anawaza au anafikiri kwa jinsi vile anavyofikiria. Inaonyesha kwa ushawishi mkubwa sana kwamba ni mpangilio wa homoni na ubongo ndio unaohusika na hali zetu, machaguo yetu na tabia zetu. Hivyo basi, kama mwanaume na mwanamke watakua kwenye kisiwa kilichotelekezwa jangwani peke yao bila ya muongozo wa jamii au wazazi wao, mwanamke bado atapendelea kubembelezwa, kuwa na marafiki na kucheza na madoli wakati mwanaume ataendelea kupambana kimwili na kiakili na kila mtu na kuhakikisha anatengeneza makundi yenye mpangilio wa matabaka ya nyanja mbalimbali. (mwisho)

Kwasasa dunia iko busy kuhakikisha unaletwa usawa na utangamano wa kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke kitu ambacho si sawa. Mwanamke hata awe na mamlaka ya kiasi gani bado mwanaume ndio atabaki kuwa kiongozi na mpiganaji wa mstari wa mbele katika mapinduzi ya kidunia na ustawa katika jamii. Haya mambo tusiyalazimishe ni vitu viwili visivyofanana kabisaa, bado hatujachelewa twendeni turudi kwenye asili yetu.

Wasalam!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom